Battle: Magufulians vs Anti-Magufuli

The best 007

JF-Expert Member
Oct 6, 2019
37,832
82,367
Habari zenu wanajukwaa, baada ya kugundua kuwa mtu huyu imeshindikana kabisa kusahaulika ndani ya mioyo ya Watanzania na wasio Watanzania nimeona nianzishe uzi ambao utagusa pande zote yani wale wanaodhani alikuwa Rais bora na wale wanaodhani hakuwa Rais bora.

Ikumbukwe kwamba tangu amefariki mtu huyu imepita takribani miezi sita na siku kadhaa mpaka hapa ninapoandika huu uzi, sasa naomba wale Magufulians waseme kwanini wanadhani huyu alikuwa Rais bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania na watoe sababu za kusema hivyo pia wale wanaodhani hakuwa Rais bora watoe sababu zao.

Ndugu zangu nimelazimika kuanzisha huu uzi kutokana na kile ninachokiona kwamba jina la Magufuli sasa limekuwa kama dini mana unapomponda tu kama pembeni yako kuna mfuasi wake basi hawezi kukuacha salama.

Hii imepelekea kutokea mikanganyiko na sintofahamu kwenye majukwaa mbalimbali inafikia kipindi unakuta mada haihusiani na Magufuli lakini uzi unaharibika kwa sababu ya u-Magufuli vs u-Anti Magufuli.

Sasa ndugu zangu tusiendelee kuharibu nyuzi za watu, kama una dukuduku lako kuhusiana na kiongozi huyu mashuhuri aliyewahi kuongoza Tanzania basi weka hapa dukuduku lako au maoni yako juu ya mwamba huyu yaweke hapa jamii ifahamu ni kwa namna gani kiongozi huyu alikuwa mzuri au mbaya.

Nianze na mimi binafsi msimamo wangu juu ya JPM, ni kwamba namuona kama Icon na benchmark ya viongozi waliopo na watakaokuja kwasababu zifuatazo

1. Muanzilishi wa Tanzania mpya. JPM alikuwa kiongozi mwenye uthubutu wa kuwakaripia viongozi wote walio chini yake kwa mamlaka aliyopewa kikatiba iwe ni viongozi wa kuteuliwa na yeye mwenyewe au wa kuchaguliwa basi viongozi walitii, ilikuwa ni utaratibu kwa viongozi wa Tanzania waliochini ya Rais kikatiba kujiamulia mambo watakavyo wao ikibidi hata kukaidi maagizo yanayotolewa na Rais, hii ilipelekea huko nyuma nchi yetu kupoteza muelekeo lakini chini ya JPM maagizo yakawa yanafuatwa na kasi ya utendaji ikawa kubwa kuwahi kutokea Tanzania.

2. Kiongozi mkweli daima. Mtu huyu alikuwa ni moja kati ya binadamu wachache wakweli, alikuwa mwanasiasa pekee asiyejuwa kuongopa, ilifika mahali akajiingiza kwenye mgogoro na wanasiasa wenzake ndani ya CCM kwakuwa wengi wao hawakuzoea ukweli, JPM akisema hili hapana basi juwa kwamba halitatokea au akisema hili linawezekana basi juwa hivyo, hakuwa mtu wa kupepesa macho, alikuwa na uwezo wa kuongea ukweli hadharani pasipo kuficha ficha kitu chochote, hii ikapelekea viongozi waliokuwa wanaendekeza siasa majitaka kumuogopa kwani mzee yule hakuwa akijali kama unatokea CCM au upinzani.

3. Msimamo mkali. Chini ya JPM tuliona Tanzania yenye msimamo na isiyoyumbishwa na mtu yeyote au taifa lolote lile liwe na uchumi mkubwa au mdogo, hii ikapelekea Tanzania kufahamika zaidi kimataifa na duniani kote.

4. Kiongozi mwenye maono. Hayati JPM alikuwa ni kiongozi mwenye maono, hili liko wazi kwani maono yake hasa kwenye nyanja za kiuchumi ndio zikapelekea nchi yetu kuingia uchumi wa kati kabla ya muda uliokusudiwa, hii ilitokana na maono na jitihada zake kuhakikisha nchi yetu inajitegemea kwa kuanzisha miradi iliyoonekana haiwezekani lakini chini ya uongozi wake ikawezekana, pia maono yake yalijidhihirisha hata kwenye ugonjwa ulioikumba dunia kwa sasa ugonjwa wa Corona, nchi nyingi duniani zimeanza kutumia theories alizozitoa Hayati JPM.

