Basi gani la mkoani ulipanda ukajutia?

Basi gani la mkoani ulipanda ukajutia?

Kuna basi nilipanda kutoka ifakara to Dodoma, aise gari ndani Lina mifugo mingi kuliko abiria, just imagine mtu anapanda ndan ya bus amebeba mbuzi na kuku ndan ya gari,,kilicho niboa zaid nimelala usingiz kuja kushtuka nashangaa mbuzi ananilamba nywele.
Wewe ni shujaa kama uliweza kupata usingizi kwenye basi la sampuli kama hiyo
 
Kuna Bus jina lake limenitoka Dar - Mwanza, picha linaanza Tv ipo pale kwa dereva kwenye dashboard yake, alafu anasimulia hiyo movie anayotizama kwa sauti mpaka watu wa siti ya mwisho anataka wasikie.
Nimepitiwa na usingiz kuja kuamka kofia yangu kavaa yeye dereva afu nipo siti ya kati kati nikajiuliza imemfikiaje😂.
Wanauza maji ila wanasema hatukupi mpak tusimame sehemu tusije tukakupa ukatusumbua mkojo.
Kila abiria ana tiketi ya rangi yake mwingine njano mwingine nyekundu acha tuu.
Mara konda aje asemw jamani tunapiga self wote tuseme ndiziii ili apost kwenye page ya UNICEF sijaelewa mpaka leo.
Wakaanza kubishana Ali kiba vs Diamond, dereva na konda
 
Mwezi ulopita nilipanda ALLY's STAR kutoka DOM - MORO, lile Basi halikuwa na Mwendo, lilisimama Njiani x3 , pale 88 Dom walipanda wamama wajasiriamali na nyungo, Ndoo & vikapu vya karanga... humo ndani wanasukumana kuuza mixer kubembeleza abiria kuwauziaa... Mwanzoni nikachukulia powa... nikajua watashuka hapo tu mbele... daaah I see tulikwenda nao ... hata sikumbuki walishuka Gairo ama wapi...
 
Nilikata kidinilo muda wa safari wanasema halipo tukapewa lingine sikumbuki jina tumepanda nimekaa karibu na mlango wa dharura aise Barabara zimechimbwa vumbi la njiani lote linaingia ndani pumzi inakata nikasimama ili kukwepa kuoga vumbi mpaka kwenye lami tulioga vumbi haswa kufika ubungo ilibidi kuoga Kwanza
 
Kuna basi lakwenda Kilindi/Songe mkoani Tanga linaitwa KIPACHA. Wamekaa waswahili yani unakatiwa tiketi ya kwenda Songe ila ukifika Handeni mjini unafaulishwa kwenye gari yao nyingine.
Ukikosa siti utasimama kuanzia Handeni mpaka Songe.
Kampuni ya hovyo sana sijawahi ona
nilikata Siti mbili na mwanangu kufika handeni tumefaulishwa basi lingine hakuna Siti 😔😔😔 limejaa.
 
Hii ya kujinyea niliwahi kutana nayo kwenye safari flani hivi huyo kaka nilimuhurumia sana
Nawaza aibu hii.. Kuna mwamba tumbo lilimchafuka tunatoka Dar kwenda Njombe, njiani alisimamisha gari zaidi ya mara 3. Ila yeye sikumuona anakula kula vibaya. Ile aibu haielezeki.

Sema mwamba akajiongeza, tumefika Mikumi kuna mtu alikua anashuka. Jamaa nae akaona ashuke safari iishie hapo, akihofia anawasimbua abiria ile simama simama.

Sema kuna faza alikua amekaa nae akasema hapana dogo shuka, kajisitiri tunaendelea wote ata ukisimamisha mara 10 na abiria wengine walisupport.
 
Happy Africa ni Luwinzo
Hapana. Luwinzo basi zake nyingine huwa anaziita Sweet Africa.

Hizo Happy Africa zilikuwa ni basi fulani hivi kuukuu za bodi ya kuchonga! Za jamaa mmoja wa Mafinga. Kuna msimu mmoja wa sikukuu nilikosa usafiri wa uhakika wa kwenda Njombe pale Ubungo, nikalazimika kupanda hilo basi. Kiukweli ile safari ilikiwa ni ngumu sana.
 
Back
Top Bottom