Kupitia thread hii mambo mengi yamewekwa wazi. Tumeona mbichi na mbivu baina ya majiji haya mawili.
Mimi makao yangu ni Dar es salaam na huwa naenda Nairobi mara kwa mara.
Tukiangalia future Dar es salaam ndio superpower dhidi ya Nairobi.
Jiji lililo kando kando ya bahari hakika huwezi fananisha na jiji lililo mbali na bahari au ziwa.
Kwa sasa Nairobi na Dar es salaam zinatofautiana sana.
Zinatofautiana kiutamaduni, mazingira na mvuto.
Kwa upande wa mvuto Dar es salaam inavutia sana. Imepambwa na bahari huku beaches na islands zikiifanya iendelee kunawili.
Upatikanaji wa pesa hakika Dar es salaam inaizidi Nairobi kwa mbali. Hapa naongelea watu wa kawaida kabisa. Huko Nairobi ni watu wenye status ya juu kidogo ndio wanaopata pesa. Lakini Dar es salaam nguvu yako na akili yako ndiyo limitation.
Tukija upande wa upatikanaji wa chakula. Hakika hapa usiseme. Dar es salaam ipo na aina tofauti tofauti ya chakula. Wakati Nairobi chakula kikuu ni ugali pekee.
Dar es salaam utakuta mitaani wanauza aina tofauti ya chakula tena kwa bei ya chini. Ukitaka calamari, dagaa kamba, supu, Nyama choma, Wali, chips kuku au mayai unapata sehemu yoyote kwa tsh 2000 au chini yake yaani 1500. Ambayo ni chini ya dollar moja ya kimarekani.
Sasa tukija usafiri ndani ya jiji. Hapa dar kuna aina tofauti tofauti ya usafiri ukilinganisha na Nairobi.
1. Daladala
2. Boat na vivuko
3. Bajaji
4. Pikipiki
5. BRT
6. Train
7. Normal Tax
8. Urber tax
Kwahiyo ni uchaguzi wako tu na pesa yako.
Nairobi unaonekana ni mji wa old age ulitamba kipindi kile. Watu wake hawataki kubadilika. Na wanajivunia ukoloni.
Kwa hakika nimeweza kuona kwamba kumbe Nairobi ipo overrated kutokana na kukumbatiwa na wazungu wa uingereza ambao wanamilk media kubwa kubwa duniani kwa kutoa taarifa nyingi kuhusu Nairobi.
Lakini sasa mambo yamebadilika, game ina change, lakini vijana wa nairobi hawataki kubadilika.
Kwahiyo nyie vijana wa nairobi endeleeni hivyo hivyo akili zikiwakaa itakuwa asubuhi