Bashite kufunga namba za Serikali kwenye magari binafsi, hii imekaaje?

Bashite kufunga namba za Serikali kwenye magari binafsi, hii imekaaje?

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
18,875
Reaction score
29,421
IMG-20260214-WA0026.jpg


Huu ushamba haufai kuachwa hivihivi, TISS, TRA, TEMESA sijui nani anahisika hapo atuondolee aibu hii
 
Ndio shida yetu vijana, tunaaminiwa, tunapendwa na tunapewa madaraka. Badala ya kufanya mambo ambayo yataonesha uwezo wetu mpaka kuzipa sifa mamlaka zetu za uteuzi, tunaanza kufanya utoto ambao unaishia kuzipa wakati mgumu mamlaka za teuzi zetu. Kwani Mh. angetembea tu na namba za kawaida kwenye gari yake angepunguza nini? Kuna kelele nyingine tunazitafuta wenyewe bila sababu za msingi.
 
View attachment 3543628

Huu ushamba haufai kuachwa hivihivi, TISS, TRA, TEMESA sijui nani anahisika hapo atuondolee aibu hii
Nilikuwa nasoma jinsi Hitler na Mussolin walivyoingia madarakani, naona viashiria vyote kwa Makonda. Kuna kosa moja kubwa sana linafanyika na naona linaenda kujirudia. Vikundi vyote vya utekaji wakati wa Magufuli vilikuwa vinaratibiwa na Makonda. Makonda atakuja kuwa kiongozi mkubwa nchi hii maana kwa sasa uongozi hautoki kwa wananchi, bali kutoka magenge ya madaraka, na atafanya mauaji ya kutisha.

Sehemu kubwa ya tabia za Makonda ni kama za Magufuli. Huyu anachanganya tabia zake binafsi na madaraka, na kwa vyovyote atafanya anachotaka na sio sheria zinavyotaka. Haya ya Makonda kufanya ayatakayo akiwa madarakani hayajaanza sasa, bali ni tabia yake toka huko nyuma. Tunza uzi huu, na tuombe uzima.
 
Ndio shida yetu vijana, tunaaminiwa, tunapendwa na tunapewa madaraka. Badala ya kufanya mambo ambayo yataonesha uwezo wetu mpaka kuzipa sifa mamlaka zetu za uteuzi, tunaanza kufanya utoto ambao unaishia kuzipa wakati mgumu mamlaka za teuzi zetu. Kwani Mh. angetembea tu na namba za kawaida kwenye gari yake angepunguza nini? Kuna kelele nyingine tunazitafuta wenyewe bila sababu za msingi.
Unaweza kumtoa Bashite kutoka Kolomije, lakini huwezi kuitoa Kolomije kichwani mwake
 
Siungi mkono upuuzi huu wa Bashite
Hakika huo upuuzi unakera sana.

Ila huyo Bashite ni waziri katika serikali mbovu ya Samia.
Huwezi kutenganisha waziri na serikali, aitha utapenda vyote au kuchukia vyote pale linapotokea jambo la kuudhi au la kufurahisha.

Kama huu ubadhirifu na matumizi mabaya ya cheo ni ya kweli na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na aliyemweka madarakani, basi kumchukia Makonda huko ni kumwonea wivu.

Makonda endelea kula 'minyama' mpaka watu wote waone nyeupe na nyeusi ya hii serikali dhalimu iliyopora madaraka..
 
Back
Top Bottom