5. Kiongozi mwenye ushawishi. Hayati JPM alikuwa na karama ya ushawishi mbele ya jamii, alikuwa na uwezo wa kusema jambo fulani na jamii nzima ikakubaliana naye kwa asilimia kubwa, kiukweli kabisa hata leo hii JPM akiamka na akasema watanzania wachanje basi believe me dawa za kuchanja hazitatosha, hii ni kutokana na imani kubwa aliyojiwekea mbele ya jamii kwakuwa watanzania waliamini kwamba JPM ana upendo wa dhati kwa wananchi wake na hawezi kuwarubuni kwa namna yoyote ile.

6. Mtu wa Mungu. Licha ya mapungufu yake kibinaadamu lakini ni ukweli usiopingika kwamba JPM alikuwa ni mtu wa Mungu, siku zote za uongozi wake hakuacha kumtegemea Mungu na hili alilifanya hadharani kwa kumtaja Mungu popote alipoenda na watu wake wakaribu wanasema mzee yule ulikuwa ni utaratibu wake kumtanguliza Mungu mbele.

7. Kipenzi cha wengi. Ukiacha mitandao ambao kuna wachache wanaomsema vibaya Magufuli ni dhahiri shairi kwamba hayati alipendwa na wengi, hii ilijidhihirisha pale alipofariki, umati uliojitokeza haukuwahi kutokea na sidhani kama utatokea kwa siku za karibuni, sio kwamba walioenda kumuaga walienda kukejeli bali waliguswa haswa, vilio kila pembe ya waagaji na kila sehemu mwili ulipoenda, hii inathibitisha ni jinsi gani watanzania walimpenda kiongozi wao.

Yako mengi ya kumuelezea Magufuli lakini itoshe kwa haya niliyoyaandika kumuelezea, mengine niwaachie ninyi wenzangu karibuni.
 
Umeandika vyema. Hakika huyu alikuwa kipenzi cha watu na ninathubutu kusema MAGUFULI ndiye kiongozi bora Tanzania kuwahi kushuhudia na yote aliyoyatenda ameyatenda katika kipindi cha miaka sita tu! Tofauti na wengine,Sasa fikiria angemaliza miaka yake 10 Tanzania ingekuwa wapi sasa?.Binafsi ninaona fahari kuishi katika zama za Magufuli Mungu akinijalia umri mrefu nitawasimulia vizazi vijavyo kuhusu mtu huyu! Hakika tumeona ukuu wa Mungu kupitia mtu huyu!

Itoshe tu kusema Bwana ametoa Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.
 
Kati ya watanzania wanne basi mmoja ana ugonjwa wa akili, sio maneno yangu bali ni data za wizara ya afya pamoja na NBS.

11215697_1167859589910086_8793861981273459784_n.jpg
 
Shujaa wa kweli wa Watanzania wanaojitambua. Ni aibu kubwa sana kwa Kiongozi wa Tanzania kwenda kujikomba komba huko nje na kutafuta umaarufu na kuwatukuza walio na ngozi nyeupe, ni aibu kubwa sana.

JPM ndiye mwanzilishi wa kujitegemea kwa vitendo kuanzia pesa za uchaguzi mkuu, kujenga mahospitali kila kona, kuwezesha umeme kumfikia kila Mtanzania, na mengineyo mengi.

RIP JPM. Tutakukumbuka daima.
 
Magufuli alikuwa ni mchapa kazi, asiyevumilia uvivu, mwenye vision, na mwenye kujiamini na kuamini uwezo Wa ngozi nyeusi katika kujitegemea na kujisimamia.
A free minded person,
Angalau nchi yetu iliyokuwa underdog for years ilipata heshima iliyostahili na ilitajwa kote duniani.
Alikuwa too much agressive kwa upinzani and especially while dealing with mediocrity,
Hakupenda ujinga kama mimi nisivyopenda incompetency, uvivu na ujinga.

Hapa I can rank the best presidents Tangu tupate uhuru

1. Mwalimu JK Nyerere
2. John P Magufuli
3. Benjamin Mkapa
4. Ally Hassan Mwinyi
5. Jakaya Kikwete
6. Samia Suluhu Hassan

NB. Tunahitaji kiongozi kama Magufuli, Huku mtaani watu Wa kawaida ambao ni over 99% ya Watanzania they miss him big time,
Duniani hatudumu milele, Apumzike kwa Amani.
 
Alikua Mwizi aliyejificha kwenye kivuli Cha Uzalendo uchwara, Hii ilidhihirika pale alipokuwa waziri wa ujenzi baada ya kuchukua nyumba za Nation Housing maeneo ya upanga na Oysterbay na kuwapa ndugu,marafiki na hawara kwa janja janja za nyani
Yaani kiufupi ni alifoji document Kwa kuzuga kauza kumbe kajiuzia mwenyewe Kwa Bei ya maandazi!

