Bashe anusurika kutekwa

Bashe anusurika kutekwa

JUMAMOSI, MACHI 30, 2013 01:07 NA MWANDISHI WETU, DAR

WIMBI la viongozi wakuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, kuendelea kuwindwa na watu wasiofahamika, limeendelea kushika kasi, baada ya usiku wa kumkia jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Hussein Bashe, kunusurika kutekwa.

Tukio hilo, lilitokea juzi usiku wakati Bashe alipokuwa akitoka ofisini kwake Sinza Kijiweni, akielekea nyumbani kwake Mbezi.

Akizungumzia tukio hilo, Bashe alisema wakati anaondoka ofisini kwake kwa gari lake, alianza kufuatiliwa kwa nyuma na magari mawili, likiwamo aina ya NOA ambalo hata hivyo hakufanikiwa kujua lilikuwa na watu wangapi.

"Kama kawaida nilishinda ofisini kwa ajili ya majukumu yangu ya kazi na muda wa kutoka ulipowadia, niliondoka kurudi nyumbani.

"Awali wakati navuka geti la pale ofisini, sikuwa na shaka yoyote, lakini kadri nilivyozidi kuendelea na safari yangu, niliona nyuma nafuatiliwa na magari mawili ambayo yalikuwa yakiendeshwa kwa tahadhari.

"Nilipofika Mwenge ile NOA ilikuwa bado iko nyuma yangu, sasa nikaanza kupatwa na wasiwasi, nikajua hapa kuna jambo.

"Moyoni niliendelea kumuomba Mungu, huku nikijiuliza maswali mengi hawa jamaa ni akina nani, kwa kweli sikupata jibu zuri.

"Nilipofika Mbezi, niliona yale magari yanazidi kunisogelea, kwa hiyo, nikaamua kuongeza kasi na wao wakazidi kuja tu.

"Wakati niko Mbezi jirani na njia panda ya kwenda kwangu, gari moja lilinipita kwa kasi na kuendelea mbele.

"Unajua kuelekea kwangu pale kuna barabara kama tatu ambazo zote unaweza kuzitumia na zikakufikisha hadi nyumbani kwangu," alisema Bashe na kuongeza:

"Nilichokifanya nilipita barabara ya kwanza na wao wakapita barabara ya pili na ghafla nilikutana nao uso kwa uso, wakati huo naelekea kwangu na kibaya zaidi, gari lao walizima taa kubwa na kuacha ndogo.

"Walivyona gari langu, walinipiga taa kuashiria wanakata kona, lakini cha ajabu walinifuata nyuma na hapo nikaanza kujua sasa nafuatiliwa.

"Nilichokifanya sikwenda nyumbani moja kwa moja, bali niliamua kupaki gari kwenye grosari moja iliyoko jirani na kwangu.

"Baadaye niliamua kuondoka ili niwazunguke kwa nyuma nisome namba za gari lao, lakini sikufanikiwa kwa sababu taa za nyuma zilikuwa zimezimwa," alisema Bashe.

Kwa mujibu wa Bashe, baadaye aliingia nyumbani kwake na kuwakuta wageni ambao alikaa nao hadi saa sita usiku baada ya kuwasimulia tukio lilivyokuwa.

"Sasa basi, wakati jamaa zangu hao wanaondoka kurudi kwao, walikuta lile gari pale pale njiani, wakanipigia simu, kwamba lile gari nililowasimulia linawafuatilia.

"Nikawaambia wageuze gari lao ili wasome namba, lakini hawakufanikiwa hata kidogo kwa sababu wale jamaa walishtuka na kuamua kutimua.

"Kwa hiyo, nilichokifanya nilikwenda pale Polisi Kawe na kutoa taarifa ambapo nilipewa RB yenye namba KW/RB/2899/2013," alisema.

Machi 6, mwaka huu, Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alitekwa na kuteswa na watu wasiofahamika.

Katika tukio hilo, Kibanda alitobolewa jicho la kushoto, alipigwa kichwani na kitu chenye ncha kali na kunyofolewa kucha. Kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini ambako anaendelea na matibabu

Hii ni ya kupikwa.......Hakuna ukweli hapa.....

Haina tofauti na Hekaya za Abunuwasi............

Ni muendelezo wa Bashe na New Habari Corp. kuendelea kutumika...............

Bashe na wenzako acheni kutumika na kupotosha/kujenga hofu kwa watanzania.....
 
Matunda ya Rwakatare.

