jamaa alikua bingwa wa kupika data,hivi Kwa akili zako timamu Kuna mchumi enzi zake angeweza kwenda kinyume na jiwe Kwa kutoa taarifa za kweli?
Apike data wapi wakati mambo yapo hadharani kabisa.
Tunaona flyovers ambazo hatujawahi kuziona tangu uhuru.
Tunaona reli ya umeme ambayo ilikuwa ni ndoto, tangu uhuru hakuna rais aliyejenga hata sentimita moja ya reli.
Tunaona bwawa kubwa la umeme ambapo marais wote waliofuatia baada ya Nyerere hakuna aliyethubutu kujenga hata kisima ili atuzuge kuwa alikuwa na lengo la kujenga bwawa la umeme.
Tunaona ndege mpya, hivi tunavyoongea kuna chuma kingine kinaitwa Tanzanite ni brand new Airbus, kwa hapa Afrika ni nchi mbili tu ndio tunazo.
Tunaona madaraja ya kisasa kabisa, tena ni cable stayed bridges ambazo mpk ss hapa East and Central Africa ni Tz tu ndio tunayo ukiachilia uganda ambao nao wamejitutumua kdg.
Tunaona barabara za viwango hata kama zimejengwa na Mayanga construction company lkn ni za viwango, huko nyuma tulishuhudia barabara zilizojengwa na chinese construction companies lkn mwaka mmoja tu barabara kwisha.
Tunaona meli kubwa mpya zikijengwa hapa hapa Tanzania, tangu uhuru ni Magufuli na Nyerere tu ndio waliowahi kununua meli.
Tunaona Airports, Ports, vituo vya afya vya kisasa mpk uswahilini plus barabara za lami mpk Yombo uswazi.
Tunaona...... au wacha nisiendelee mana ni mengi hata wewe unajua, sasa niambie hzo data zilizopikwa ziko wapi [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]