Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

SGR imeanza ssa. Naona kelele za wakenya zitaanza kufa
SGR1.jpg
SGR2.jpg
 
Wakenya vichwa ngumu mko wapi ?? noeni na the so called Kenyan SGR tulinganishe na ya Tz....😀
 
Tena ni hadi morogoro....Si kigali?
phase by phase hahahahah kwani yenu imefika kisumu 😀😀😀😀😀😀😀😀😀 na sio morogoro tu kwanza chain yake inaanza kusambazwa dar nzima alaf to morogoro phase ya kwanza hio
 
alafu kuna project inaendelea ruvu ya kujenga 500 hectares dry port ambayo makontena yanayotoka port of dar es salaam yatakuwa yanasifiri kwa treni mpaka ruvu dry port alaf hakuna trucks kuingia mjini yote yanaishia ruvu na kubeba mzigo hukohuko
 
SUMA JKT KUJENGA BANDARI KAVU RUVU
Alex February 14, 2017 MCHANGANYIKO Leave a comment 272 Views

GUPO.jpg

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko (Wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kulia) kabla ya kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa bandari kavu baina ya TPA na Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la kujenga Taifa –SUMA JKT jijini Dar es salaam.

GUPO-1.jpg

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko (Wa pili kushoto) na Mwanasheria Mkuu wa Shirika la uzalishaji Mali Jeshi la kujenga Taifa –SUMA JKT Kanali John Mbungo, (Wa pili kulia), wakitiliana saini mkataba wa ujenzi wa bandari kavu katika eneo la Kwala-Ruvu mkoani Pwani. Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es salaam.

GUPO-2.jpg

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko (kushoto) na Mwanasheria Mkuu wa Shirika la uzalishaji Mali Jeshi la kujenga Taifa –SUMA JKT Kanali John Mbungo (Kulia) wakikabidhiana mikataba ya ujezi wa wa bandari kavu katika eneo la Kwala-Ruvu mkoani Pwani. Katikati ni Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akishuhudia makabidhiano hayo.

GUPO-3.jpg

Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa(Katikati), akisisitiza jambo kwa watendaji wa Mamlaka ya Bandari (TPA) mara baada ya kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa wa bandari kavu katika eneo la Kwala-Ruvu mkoani Pwani.

Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

…………..

Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), imetiliana saini Mkataba wa ujenzi wa Bandari Kavu na Shirika la Uzalishaji mali la Jeshi la kujenga Taifa (Suma JKT), eneo la Kwala – Ruvu mkoani Pwani.

Mkataba huo wa zaidi ya shilingi bilioni 7.2 unaitaka Suma JKT kukamilisha bandari hiyo katika kipindi cha wiki Tisa kuanzia sasa ambapo tayari eneo la Hekta 500 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi huo.

Akizungumza jijini Dar es salaam leo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema ujenzi huo utapunguza msongamano bandarini na katika jiji la Dar es salaam kwa kuwa magari mengi ya mizigo yanayokuja bandarini kuchukua mizigo sasa yataishia katika bandari hiyo.

“Mizigo itasafirishwa kwa njia ya reli kutoka bandarini kwenda Ruvu, hivyo magari ya mizigo hayatafika Dar es salaam na hivyo kupunguza msongamano”, amesema Waziri Mbarawa.

Aidha, Profesa Mbarawa ameitaka Suma JKT kufanya kazi kwa uadilifu na kwa muda mfupi ili kuiwezesha mipango na mikakati ya Mamlaka hiyo kufanikiwa kwa urahisi.

Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa amesema Mamlaka hiyo itaanza ujenzi wa gati lenye urefu wa mita 300 katika bandari za Dar es salaam na Mtwara ili kuwezesha meli kubwa kuweza kutia nanga na kuongeza ufanisi wa Bandari nchini.

“Upanuzi wa Bandari za Dar es salaam na Mtwara utavutia wasafirishaji wengi kutumia bandari hizi, hivyo wafanyakazi wote wa Mamlaka hii wafanye kazi kwa bidii na weledi”, amesisistiza Waziri Mbarawa.

Kwa upande wake Mwanasheria mkuu wa JKT, Kanali John Mbungo, amemhakikishia Waziri huyo kuwa kazi ya ujenzi huo itafanyika kwa ubora na katika kipindi kilichopangwa.