Matunda ya EL, anyway Bashe ajaribu kujilinda mwenyewe asitegemee ulinzi kutoka kwenye taasisi ya serikali kwani ana maadui wengi tu ndani ya CCM pia nje kwenye Biashara za EL&Rostam kamwe hawatamwacha bila kuwa marked kama threat kwao, Hivi ile Bastola aliyomtishia Kigwangalla kule Nzega bado ipo Polisi?

Endapo kweli aligundua mapema kuwa anafuatwa basi yeye alitakiwa kuwaarifu jamaa wa karibu yake nao wachukue gari na kuwafuatilia hao jamaa kwa nyuma na wangeweza kujua namba za gari kwa urahisi kabisa kuliko juhudi alizotumia yeye binaafsi
 
Hii Tz sasa inaendelea kuwa nchi yenye kuleta hofu nyingi juu ya usalama wa raia. Maana kwa sasa kila raia ana taharuki kubwa na usalama wa maisha yake. Nchi imejaa rushwa, watu masikini, udini, ukabila na sasa linaongezeka ugaidi. Maana hata ukiripoti polisi hakuna reaction yoyote hasa kwa mipango ambayo inaratibiwa na serikali au watu wenye nguvu kubwa ya kifedha na ushawishi mkubwa serikalini.
Haka kamchezo ni katamu ila kna uchungu ndani yake! Hao New Habari corporation wamekuwa king makers. Mwaka 2005 magazeti ya Rai na Mtanzania and fellows ndio walimpamba sana kikwete chini ya Salva Rweyemamu ambaye kwa sasa anakula shavu ikulu na ndio mpaka sasa watanzana tunahangaikakutokana na kuingizwa chaka na haya magazet kuwa JK ni kiboko ya matatizo ya watanzania huku wakituaminisha kuwa wagombea wengine hamna kitu!. Sasa inawezekana kabisa wapinzan wenu ndani ya CCM wanaoutaka urais na ambao wanajua mbinu iliyotumika kuuingiza madarakani huu utawala uliopo wanataka kuzima hizo mbinu kabla hazijafanikiwa!
Poleni lakini kwa kuandamwa na kama mnasimamia haki basi hao wanaowawinda watashindwa!
 
JUMAMOSI, MACHI 30, 2013 01:07 NA MWANDISHI WETU, DAR

WIMBI la viongozi wakuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, kuendelea kuwindwa na watu wasiofahamika, limeendelea kushika kasi, baada ya usiku wa kumkia jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Hussein Bashe, kunusurika kutekwa.

Tukio hilo, lilitokea juzi usiku wakati Bashe alipokuwa akitoka ofisini kwake Sinza Kijiweni, akielekea nyumbani kwake Mbezi.

Akizungumzia tukio hilo, Bashe alisema wakati anaondoka ofisini kwake kwa gari lake, alianza kufuatiliwa kwa nyuma na magari mawili, likiwamo aina ya NOA ambalo hata hivyo hakufanikiwa kujua lilikuwa na watu wangapi.

“Kama kawaida nilishinda ofisini kwa ajili ya majukumu yangu ya kazi na muda wa kutoka ulipowadia, niliondoka kurudi nyumbani.

“Awali wakati navuka geti la pale ofisini, sikuwa na shaka yoyote, lakini kadri nilivyozidi kuendelea na safari yangu, niliona nyuma nafuatiliwa na magari mawili ambayo yalikuwa yakiendeshwa kwa tahadhari.

“Nilipofika Mwenge ile NOA ilikuwa bado iko nyuma yangu, sasa nikaanza kupatwa na wasiwasi, nikajua hapa kuna jambo.

“Moyoni niliendelea kumuomba Mungu, huku nikijiuliza maswali mengi hawa jamaa ni akina nani, kwa kweli sikupata jibu zuri.

“Nilipofika Mbezi, niliona yale magari yanazidi kunisogelea, kwa hiyo, nikaamua kuongeza kasi na wao wakazidi kuja tu.

“Wakati niko Mbezi jirani na njia panda ya kwenda kwangu, gari moja lilinipita kwa kasi na kuendelea mbele.

“Unajua kuelekea kwangu pale kuna barabara kama tatu ambazo zote unaweza kuzitumia na zikakufikisha hadi nyumbani kwangu,” alisema Bashe na kuongeza:

“Nilichokifanya nilipita barabara ya kwanza na wao wakapita barabara ya pili na ghafla nilikutana nao uso kwa uso, wakati huo naelekea kwangu na kibaya zaidi, gari lao walizima taa kubwa na kuacha ndogo.

