Bastola ya Aden Rage na CCM

Bastola ya Aden Rage na CCM

Sishangai Rage na hata wengine kufanya hivyo. Hilo ni suala la muda tu, na wengine wengi sasa watafanya hivyo hivyo pia.

Wakati umiliki wa silaha za moto unaruhusiwa na Mkapa na genge lake akina Mapuri na Mahita, watu walisema sana kuhusu hili. Wenye uwezo wa kumiliki silaha ndiyo hao hao tayari wanalindwa na jamhuri au usalama wao hauko hatarini kama siye wa uswazi.

Wanaishi kwenye maeneo bora, nyumba zao zina nondo hadi madirisha ya chooni, wanazungukwa na kuta za futi 14 zenye nyembe juu, wana walinzi ndani na nje ya kuta hizo, sehemu zao za kazi na biashara pia 'ulinzi' ni wa juu. Pia ni hao hao ndiyo wanaotuambia na kutuimbia kila siku kuwa nchi yetu chini ya CCM na serikali yake, ni nchi ya AMANI na UTULIVU.

Je, ni usalama gani wanautaka kwa kumiliki silaha katika AMANI na UTULIVU wote huo?


Ni wazi kuwa huo usalama wanaoutafuta ni dhidi ya wananchi wao wenyewe. Na ni kwa nini wawaogope wananchi wao, wapiga kura wao, wenye AMANI na UTULIVU ulioletwa na CCM na serikali yake kwa miaka yote hii?

Watu wa Asia ya Mashariki (East Asia) wana msemo kuwa ukitaka kumpika chura usimuweke kwenye maji ya moto, ataruka. Unamweka kwenye maji baridi, unawasha moto chini ya sufuria, na maji yanavyozidi kupata uvuguvugu chura hawezi kuona tofauti na kujua kuwa moto unaongezeka. Taratibu anaiva. Ila wewe mpishi, unajua maji ni ya moto na unafunika mikono yako kabla hujaepua sufuria.

Tanzania tuliwekwa kwenye maji baridi, na kidogo kidogo maji yameishakuwa vuguvugu au ya moto (EPA, Richmond, Meremeta, Kiwira, Barick, Kahama Mines, Dowans, Deep Green, Tangold, Mbolea/Matrekta Kilimo Kwanza, BOT Twin Towers, Rada, Ndege ya Rais. MV Victoria, MV Spice Islander, Mbagala, Gongo La Mboto, n.k.), na waliotufikisha hapa ndiyo hao wanafunika mikono yao (bastola kibindoni, nyumbani au kwenye magari yao) ili wasiungue wakati wanaopoa chura.
 
Hii inadhihirisha kuwa wameingia madarakani kwa mizengwe ya wizi wa kura iweje uwaogope waliokuchagua hadi uwe na silaha wakati wa kuwahutubia wajue yana mwisho nguvu ya umma itachukua haki yao waliyowapora
 
Sasa kama mnawavua hijab hadharani wafanyaje? Wasubiri muwavue suruali bila kujihami?
Silaha ni haki yake, kuonekana ni bahati mbaya tu. Tujadili mambo mengine ya maana
 
Mnamlaumu tu bure. Akili ya Rage imeishia hapo. Huwezi toa kitu usichokuwa nacho. Na akili yake ni akisi ya mabos wake na lichama lake.
 
Na mimi kesho naenda na panga langu kwenye kampeni
 
Maadili ya Uchaguzi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kifungu namba 2.2(c) kinasema...

"Mtu yeyote haruhusiwi kuwa na/au kubeba silaha ya aina yoyote ikiwa ni pamoja na silaha za jadi au zana yoyote inayoweza kumdhuru mtu katika mkutano wa kampeni au mkusanyiko wowote wa kisiasa."


 
SOO for what???? Anyway,Mtamtambuaje kuwa kumbe naye ana mguu?? Yaani wabongo bana....!
 
leo kapanda na bastola,kesho atapanda na gobore,kesho kutwa atapanda na mabomu ya kurusha kwa mkono.atachosema ni anajilinda,anajilinda na nini katika mkutano wa hadhara uliojaa watu wa usalama,tena wakutosha.
 
Nimeshtushwa na picha iliyopo kwenye ukurasa wa mbele wa moja ya magazeti ya leo. Mbunge wa Tabora mjini Ismail Aden Rage anapanda jukwaani na Libastola kiunoni. Mungu amejibu swali gumu ni nani anaeleta vurugu kwenye kampeni za Igunga? Bastola ya nini kwenye mikutano wakati kuna wanausalama weengi hivyo? CCM NI HATARI JAMANI NI KIFO..

Hii kitu angekutwa nayo Lipumba au Mbowe tungesikia wanaharakati wa kiislamau wakipiga kelele
 
Nakumbuka Mbowe aliwahi kuvamiwa baada ya mkutano kwenye kampeni za mwaka jana akajihami kwa kufyatua risasi juu bado ilikuwa issue sana na hapo alikuwa anavamiwa na akihojiwa .Mbowe anayo pistol muda wote lakini sijui kama kuna mtu kesha kuiona .Kitendo cha huyu jamaa kuwa na pistol tena kwa uwazi hivi kwenye mahali pa amani maana yake nini ?Je naye atahojiwa au kwa kuwa ni CCM basi hakuna kitu ? CCM wana hatarisha amani na usalama wa Nchi .
 
Ni kinyume cha sheria..... inatakiwa ashitakiwe au akamatwe.
 
Maadili ya Uchaguzi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kifungu namba 2.2(c) kinasema...

"Mtu yeyote haruhusiwi kuwa na/au kubeba silaha ya aina yoyote ikiwa ni pamoja na silaha za jadi au zana yoyote inayoweza kumdhuru mtu katika mkutano wa kampeni au mkusanyiko wowote wa kisiasa."


Nilikuwa nataka kumwaga hiyo sheria hapa jukwaani, ila umeniwahi.
He can be sued...the evidence is right there.
 
Mimi nilikuwa mpenzi na shabiki mkubwa klabu ya Simba, lakini tangu nilipoona upuuzi wa mwenyekiti Aden Rage nimesitisha mapenzi yangu kwa klabu hiyo hadi siku huyu gaidi wa kisomali atakapo ondoka madarakani hapo msimbazi.
 
Hivi hatua ya Rage ya kupanda jukwaani na bastola tena kuiacha wazi inaonekana ilikuwa yamaanisha nini?
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"][/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
07ragekam.jpg




[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
View attachment 37697Source hiyo mwananchi ya leo
Unajuaa sikuona hii picha nikadhani hiyo pisto ilionekana kwa bahati mbaya kutoka mafichoni, but kwa mtindo huu huku ni kudhamilia kabisa. Na kwa kuwa sheria yetu siku hizi inaonekana kama inauchaguzi na kubagua nani wa kumkata. Basi ndo tujionee wenyewe! Ila ni tahadhari kuwa AMANI tuipigiayo debe kila uchao ishaanza kwenda kwao! Sishangai saaaaana maana wengine ndo asili zao bwana, twendeni tutafika!
 
Back
Top Bottom