Harafu Sasa alikataa kukaguliwa na CAG prof Assad upotevu wa zaidi ya Tsh trillion 1 zilizopotea kimagumashi na Kwa kutopitishwa na bunge,
Akamuundia zengwe CAG Kwa kumstaafisha chini ya kamati ya roho mbaya wakiongozwa na Kimbunga Jobo wa pale Makao Makuu ya Bunge!

Miradi ya Matrillion kupelekwa kijijini kwao Chato ikiwemo intanational airport ambapo haikuidhinishwa na bunge Wala kukaguliwa na mkaguzi Mkuu wa serikali yaani CAG

Naanza na hayo kwanza nakuja na povu la buku jero kumkandia Nduli Jiwe!
Keep waiting!
 
Hapendwi na nani, hebu kesho asubuhi toka hapo kwenye nyumba ya baba alafu sema kwa sauti Magu hapendwi alafu uone kichapo, pumbavu!!!
'Anapendwa' na uneducated class because they can't see past his propaganda and cooked statistics.

Ukweli ni kwamba ndani ya miaka 6 ya uongozi wake, GDP per capita imeongezeka by 30 USD, wakati chini ya miaka 10 ya Kikwete iliongezeka by 500+ USD.
 
Magufuli alikuwa ni mchapa kazi, asiyevumilia uvivu, mwenye vision, na mwenye kujiamini na kuamini uwezo Wa ngozi nyeusi katika kujitegemea na kujisimamia.
A free minded person,
Angalau nchi yetu iliyokuwa underdog for years ilipata heshima iliyostahili na ilitajwa kote duniani.
Alikuwa too much agressive kwa upinzani and especially while dealing with mediocrity,
Hakupenda ujinga kama mimi nisivyopenda incompetency, uvivu na ujinga.

Hapa I can rank the best presidents Tangu tupate uhuru

1. Mwalimu JK Nyerere
2. John P Magufuli
3. Benjamin Mkapa
4. Ally Hassan Mwinyi
5. Jakaya Kikwete
6. Samia Suluhu Hassan

NB. Tunahitaji kiongozi kama magufuli, Huku mtaani watu Wa kawaida ambao ni over 99% ya Watanzania they miss him big time,
Duniani hatudumu milele, Apumzike kwa Amani.
Shukran sana mkuu kwa uchambuzi mfupi uliotukuka.
 
Alikua Mwizi aliyejificha kwenye kivuli Cha Uzalendo uchwara,Hii ilidhihilika pale alipokua waziri wa ujenzi baada ya kuchukua nyumba za Nation Housing maeneo ya upanga na Oysterbay na kuwapa ndugu,marafiki na hawara kwa janja janja za nyani
Yaani kiufupi ni alifoji document Kwa kuzuga kauza kumbe kajiuzia mwenyewe Kwa Bei ya maandazi!

Harafu Sasa alikataa kukaguliwa na CAG prof Assad upotevu wa zaidi ya Tsh trillion 1 zilizopotea kimagumashi na Kwa kutopitishwa na bunge,
Akamuundia zengwe CAG Kwa kumstaafisha chini ya kamati ya roho mbaya wakiongozwa na Kimbunga Jobo wa pale Makao Makuu ya Bunge!

Miradi ya Matrillion kupelekwa kijijini kwao Chato ikiwemo intanational airport ambapo haikuidhinishwa na bunge Wala kukaguliwa na mkaguzi Mkuu wa serikali yaani CAG

Naanza na hayo kwanza nakuja na povu la buku jero kumkandia Nduli Jiwe!
Keep waiting!
Shukran mkuu kwa uchambuzi mzuri, nina maswali machache.

1. Hizo nyumba za NHC alizojimilikisha vipi una ushahidi wowote kwamba zipo chini ya familia ya JPM?

2. Muda halisi wa kustaafu CAG ni miaka mingapi?

3. Kwani miradi ya maendeleo ilipelekwa Chato pekee? Je Chato co Tz? Na vipi miradi ya maendeleo iliyopelekwa Dodoma au maeneo mengine unaiongeleaje haikupendelewa?
 
01: Magufuli alinunua nyumba ngapi yeye binafsi kati ya nyumba zaidi ya 8,000 alizosimamia uuzwaji wake? Je, sheria haikumruhusu kununua? Je, kama alitenda kosa kisheria, kwanini hakuna yeyote aliyemshitaki?

02: Magufuli amefanya maendeleo maeneo mangapi Tanzania? Je, Chato haipo Tanzania? Rais haruhusiwi kufanya maendeleo sehemu anayotokea?

03: Je, kuna Rais gani wa wakati wetu aliyependwa na wananchi kama Magufuli? Ni Rais gani wa wakati wetu aliyeeleweka kwa wananchi kama Magufuli?

Ni Rais gani mwingine wa wakati wetu aliyetegemewa na kupelekewa shida directly na wananchi wa kawaida kama Magufuli?