“Walivyona gari langu, walinipiga taa kuashiria wanakata kona, lakini cha ajabu walinifuata nyuma na hapo nikaanza kujua sasa nafuatiliwa.

“Nilichokifanya sikwenda nyumbani moja kwa moja, bali niliamua kupaki gari kwenye grosari moja iliyoko jirani na kwangu.

“Baadaye niliamua kuondoka ili niwazunguke kwa nyuma nisome namba za gari lao, lakini sikufanikiwa kwa sababu taa za nyuma zilikuwa zimezimwa,” alisema Bashe.

Kwa mujibu wa Bashe, baadaye aliingia nyumbani kwake na kuwakuta wageni ambao alikaa nao hadi saa sita usiku baada ya kuwasimulia tukio lilivyokuwa.

“Sasa basi, wakati jamaa zangu hao wanaondoka kurudi kwao, walikuta lile gari pale pale njiani, wakanipigia simu, kwamba lile gari nililowasimulia linawafuatilia.

“Nikawaambia wageuze gari lao ili wasome namba, lakini hawakufanikiwa hata kidogo kwa sababu wale jamaa walishtuka na kuamua kutimua.

“Kwa hiyo, nilichokifanya nilikwenda pale Polisi Kawe na kutoa taarifa ambapo nilipewa RB yenye namba KW/RB/2899/2013,” alisema.

Machi 6, mwaka huu, Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alitekwa na kuteswa na watu wasiofahamika.

Katika tukio hilo, Kibanda alitobolewa jicho la kushoto, alipigwa kichwani na kitu chenye ncha kali na kunyofolewa kucha. Kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini ambako anaendelea na matibabu

Hii siyo style nyingine ya kutafuta umaarufu?
 
Hapa katikati magazeti yenu hasa mtanzania yameandika sana habari za lwakatare na chadema na jana kuna thred ilirushwa hapa kwamba akina shonza wanatoa taarifa kwenu ili mzitoe kuumbua chadema unadhani mtapona?
 
Wakati mwakyembe akilalamika juu ya maisha yake alitaja mpaka watu na magari yaliyotaka kumteka hatukusikia polisi wakikamata au kufatilia magari hayo lakini bado matukio hayo yameendelea ila nataka hii story inaweza kuwa kweli au ya kupika muda sahihi wa kutoa taarifa ilikuwa pale wakati anafatiliwa sijui alikuwa anajiamini nini kuwa anaweza kufika kwake salama angeweza kutoa taarifa hata kwenye vyombo vya habari kwamba ninafatiliwa na wakati huo huo kuripoti polisi hii taarifa ina walakini lakini usalama wote huu shakani kutokana na kila mtu hasa mataifa yenye vita raia wake kuingia nchini
 
Bashe kapika SINEMA hii ili ku-draw attention ya watu.Kwanza amejuaje kama wanakuja kumteka?Je kama lengo ni kumpiga risasi na kuishia, wangempata vizuri aliposhuka hapo glossary.Ni ishara gani zilizoonyesha kwamba wanamfuata ili wamteke?

Nakubaliana na hoja yako.
Ingawa hali iliopo sasa hivi walio wengi wanatembea kwa tahadhari kutokana na matukio ya kutekwa kisha kungolewa meno, macho na kucha bila ganzi, lakini tukio la huyu Bashe haliingii akilini mwangu mtu ufuatwe kitambo kirefu hivyo wakati ana nafasi ya kuwasiliana na vyombo vya usalama wafuatilie nani anamfuata kwa nyuma, na pengine angeweza kuendelea na safari hadi kuishia kitu cha polisi badala ya kwenda moja kwa moja nyumbani kama alikuwa na hakika anafuatwa. Kuna kitu hakijakaa sawa hapa.
 
Membe akamatwe apewe masharti iwapo bashe lowassa dr slaa watadhurika atashitakiwa.
 
...nchi hii kama una meno, kucha, korodani, unapinga baadhi ya mambo...eti unalazimishwa kukaa kimya!!
Wao wanajua kuliko wote.
Kazi ipo.
 
Bashe pole sana aisee!

Bahati mbaya hao jamaa sio "kondoo" wapatikane kwa urahisi!
 
watamtambua yule brothermen,hamkujua mwanzoni kuwa urais ni mbio za kufa na kupona !
 
