Basi gani la mkoani ulipanda ukajutia?

Basi gani la mkoani ulipanda ukajutia?

Zakaria Trans,Mwanza -Tarime.Bus lilikuwa poa tu ila ngumi sasa.1.Dereva v/s konda 2.Konda v/s abiria 3.Abiria v/s Dereva 4 .Konda na derevav/s abiria 5.Abiria v/s Abiria.Mwisho kabisa Sister wa Kikatoliki v/s Konda.
 
Master line, mwanza to dar , gari bovu linavuja halina tv wala Air conditioner A.C siti mbovu gari linatembea linatoa milio ya kichovu linaharabika Kila masaa muonekano ziroooo. Bright line , dar to dodoma Yani ticket imeandika kuripot sasa 7: 30 na kuondoka saa 8:00 Cha ajabu tukatoka saa 10 limekaa tu linapakia abiria kama daladala vile 😠
 
Kuna basi nilipanda kutoka ifakara to Dodoma, aise gari ndani Lina mifugo mingi kuliko abiria, just imagine mtu anapanda ndan ya bus amebeba mbuzi na kuku ndan ya gari,,kilicho niboa zaid nimelala usingiz kuja kushtuka nashangaa mbuzi ananilamba nywele.
 
Back
Top Bottom