04: Ni Rais gani wa wakati wetu aliyesimamisha miradi mikubwakubwa kama Magufuli? Ni rais gani amesimamia ujenzi wa miundombinu kama Magufuli?

Ni Rais gani wa wakati wetu ameiongoza Tanzania kwa kujitegemea yenyewe kushinda Magufuli?

05: Kuna Rais gani mwingine aliyefanya ziara za ndani ya nchi na kujionea mwenyewe utendaji kazi, siyo kuletewa tu ripoti ofisini, kushinda Rais Magufuli?

06: Je, ni Rais gani wa wakati wetu amekiheshimisha kiti cha Urais na kukirudishia hadhi yake kuzidi Magufuli?

Magufulia ni Rais bora kabisa wa wakati wetu, itatuchukua muda sana kupata Rais mwingine bora na imara kama Magufuli.
 
Magufuli alikuwa ni mchapa kazi, asiyevumilia uvivu, mwenye vision, na mwenye kujiamini na kuamini uwezo Wa ngozi nyeusi katika kujitegemea na kujisimamia.
A free minded person,
Angalau nchi yetu iliyokuwa underdog for years ilipata heshima iliyostahili na ilitajwa kote duniani.
Alikuwa too much agressive kwa upinzani and especially while dealing with mediocrity,
Hakupenda ujinga kama mimi nisivyopenda incompetency, uvivu na ujinga.

Hapa I can rank the best presidents Tangu tupate uhuru

1. Mwalimu JK Nyerere
2. John P Magufuli
3. Benjamin Mkapa
4. Ally Hassan Mwinyi
5. Jakaya Kikwete
6. Samia Suluhu Hassan

NB. Tunahitaji kiongozi kama magufuli, Huku mtaani watu Wa kawaida ambao ni over 99% ya Watanzania they miss him big time,
Duniani hatudumu milele, Apumzike kwa Amani.
Umeongea vizuri sana mkuu. Hapo kwenye ranking yaani kama ulikuwa kichwani kwangu! Sema huyo namba sita nina uhakika miaka ya mbeleni huko ataporomoka mpaka 108th president!
 
Shukran mkuu kwa uchambuzi mzuri, nina maswali machache.

1. Hizo nyumba za NHC alizojimilikisha vipi una ushahidi wowote kwamba zipo chini ya familia ya JPM?

2. Muda halisi wa kustaafu CAG ni miaka mingapi?

3. Kwani miradi ya maendeleo ilipelekwa Chato pekee? Je Chato co Tz? Na vipi miradi ya maendeleo iliyopelekwa Dodoma au maeneo mengine unaiongeleaje haikupendelewa?
Naanza na no 3
Sikatai miradi kupelekwa Chato kimkakati ila napinga kwanini miradi mingi iliyopelekwa Kule Ina bajeti kubwa kuzidi uhalisia wa eneo
Kingine mingi ya miradi hiyo haikukaguliwa na mkaguzi Mkuu wa serikali wala haikupitishwa na bunge
Kingine kandarasi ya miradi hiyo haikuwekwa wazi Kama sheria inavyotaka kua tenda itangazwe na Wazabuni wajitokeze wagombee tenda kisheria ila maajabu ikapewa kandarasi Mayanga Construction ambayo Kwa tetesi inadai ni kampuni iliyokua na mkono wa Jiwe!

Hilo swala unalichukuliaje?
 
Alikua Mwizi aliyejificha kwenye kivuli Cha Uzalendo uchwara,Hii ilidhihilika pale alipokua waziri wa ujenzi baada ya kuchukua nyumba za Nation Housing maeneo ya upanga na Oysterbay na kuwapa ndugu,marafiki na hawara kwa janja janja za nyani
Yaani kiufupi ni alifoji document Kwa kuzuga kauza kumbe kajiuzia mwenyewe Kwa Bei ya maandazi!

Harafu Sasa alikataa kukaguliwa na CAG prof Assad upotevu wa zaidi ya Tsh trillion 1 zilizopotea kimagumashi na Kwa kutopitishwa na bunge,
Akamuundia zengwe CAG Kwa kumstaafisha chini ya kamati ya roho mbaya wakiongozwa na Kimbunga Jobo wa pale Makao Makuu ya Bunge!

Miradi ya Matrillion kupelekwa kijijini kwao Chato ikiwemo intanational airport ambapo haikuidhinishwa na bunge Wala kukaguliwa na mkaguzi Mkuu wa serikali yaani CAG

Naanza na hayo kwanza nakuja na povu la buku jero kumkandia Nduli Jiwe!
Keep waiting!
Wezi unawafahamu kweli? Wezi wana hisa zao huko Belgium na mijengo S.A na watoto wao wanakula maisha na route za kutosha China-Dubai!
 
Back
Top Bottom