Sisemi hakuna shida sisemi waKenya huwa hawaongei Sheng. Lakini kama ulienda shuleni kenya pia lazima ukuwe uliandika insha kiasi. Yamaanisha twaweza ongea Kiswahili sanifu lakini wakati mwingi twachagua kuonyesha kimombo yetu. Nami naona ni too much. Sisi ni waafrika. Nadhani waKenya wengi huhusiana Kimombo na maendeleo lakini kimombo ni lugha tu kama Kiswahili au Kichina au Zulu.
Kenye nasema ni rahisi nchi zetu mbili ndizo nchi za Kiswahili. Wanaongea Kiswahili pia huko DRC. Lakini tuna lugha moja hatufai kuwa na uhusiano mbaya.
Sitaki Afrika Mashariki iende ile njia ya Conservative Parties duniani. Utapata Conservatives kwenye nchi za kigeni sana sana huchukia nchi jirani kabisa lakini wana fantasise kuhusu nchi zilizo mbali ambazo hawazijui.
e.g.
- US na Mexico conservatives wa Marekani hawapendi Mexican immigrants
- Uingereza ndiyo hiyo ilitoka kwenye EU
- Conservatives wa nchi kama Korea Kusini huchukia waChina lakini husifu Marekani.
- Nayo pattern inaendelea chama zilizo za far right hata Ulaya kama Front National utapata hawapendi majirani lakini same same thing wana'fantasise' about Russia.
Naona ni muhimu Afrika Mashariki iwache hiyo tabia people will sing praises of other people but none about the countries neighbouring us.