Battle: Magufulians vs Anti-Magufuli

Aliheshimu Demokrasia
Chaguzi zilikuwa za Haki na Huru
Wapinzani Walifanya Mikutano yao bila KAMATA kamata ya Polisi
Wabunge 19 Wasio kuwa na Chama Walivuliwa Ubunge Wao


Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
Magufuli was the best EVER president R. I P . Upembuzi wa Kadogosa unaonesha mzee JPM alikuwa mfanyakazi c mwanasiasa wa porojo za majukwaa anayetaka haki za mashoga na haki za wafungwa waitwe wanafunzi
 
Magufuli was the best EVER president R. I P . Upembuzi wa Kadogosa unaonesha mzee JPM alikuwa mfanyakazi c mwanasiasa wa porojo za majukwaa anayetaka haki za mashoga na haki za wafungwa waitwe wanafunzi
Mpaka leo timu Msoga nadhani wameanza kuelewa hasara tuliyopata kama taifa kwa kumpoteza Magufuli.
 
Magufuli was the best EVER president R. I P . Upembuzi wa Kadogosa unaonesha mzee JPM alikuwa mfanyakazi c mwanasiasa wa porojo za majukwaa anayetaka haki za mashoga na haki za wafungwa waitwe wanafunzi
Unaanzaje kumlinganisha Maghufuli na taka taka zilizopo sasa hv , wanamkosea heshima Sana
 
Nakumbuka time ile wenyewe walishakubali ile speed yetu kila siku wanaletewa multibillions projects, wao walibaki na white elephants projects zao , mpaka alipokufa magu nikawa nikipita kule roho inaniuma sana
Ni kweli speed imepungua ila bado tunawatesa na miradi ile ile aliyoanzisha mwamba.
 
Ni kweli speed imepungua ila bado tunawatesa na miradi ile ile aliyoanzisha mwamba.
Bro nina kumbukumbu zako since march 2021, kuna comment ulisema hivi

" KATI YA WATU 10 WALIOKUA WANAMCHUKIA MAGUFULI,

-WATANO WANAMCHUKIA KWA MKUMBO.
  • 3 HAWAJUI KWA NINI WANAMCHUKIA.
  • 2 NI UPINZANI UCHWARA."
Screenshot hyo hapo

Screenshot_2021-03-21-09-41-21.jpg
 
Habari zenu wanajukwaa, baada ya kugundua kuwa mtu huyu imeshindikana kabisa kusahaulika ndani ya mioyo ya Watanzania na wasio Watanzania nimeona nianzishe uzi ambao utagusa pande zote yani wale wanaodhani alikuwa Rais bora na wale wanaodhani hakuwa Rais bora.

Ikumbukwe kwamba tangu amefariki mtu huyu imepita takribani miezi sita na siku kadhaa mpaka hapa ninapoandika huu uzi, sasa naomba wale Magufulians waseme kwanini wanadhani huyu alikuwa Rais bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania na watoe sababu za kusema hivyo pia wale wanaodhani hakuwa Rais bora watoe sababu zao.

Ndugu zangu nimelazimika kuanzisha huu uzi kutokana na kile ninachokiona kwamba jina la Magufuli sasa limekuwa kama dini mana unapomponda tu kama pembeni yako kuna mfuasi wake basi hawezi kukuacha salama.

Hii imepelekea kutokea mikanganyiko na sintofahamu kwenye majukwaa mbalimbali inafikia kipindi unakuta mada haihusiani na Magufuli lakini uzi unaharibika kwa sababu ya u-Magufuli vs u-Anti Magufuli.

Sasa ndugu zangu tusiendelee kuharibu nyuzi za watu, kama una dukuduku lako kuhusiana na kiongozi huyu mashuhuri aliyewahi kuongoza Tanzania basi weka hapa dukuduku lako au maoni yako juu ya mwamba huyu yaweke hapa jamii ifahamu ni kwa namna gani kiongozi huyu alikuwa mzuri au mbaya.

Nianze na mimi binafsi msimamo wangu juu ya JPM, ni kwamba namuona kama Icon na benchmark ya viongozi waliopo na watakaokuja kwasababu zifuatazo


1. Muanzilishi wa Tanzania mpya. JPM alikuwa kiongozi mwenye uthubutu wa kuwakaripia viongozi wote walio chini yake kwa mamlaka aliyopewa kikatiba iwe ni viongozi wa kuteuliwa na yeye mwenyewe au wa kuchaguliwa basi viongozi walitii, ilikuwa ni utaratibu kwa viongozi wa Tanzania waliochini ya Rais kikatiba kujiamulia mambo watakavyo wao ikibidi hata kukaidi maagizo yanayotolewa na Rais, hii ilipelekea huko nyuma nchi yetu kupoteza muelekeo lakini chini ya JPM maagizo yakawa yanafuatwa na kasi ya utendaji ikawa kubwa kuwahi kutokea Tanzania.

