Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Ikiwa hii kitu ndiyo CSR ya JNHPP project basi Tz tumepiga hatua kubwa sana kwenye negotiations za mega projects.
 
Hivi ahadi za mfalme wa Morocco ndio basi tena.
 
Bado ile stadium kubwa ya dodoma yani dodoma itakua balaa [emoji1241][emoji1241][emoji1241][emoji1241]
Siyo kwamba ndiyo mbadala wake. Maana baada ya kuona mfalme wa Morocco anazingua gavoo ilianza negotiations na Arab Contractors ili watumie ile CSR kutoka Nyerere Dam project ambayo ni 10% ya total project cost itumike kufanya kazi hiyo.
 
Imeisha hiyo.
 
BTW ule uwanja wa Mwanza unaweza kuboreshwa ukawekwa paa, viti na kuongezwa capacity ukafikia quality ya wa Dar! Kama uwanja wa Olympic Berlin ulivyofanywa!

From






To

 
Yeah sio kila mchina ila wengi wao wanapenda communism
 
BTW ule uwanja wa Mwanza unaweza kuboreshwa ukawekwa paa, viti na kuongezwa capacity ukafikia quality ya wa Dar! Kama uwanja wa Olympic Berlin ulivyofanywa!

From






To


huu ni wa CCM.. hao ndo wafanye kuboresha.. sidhan kama ni kipaumbele kwao.. wao wanawaza kujenga apartments tu huku Dar
 
Demokrasia is an illusion mzee sijawahi kuamin kwwnye ilo jambo tangu
Democracy ni mind game tuliletewa Africa kama obstacle ya kuendelea mbele, hakuna mafanikio yoyote ya kimaendeleo kwenye so called democracy, kama ingekua hivyo basi kusingekua na umasikini mkubwa kwenye nchi za kidemokrasia

Wazungu wenyewe democracy wameiunda wakiwa tayari wlishapiga hatua kubwa za kimaendeleo good decades ago na wengine hata leo hiyo democracy hawafati ndio maana Markel na Putin wapo madarakani miaka mingi sasa na nchi nyingi za ulaya zipo na mifumo yao ya asili ya utawala
 
Imagine Madini yetu KE Ni untapped 96% Sjui tukiguza Tutakuwa wapi Tutapaa Kama vile Saudi.Imagine Kenya only rely kwa mimea pekee.Nyinyi TZ mnauza Madini Lakini sijui Pesa inapotelea wapi[emoji848]
Wacha upuuzi na wewe bhn Kenya madini mtoe wapi, mngekuwa na madini km sisi unadhani viongozi wenu saizi wangekuwa wanarandaranda hapo Kenya? Saizi wangekuwa wanabadilisha ndege tu ku sign deals za 10% [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli mzee ni utopolo tuu iyo demokrasia cha muhimu amani tuu
 
Yeah sio kila mchina ila wengi wao wanapenda communism
Hakuna kitu kama “wengi wao wanapenda communism”

Kwenye nchi kama hizo, wanaofurahia uongozi usio na demokrasia ni wale wanaofaidika moja kwa moja na uongozi huo na wasioelewa haki zao.

Bali wale ambao ungozi unawakandamiza ndio huteseka! Hebu fikiria Uyghur muslims. Wanachukuliwa kinguvu kutoka kwenye nyumba zao halafu wanapelekwa kwenye camps ambapo wanafundishwa ku-behave kama wachina halisia. Wanakuwa-brainwashed kuamini kuwa dini yao sio nzuri na pia wanafungwa vizazi ili wasizae na kuongeza Idadi ya waislamu. Na kama walikuwa na watoto, hao watoto wanaibiwa halafu wanapelekwa kwenye nyumba za kulelea watoto za kichina Kwa lengo la kuwakuza kwenye ya tamaduni tofauti na za Kwao. Sasa imagine uwe kwenye position ya hawa jamaa Na Ndio utafahamu kuwa demokrasia sio illusion. Au nenda North Korea halafu utanielewa zaidi.

Mnaishi kwenye hii nchi mnachukulia kila kitu for granted! Yes, demokrasia Tanzania haina nguvu sana (Mama anajaribu kuipa nguvu) lakini there are worse places.
 
Ikiwa hii kitu ndiyo CSR ya JNHPP project basi Tz tumepiga hatua kubwa sana kwenye negotiations za mega projects.
Magufuli alikua notorious kwenye negotiating and bargaining, alikua na akili kubwa kupindukia kwenye issues za miradi ya ujenzi

Cha kushangaza naona Egypt wanaliweka sana kama ni msaada wakati ni takwa la mkataba.
 
Nina hofu.

Na hafu yangu sio tu hofu.

Bro, hizi kitu zinaumiza sana kwa wazalendo. Kuna wengine hudhani kuwa hizi kitu zinatupatia kiburi cha kuwagaragaza wakenya hapa zitaendelea tu kuchipua hata kama mafisadi yataanza kushamiri tena kwenye serikali na mamlaka zake.

Ukweli lazima usemwe na kelele lazima zipigwe ili angalau kuwapunguzia kasi hawa majangili. Imagine kasi ya kuondoa wazalendo aliyoanza nayo huyo bi mdashi wao. Ingekuwaje bila watu kupiga kelele! Ingekuwaje bila viongozi wa dini kuibuka na kuweka maandishi ukutani!

Je leo TPDC si ingekuwa mikononi mwa majangili bila hizi kelele! Hao akina Mulamula ni brainwashed so called diplomats. Sishangai sasa hivi balozi wa Marekani anashinda kwenye ofisi za wizara zetu kuahidi maendeleo.

Let's not be fooled! Hakuna wajomba au shangazi wa kutuletea maendeleo. Jana huyo mama alisema CCM ina wenyewe na kweli tunawaona wakirejea kwa kasi. Wazalendo wa ukweli wanapukutishwa kwa kutumia tuhuma za mitandaoni ambazo kimsingi hutangulizwa tu ili kuhalalisha hayo mabadiliko.

Narudia. Hii battle na wakenya lazima iende sambamba na sisi kutambua yale yanayotufanya kuwa superiors kwao. Tukikaa kimya, soon tutaanza kuona parachichi zetu zikianza kwenda tena Kenya kuwekwa chapa za "made in Nyang'auLand".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…