Kuna kampuni ilikuwa inaitwa spider au taqwa, route yake dar-arusha-nairobi-busia-kampala. Gari zao zilikuwa zote ni Nissan diesel, chuma cha route nzito. Pia zilikuwa na route ya Dar tunduma. Zile chuma zipo slow kama malory, kwenye milima ndio usiseme. Chuma ilikuwa inabeba mizigo nyuma. So kila tukikaribia wanapopima uzito, abiria nusu wanashushwa, nusu wanasogea mbele ili bus libalance uzito maana nyuma kuna mizigo. Ilinyesha mvua, kila upande majanga. Wachache sana hayakuwakuta. Tulitoka dar 12asubuhi, tukaingia Nairobi sa8usiku. Mgongo unawaka moto.