Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Unasema ati asilimia kubwa ni slum? Ndio nakuambia kwamba huijui Nairobi wewe. Zaidi ya unachotazama kwenye TV wewe hujui lolote.
Bro Nairobi nimekaa mitaa mbali mbali siwezi nikasingizia kitu ambacho hakipo mfano umoja one,2,3 mpaka kwa chief kuna washikaj wangu wengi wa rundi na wa Congo,komarock south c wasudani,rongai,kasarani,Zimmerman,mpaka githurai 45 wanakaa wanyarwanda/warundi,pangani waithiopia, Eastleigh/komaraock wasomali etc mbona wakimbizi Wanakaa maisha ya juu kuliko nyie wenyeji?
 
kawaulize Kiswahili chao cha Kenya au Tanzania!! Nina uhakika utaambiwa wana-linkage na Tanzania!
 
We unaongelea nairobi ya kitambo labda
 
Mimi zamani kidogo kabla ya mambo yangu ya kifedha kubadilika nilikuwa naishi Umoja 1. Sasa unasema kwamba Umoja ni slum? Kichwa chako ni kizuri kweli wewe? Kama Nairobi ni slum mbona kuna Watanzania wengi wanaoishi Nairobi? Kwa mfano wakati bado nilikuwa naishi Umoja, nilikutana na Watanzania wengi sana pamoja na Waganda na Warundi. Cha kushangaza ni kwamba wote wanafanya biashara ndogo ndogo. Kuna Mtanzania msichana alikuwa waiter kwenye hoteli ambayo nilikuwa napenda kula na aliniambia kwamba anatokea Mwanza. Kuna Mtanzania mwingine ambaye alikuwa anauza kwenye duka. Kuna Watanzania wengi walikuwa wanauza nguo mahali panapoitwa Mtindwa, nadhani unapafahamu. Sasa kama Nairobi ni slum mbona mumejazana humu mkifanya biashara ndogo ndogo haswa ya kuuza mitumba? Hadi MP Jaguar aliposema Watanzania wanaouza mitumba Nairobi waondolewe mkapiga makelele hadi serikali yenu ikaanza kutoa vitisho? Nakumbuka hata bunge lenu lilijadili hili swala na kutishia Kenya kwamba tusiwafukuze Watanzania wauza mitumba? Mnafanya nini huku kama huku ni slum tupu? Mnatafuta nini Nairobi? Mbona msibaki huko kwenu ambako hakuna slum?
 
Tunaongea kuhusu population between Dar and Nairobi wewe usharuka hadi unamention mikoa mengine. Hata jumbo rahisi kama kufuatilia hoja ni tatizo kwenu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…