The Burning Spear
JF-Expert Member
- Dec 23, 2011
- 9,111
- 21,984
WAJALUO WAMETANGULIA CHATO?!
Kesho 17/3/2025 inatimia miaka 5 ya kumlilia hayati Rais JPM. Kimsingi, siyo “maadhimisho” ya miaka 5 bila. Hatuna cha kuadhimisha; tuna cha kulilia. Hata ambao “hawakumpenda” wanamlilia sambamba na waliompenda.
Viongozi wetu wako njiani kwenda Chato. Nimesikia Rais Hussein Mwinyi, Makamu wa Rais Nchimbi, Waziri Mkuu Mwigulu, Makamu wa Rais Mstaafu, Waziri Mkuu Mstaafu Majaliwa, Mtani wangu, “Mfalme wa Bunda” Mzee Wasira na wengine watakuwepo. Karibuni sana Chato. Mimi niliishi na kusoma Chato S/M. Lakini pia….
1. Nimesikia kuna Wajaluo wametangulizwa Chato kwenda kufanya siasa za kitoto. Bajameni, Chato siyo St. Joseph.
2. Nasikia wanataka kuwagawa viongozi wetu kwa kuwapigia makofi ya bandia ili kufunika makofi ya kweli yatakayopigwa.
3. Nimesikia wanajaribu kuingilia itifaki za kanisa na za familia. Wao kila kusanyiko ni siasa! Punguzeni wasemaji. Waliobaki toeni machozi tuone mlivyompenda JPM. Inatosha na kubaki. Wajaluo bhana!
4. Napenda niwakumbushe haya:
i) Hayati JPM alikuwa hatumi mtu; alijituma mwenyewe. Mliotuma Wajaluo, kwa nini msiende wenyewe.
ii) Hayati JPM alikuwa tayari kupendwa na kuchukiwa pia. Nyie mnataka kupendwa tu. Ebo! Mbataka kula tu bila ku…(Mwombeni mtani wa JPM awashauri).
iii) JPM alikuwa anakemea rushwa. Siku hizi rushwa inakemea viongozi.
iv) Hayati JPM hakukubali kuchonganishwa na wananchi. Viongozi wetu wanajichonganisha wenyewe. “Spinning” ni nyingi kuliko umaskini wetu. Semeni kweli mpone na taifa lipone.
v) Hayati JPM alikuwa mgeni kwenye eneo la Haki za Binadamu. Viongozi wetu hata kuzisikia zinawakera.
5. Hayati JPM hakupatanishwa kirahisi lakini aliwaheshimu wapatanishi. Tunaelekea kuwatumia wasiopatanishwa ili wafanye upatanisho/maridhiano.
Narudia tena:
Maridhiano ya taifa letu, sehemu kubwa hayahitaji vikao, meza, wala posho. Ni maamuzi yanayozingatia ukweli, haki na uwajibikaji.