Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Vipi hapo kwenye bandari ?
 
Wiki ijayo wapi kaka! [emoji23][emoji23][emoji23]
Nimetoka NMB muda huu iko 14.46
Inaitwa Free fall, mpk kumaliza huu mwaka itakuwa 1ksh=5tzs na baadaye mwakani itakuwa 1ksh=1tzs, mind you pesa ya Tz ina thamani kuliko ya Kenya, sasa ikifika kwenye 1by1 sijui itakuwaje [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Watatumbua [emoji3][emoji1787][emoji1787] ngoja ishuke
 
Vipi hapo kwenye bandari ?
Swali zuri Sana; Bandari, viwanda na miundombinu mingine, Kenya ilikua inafanya vizuri kutuzidi kutokana na historia za hizi nchi.

Hata kabla ya Uhuru, wakoloni waliichagua Kenya Kama makao makuu Yao, Tanzania na Uganda zilikua ni Kama mashamba Yao, hivyo walijenga viwanda vingi Kenya, barabara na bandari Ili kuweza kuisafirisha bidhaa zao.

Hata baada ya Uhuru, bado Kenya ndiyo ilikua ni chaguo la nchi za Magharibi kwasababu wazungu hawakufukuzwa Wala kunyang'anywa viwanda, Nyumba au Ardhi yao Kama tulivyofanya huku Tanzani. Nchi za Ulaya ziliendelea kutumia bandari ya Mombasa na uwanja wa ndege wa Nairobi Kama milango Yao mikuu katika Kanda hii.

Vuguvugu la ukombozi wa kusini mwa Afrika nalo likawafanya wazungu kuzidi kuichukia Tanzania, kwahiyo bandari ya Dar ilikua inatumiwa na Zambia pekee kabla ya nchi za kusini mwa Afrika hazijawa huru, Mabutu na Kenyatta walikua ni vibaraka wa wazungu, Tanzania tulitengwa.

Baada ya hivyo vita kukamilika, Sasa taratibu tunaanza kuinyang'anya Kenya masoko yake. Rwanda, DRC, Uganda, na South Sudan, haya ni masoko ya Kenya ambayo tunayanyakua kwa Kasi kubwa Sana.

Hapo katikati tulizembea kidogo, ila Sasa tumeamka Sana, Kumbuka kuishawishi nchi kubadilisha njia waliyokwisha wekeza na kuingia mikataba kwa muda mrefu inahitaji muda, ila hivi Sasa Kila kitu kinakwenda vizuri.



Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Hapo nimepata somo .

Kwa nini na sisi tusijiboreshe kwenye hivyo vipengele ? nakumbuka Magufuli alizungumzia Tanzania ya viwanda amekufa mpka leo kimya
 
Hiii ya Dar Moro inapita ndani ya posta,kariako na upanga plus ni viaduct?
Kuna land serikali watanunua pia?
The fact kwamba ni expressway haina tofauti kabisa, actually expressway ya Dar itapita kwenye junctions nyingi kuliko ya Nairobi na unaelewa kwenye junctions lazima kuwepo viaducts due it's an expressway
 
Hapo nimepata somo .

Kwa nini na sisi tusijiboreshe kwenye hivyo vipengele ? nakumbuka Magufuli alizungumzia Tanzania ya viwanda amekufa mpka leo kimya
Mkuu, Tanzania hivi Sasa ni moto Kama pasi, japo bado tunayomapungufu, lakini hivi Sasa kwa huu ukanda wa kusini mwa Sahara, sidhani Kama Kuna nchi yoyote inayoendelea kwa Kasi Kama Tanzania, Magufuli alitubadilisha Sana watanzania, japo Kasi imepungua kidogo, lakini bado tunafanya vizuri Sana.

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…