Hakika sasa nimeamini kuwa CCM imeishiwa propagandist, kama hawa vijana wa mitandaoni ndio wanategemewa kukitetea chama kama propagandist wa chama basi tena, mbona wanaishiwa pumzi fasta wanapopambana na hoja nzito. vitisho,matusi ndo imekuwa njia rahisi kwao ya kumaliza hoja zinazo wakabili kukitetea chama dah mnaiuwa CCM masikini. Ila niwakubushe jambo moja la msingi kule mwanzo Mwl Nyerere alisomesha watu kwa ajili hiyo , wenzangu hiyo ni taaruma sio ili mradi una ka android unajiita mfia chama,kutwa nzima kujibu ovyo watu na kutoa vitisho kwa taarifa yenu mmeshageuka waua chama. Kukitetea chama kilichoko madarakani ni kazi ngumu inahitaji, upeo mzuri wa kupima mambo,uelewa,elimu ya kutosha utaalamu wa kusoma saikolojia za watu pia kupima upepo na kutambua upi upepo hatari na upepo mzuri kwa chama, hivyo kuwa na uwezo wa kutuliza hali inapochafuka na sio vitisho na rugha chafu.
Mhe Polepole watoe watu wako mtandaoni kwanza wapeleke kivukoni mkawapige msasa walau wiki mbili kisha tafuteni jinsi ya kuwasomesha kuwa wana propaganda. MSIJE MKADHANI ZAMANI WATU WALIKUWA WAJINGA ILA KULIKUWA NA PROPAGANDIST WAZURI WALIOBOBEA KAMA AKINA NGOMBARE,MOSES NAUYE na wenine wengi.Tambueni kuwa kwa sasa mnapingwa kuliko wakati wowote ule KWENYE HISTORIA YA CHAMA,kama mnabisha hebu ruhusuni mikutano ya kisiasa hata kwa mwezi mmoja tu hapo ndipo mtatambua namaanisha nini ila wangu ni ushauri tu bye.