Ujenzi wa Bandari Kavu katika eneo la Ruvu ni mkakati wa Serikali wa kupunguza msongamano katika jiji la Dar es salaam.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
 
jamaa vituko....the difference btwn Kenya na tz....Kenya wakiwa wanamalizia kitu ndio tz hua wanaanza alafu jamaa wanakuja payuka tunasonga zaidi ya Kenya....kuna mtu amegundua hili?
 
jamaa vituko....the difference btwn Kenya na tz....Kenya wakiwa wanamalizia kitu ndio tz hua wanaanza alafu jamaa wanakuja payuka tunasonga zaidi ya Kenya....kuna mtu amegundua hili?
Munamaliza SGR zimepitwa na wakati 30 yrs sisi tunaweka kitu ambayo ni history kwa east and central africa ndio kawaida yetu hahhahahhaa
 
jamaa vituko....the difference btwn Kenya na tz....Kenya wakiwa wanamalizia kitu ndio tz hua wanaanza alafu jamaa wanakuja payuka tunasonga zaidi ya Kenya....kuna mtu amegundua hili?
NO, KEJELI ZA WAKENYA NI KWAMBA WANAONGEA NA KUIPONDA TANZANIA UTAFIKIRI MAENDELEPO YAO WAMEFANYA MIAKA SABINI ILIYOPITA, YAANI UTAFIKIRI NI GAP LA MIAKA KIBAO KUMBE NI HATUA CHACHE , SISI TUNASISITIZA TANZANIA YA SASA SIO ILE WANAVYOTUAMBIA KILA SIKU YA MWAKA 1970. VITU VINGI VYAO EITHER VIPO HATUA YA MWISHO AU KATIKATI AU NDIO KWANZA WAMEMALIZA, WALICHONACHO NA SISI TUNAFANYA, SO DHARAU ZA AJABU AJABU ZIISHE. TENA HAWATAKIWI HATA KUJIFANANISHA NA SISI WANGEJITAHIDI KUJIFANANISHA NA SINGAPORE. LENGO HAPA NI KUSISITIZA KUWA TANZANIA IMEBADILIKA NA WAACHE DHARAU. BADO TUNATEMBELA WOTE KICHWA HAPA.
 
jamaa vituko....the difference btwn Kenya na tz....Kenya wakiwa wanamalizia kitu ndio tz hua wanaanza alafu jamaa wanakuja payuka tunasonga zaidi ya Kenya....kuna mtu amegundua hili?

Mmemaliza lipi!!
Mnakimbia bila breki!!?
mnajenga njia nzuri mnatumia Mitungi eti Treni
sisi tupo kimtindo mtindo
kawia ufike
umeona picha ya treni hapo juu
linganisha na Upumbavu upumbavu wenu !!
 
Mmemaliza lipi!!
Mnakimbia bila breki!!?
mnajenga njia nzuri mnatumia Mitungi eti Treni
sisi tupo kimtindo mtindo
kawia ufike
umeona picha ya treni hapo juu
linganisha na Upumbavu upumbavu wenu !!
another difference btwn Kenya na tz....Kenya wakionesha the actual thing tz wanaonesha picha.motochini na rende yako yakina geza hamchoki kwani kufukuza upepo?
 
another difference btwn Kenya na tz....Kenya wakionesha the actual thing tz wanaonesha picha.Geza hamchoki kwani kufukuza upepo?
huyu hua anajifanya kichwa ngumu lakini ataelewa tu😀😀😀😀😀😀😀😀😀
 
NO, KEJELI ZA WAKENYA NI KWAMBA WANAONGEA NA KUIPONDA TANZANIA UTAFIKIRI MAENDELEPO YAO WAMEFANYA MIAKA SABINI ILIYOPITA, YAANI UTAFIKIRI NI GAP LA MIAKA KIBAO KUMBE NI HATUA CHACHE , SISI TUNASISITIZA TANZANIA YA SASA SIO ILE WANAVYOTUAMBIA KILA SIKU YA MWAKA 1970. VITU VINGI VYAO EITHER VIPO HATUA YA MWISHO AU KATIKATI AU NDIO KWANZA WAMEMALIZA, WALICHONACHO NA SISI TUNAFANYA, SO DHARAU ZA AJABU AJABU ZIISHE. TENA HAWATAKIWI HATA KUJIFANANISHA NA SISI WANGEJITAHIDI KUJIFANANISHA NA SINGAPORE. LENGO HAPA NI KUSISITIZA KUWA TANZANIA IMEBADILIKA NA WAACHE DHARAU. BADO TUNATEMBELA WOTE KICHWA HAPA.
relax...sio mbongo mimi.alafu ujue ni watz wanajicompare na kenya sio the other way around.mfano,cheki hii thread ilianzishwa na nani,tulipojenga sgr yetu tusingeweza compare na tz cz hamna but vile mnajenga yenu ndio mnajicompare na sisi
 
Back
Top Bottom