2. Kiongozi mkweli daima. Mtu huyu alikuwa ni moja kati ya binadamu wachache wakweli, alikuwa mwanasiasa pekee asiyejuwa kuongopa, ilifika mahali akajiingiza kwenye mgogoro na wanasiasa wenzake ndani ya CCM kwakuwa wengi wao hawakuzoea ukweli, JPM akisema hili hapana basi juwa kwamba halitatokea au akisema hili linawezekana basi juwa hivyo, hakuwa mtu wa kupepesa macho, alikuwa na uwezo wa kuongea ukweli hadharani pasipo kuficha ficha kitu chochote, hii ikapelekea viongozi waliokuwa wanaendekeza siasa majitaka kumuogopa kwani mzee yule hakuwa akijali kama unatokea CCM au upinzani.

3. Msimamo mkali. Chini ya JPM tuliona Tanzania yenye msimamo na isiyoyumbishwa na mtu yeyote au taifa lolote lile liwe na uchumi mkubwa au mdogo, hii ikapelekea Tanzania kufahamika zaidi kimataifa na duniani kote.

4. Kiongozi mwenye maono. Hayati JPM alikuwa ni kiongozi mwenye maono, hili liko wazi kwani maono yake hasa kwenye nyanja za kiuchumi ndio zikapelekea nchi yetu kuingia uchumi wa kati kabla ya muda uliokusudiwa, hii ilitokana na maono na jitihada zake kuhakikisha nchi yetu inajitegemea kwa kuanzisha miradi iliyoonekana haiwezekani lakini chini ya uongozi wake ikawezekana, pia maono yake yalijidhihirisha hata kwenye ugonjwa ulioikumba dunia kwa sasa ugonjwa wa Corona, nchi nyingi duniani zimeanza kutumia theories alizozitoa Hayati JPM.

5. Kiongozi mwenye ushawishi. Hayati JPM alikuwa na karama ya ushawishi mbele ya jamii, alikuwa na uwezo wa kusema jambo fulani na jamii nzima ikakubaliana naye kwa asilimia kubwa, kiukweli kabisa hata leo hii JPM akiamka na akasema watanzania wachanje basi believe me dawa za kuchanja hazitatosha, hii ni kutokana na imani kubwa aliyojiwekea mbele ya jamii kwakuwa watanzania waliamini kwamba JPM ana upendo wa dhati kwa wananchi wake na hawezi kuwarubuni kwa namna yoyote ile.

6. Mtu wa Mungu. Licha ya mapungufu yake kibinaadamu lakini ni ukweli usiopingika kwamba JPM alikuwa ni mtu wa Mungu, siku zote za uongozi wake hakuacha kumtegemea Mungu na hili alilifanya hadharani kwa kumtaja Mungu popote alipoenda na watu wake wakaribu wanasema mzee yule ulikuwa ni utaratibu wake kumtanguliza Mungu mbele.

7. Kipenzi cha wengi. Ukiacha mitandao ambao kuna wachache wanaomsema vibaya Magufuli ni dhahiri shairi kwamba hayati alipendwa na wengi, hii ilijidhihirisha pale alipofariki, umati uliojitokeza haukuwahi kutokea na sidhani kama utatokea kwa siku za karibuni, sio kwamba walioenda kumuaga walienda kukejeli bali waliguswa haswa, vilio kila pembe ya waagaji na kila sehemu mwili ulipoenda, hii inathibitisha ni jinsi gani watanzania walimpenda kiongozi wao.

Yako mengi ya kumuelezea Magufuli lakini itoshe kwa haya niliyoyaandika kumuelezea, mengine niwaachie ninyi wenzangu karibuni.
Ukiona hunachakuonge wew tukanatu nayo ni point
 
Binafsi mwanzo alivyoingia madarakani ki ukweli kabisa sikumpemda nikawa nasema huyu ni Rais gani mbona mmbabe lkn baada ya mwaka mmoja ki ukweli nilimpenda bure nilimwelewa sana..

Kilichonifanya nimwelewe ni haki sawa kwa wote. Wenye nacho na wasiokuwa nacho. Ni kweli binadamu hatuwezi kuwa sawa kwenye suala zima la kipato kikubwa wapo wenye vidogo bali sote ni binadamu heshima iwepo. Unaenda kupata huduma anaangaliwa yule mwenye nacho wewe usiyenacho unasubiri benchi.

Ukipelekea kesi yako polisi anayesikilizwa na kuaminiwa ni yule mwenye pesa. Kipindi cha utawala wake hayo hayakuwepo una hela basi uwe na nidhamu na pesa zako.

Japo kila binadamu ana mapungufu yake,, yalikuwa machache kuliko mazuri aliyofanya. Mungu amrehemu kule aliko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom