That is your opinion.Usitake kila mtu afikiri na kutazama unavyoona wewe.Ndio maana Mimi huwa nawaona wale wanaosema JPM ni kama nyerere na kuwadharau Mwinyi,Mkapa na Kikwete ni wapumbavu kwa kua hawataki kufanya detailed analysis ya viongozi na nyakati zao,kila kiongozi amawezesha nchi kupiga hatua.Simple Mwinyi hakua na option nyingine zaidi ya kufungua uchumi the same wachina walifanya 1978 tofauti wao hawakutaka kuruhusu vitu vingine nje na uchumi walibaki na socialism kwenye tamaduni,dini,na siasa wakaingiza ubepari kwenye uchumi,Mkapa anaingia uchumi umefunguliwa lakini hatuna mtaji na wataalamu anaruhusu Western countries kuingia kama China walivyofanya sema wenzetu walituzidi kwenye kuchukua maarifa tax incentives zipo China Hadi leo kwenye technolojia mpya,Kikwete anaingia mikataba ya madini ipo inafanya kazi lakini anaikuta nchi haina miundo mbinu ya usafirishaji ya kutosha anahangaika huku na huko anasaidia kika kila mkoa unaunganishwa kwa njia ya lami,na ndio Rais aliyetoa ajira nyingi hasa kwenye utumishi wa Umma ndiye aliyekuuza uchumi zaidi na anaweka vision ya kua na SGR.JPM anaingia hahangaiki tena kuunda taasisi au kuunganisha mikoa kwa lami execpt mikoa michache kabisa anapata nafasi ya kujenga nyerere hydro power,Sgr nk ...hivyo kila mtu kafanya yake japo kila mtu anakasoro lakini hatuwezi kuwa wote wapumbavu na kubeza viongozi wetu huku tukijua ya mazuri mengi wamefanya.