JUMAMOSI, MACHI 30, 2013 01:07 NA MWANDISHI WETU, DAR

WIMBI la viongozi wakuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, kuendelea kuwindwa na watu wasiofahamika, limeendelea kushika kasi, baada ya usiku wa kumkia jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Hussein Bashe, kunusurika kutekwa.

Tukio hilo, lilitokea juzi usiku wakati Bashe alipokuwa akitoka ofisini kwake Sinza Kijiweni, akielekea nyumbani kwake Mbezi.

Akizungumzia tukio hilo, Bashe alisema wakati anaondoka ofisini kwake kwa gari lake, alianza kufuatiliwa kwa nyuma na magari mawili, likiwamo aina ya NOA ambalo hata hivyo hakufanikiwa kujua lilikuwa na watu wangapi.

“Kama kawaida nilishinda ofisini kwa ajili ya majukumu yangu ya kazi na muda wa kutoka ulipowadia, niliondoka kurudi nyumbani.

“Awali wakati navuka geti la pale ofisini, sikuwa na shaka yoyote, lakini kadri nilivyozidi kuendelea na safari yangu, niliona nyuma nafuatiliwa na magari mawili ambayo yalikuwa yakiendeshwa kwa tahadhari.

“Nilipofika Mwenge ile NOA ilikuwa bado iko nyuma yangu, sasa nikaanza kupatwa na wasiwasi, nikajua hapa kuna jambo.

“Moyoni niliendelea kumuomba Mungu, huku nikijiuliza maswali mengi hawa jamaa ni akina nani, kwa kweli sikupata jibu zuri.

“Nilipofika Mbezi, niliona yale magari yanazidi kunisogelea, kwa hiyo, nikaamua kuongeza kasi na wao wakazidi kuja tu.

“Wakati niko Mbezi jirani na njia panda ya kwenda kwangu, gari moja lilinipita kwa kasi na kuendelea mbele.

“Unajua kuelekea kwangu pale kuna barabara kama tatu ambazo zote unaweza kuzitumia na zikakufikisha hadi nyumbani kwangu,” alisema Bashe na kuongeza:

“Nilichokifanya nilipita barabara ya kwanza na wao wakapita barabara ya pili na ghafla nilikutana nao uso kwa uso, wakati huo naelekea kwangu na kibaya zaidi, gari lao walizima taa kubwa na kuacha ndogo.

“Walivyona gari langu, walinipiga taa kuashiria wanakata kona, lakini cha ajabu walinifuata nyuma na hapo nikaanza kujua sasa nafuatiliwa.

“Nilichokifanya sikwenda nyumbani moja kwa moja, bali niliamua kupaki gari kwenye grosari moja iliyoko jirani na kwangu.

“Baadaye niliamua kuondoka ili niwazunguke kwa nyuma nisome namba za gari lao, lakini sikufanikiwa kwa sababu taa za nyuma zilikuwa zimezimwa,” alisema Bashe.

Kwa mujibu wa Bashe, baadaye aliingia nyumbani kwake na kuwakuta wageni ambao alikaa nao hadi saa sita usiku baada ya kuwasimulia tukio lilivyokuwa.

“Sasa basi, wakati jamaa zangu hao wanaondoka kurudi kwao, walikuta lile gari pale pale njiani, wakanipigia simu, kwamba lile gari nililowasimulia linawafuatilia.

“Nikawaambia wageuze gari lao ili wasome namba, lakini hawakufanikiwa hata kidogo kwa sababu wale jamaa walishtuka na kuamua kutimua.

“Kwa hiyo, nilichokifanya nilikwenda pale Polisi Kawe na kutoa taarifa ambapo nilipewa RB yenye namba KW/RB/2899/2013,” alisema.

Machi 6, mwaka huu, Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alitekwa na kuteswa na watu wasiofahamika.

Katika tukio hilo, Kibanda alitobolewa jicho la kushoto, alipigwa kichwani na kitu chenye ncha kali na kunyofolewa kucha. Kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini ambako anaendelea na matibabu

Kinachosumbua ni vita ya ma CCM! Kuiingiza CHADEMA!!
Yakigombana yenyewe poa tu si yana malizana nguvu...!!
 
Au ile Vita na Mzee wa
ndoto bado wanawindana na kulipana visasi?urais 2015 tutakimbiana hapa
nchini na kuuaana!

du membe mbona alisema akiuchukua urais watu watakimbia nchi mbona wameanza mapema.
 
Back
Top Bottom