haijalishi ni urefu gani na nimelijumuisha hilo kwenye reasoning yangu, haiwezekani kufanya miradi mingi mikubwa kwa wakati 1, kwa nini tusiwekeze rasili mali zote kwenye mradi mmoja mpaka mwisho i.e uishe kwa 100% halafu ndiyo tuanze na mwingine mkubwa tena? ndivyo hata wakoloni walivyojenga reli hawakujenga zote kwa mara moja walianza na ya tanga-moshi/arusha baada ya kukamilika wakahamia reli ya kati i.e kuunganisha dar na interior na ndiyo maana iliitwa central line dar-kgm/mwanza, baadaye ikaja reli iliyounganisha nachingwea na bandari ya mtwara na kulikuwa na mpango wa kuunganisha mbaba bay na bandari ya mtwara (mtwara corridor) lkn hii yote ni mipango ambayo inakwenda kwa awamu, kwamba unafanya mradi 1 unaukamilisha unavuta pumzi unafanya tathmini and then unaanza mwingine, sasa tanzagiza miradi mikubwa kila mahali kila siku unatangazwa mradi mpya na hakuna hata 1 unaokamilika, wanapata wapi muda wa kufanya tathmini ya mradi kama hata was worth it? kwa sababu siyo kila mradi una tija na ndiyo maana kuna msemo white elephant project.
ukiangalia kenya wanafanya tofauti kwa maoni yangu, miradi yao inakaamilika ukiangalia highway systems ni kama zimekamilika and then ndiyo wanaanzisha mradi mwingine mkubwa i might wrong kwa maana naangalia kwa jicho la nje labda wakenya wao wenyewe wanaweza kuona tofuaiti lkn nafikiri angalau wana mpangilio kidogo ...