Bashe anusurika kutekwa

Bashe anusurika kutekwa



JUMAMOSI, MACHI 30, 2013 01:07 NA MWANDISHI WETU, DAR

WIMBI la viongozi wakuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, kuendelea kuwindwa na watu wasiofahamika, limeendelea kushika kasi, baada ya usiku wa kumkia jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Hussein Bashe, kunusurika kutekwa.

Tukio hilo, lilitokea juzi usiku wakati Bashe alipokuwa akitoka ofisini kwake Sinza Kijiweni, akielekea nyumbani kwake Mbezi.

Akizungumzia tukio hilo, Bashe alisema wakati anaondoka ofisini kwake kwa gari lake, alianza kufuatiliwa kwa nyuma na magari mawili, likiwamo aina ya NOA ambalo hata hivyo hakufanikiwa kujua lilikuwa na watu wangapi.

“Kama kawaida nilishinda ofisini kwa ajili ya majukumu yangu ya kazi na muda wa kutoka ulipowadia, niliondoka kurudi nyumbani.

“Awali wakati navuka geti la pale ofisini, sikuwa na shaka yoyote, lakini kadri nilivyozidi kuendelea na safari yangu, niliona nyuma nafuatiliwa na magari mawili ambayo yalikuwa yakiendeshwa kwa tahadhari.

“Nilipofika Mwenge ile NOA ilikuwa bado iko nyuma yangu, sasa nikaanza kupatwa na wasiwasi, nikajua hapa kuna jambo.

“Moyoni niliendelea kumuomba Mungu, huku nikijiuliza maswali mengi hawa jamaa ni akina nani, kwa kweli sikupata jibu zuri.

“Nilipofika Mbezi, niliona yale magari yanazidi kunisogelea, kwa hiyo, nikaamua kuongeza kasi na wao wakazidi kuja tu.

“Wakati niko Mbezi jirani na njia panda ya kwenda kwangu, gari moja lilinipita kwa kasi na kuendelea mbele.

“Unajua kuelekea kwangu pale kuna barabara kama tatu ambazo zote unaweza kuzitumia na zikakufikisha hadi nyumbani kwangu,” alisema Bashe na kuongeza:

“Nilichokifanya nilipita barabara ya kwanza na wao wakapita barabara ya pili na ghafla nilikutana nao uso kwa uso, wakati huo naelekea kwangu na kibaya zaidi, gari lao walizima taa kubwa na kuacha ndogo.

“Walivyona gari langu, walinipiga taa kuashiria wanakata kona, lakini cha ajabu walinifuata nyuma na hapo nikaanza kujua sasa nafuatiliwa.

“Nilichokifanya sikwenda nyumbani moja kwa moja, bali niliamua kupaki gari kwenye grosari moja iliyoko jirani na kwangu.

“Baadaye niliamua kuondoka ili niwazunguke kwa nyuma nisome namba za gari lao, lakini sikufanikiwa kwa sababu taa za nyuma zilikuwa zimezimwa,” alisema Bashe.

Kwa mujibu wa Bashe, baadaye aliingia nyumbani kwake na kuwakuta wageni ambao alikaa nao hadi saa sita usiku baada ya kuwasimulia tukio lilivyokuwa.

“Sasa basi, wakati jamaa zangu hao wanaondoka kurudi kwao, walikuta lile gari pale pale njiani, wakanipigia simu, kwamba lile gari nililowasimulia linawafuatilia.

“Nikawaambia wageuze gari lao ili wasome namba, lakini hawakufanikiwa hata kidogo kwa sababu wale jamaa walishtuka na kuamua kutimua.

“Kwa hiyo, nilichokifanya nilikwenda pale Polisi Kawe na kutoa taarifa ambapo nilipewa RB yenye namba KW/RB/2899/2013,” alisema.

Machi 6, mwaka huu, Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alitekwa na kuteswa na watu wasiofahamika.

Katika tukio hilo, Kibanda alitobolewa jicho la kushoto, alipigwa kichwani na kitu chenye ncha kali na kunyofolewa kucha. Kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini ambako anaendelea na matibabu



hamna habari hapo. ni udaku tu wa bashe ili aendelee kuuza gazeti lake. njaa hizi balaa. kama walikutana uso kwa uso iweje asione namba za hilo gari?
 
hii stori mbona ipo kama imechonwa vile. muda wote ufuatiliwe halafu ushindwe kutoa taarifa polisi. ina maana Bashe hana contact za watu ambao wangeweza kujua hiyo noah wakati anaelekea kwake. maanake isije ikawa ni alibi ya kutaka huruma ya watu. lazima hii taarifa tuipokee kwa tahadhari kubwa. la mwisho kwani Bashe yeye mbaya wake si mmoja tuu na anamfahamu na alikwishamtaja kule Dodoma labda angempigia simu na kumuuliza vipi mzee.
kumbe nawe umeona..hawa jamaa wanatuchezea akili.ina maana hadi sasa hawana hata system ya kujihakikishia usalama wa wenyewe?mtu unafuatiliwa zaidi ya nusu saa unapitia grocery kuzuga,bado wako na wewe,kama haamini polis si angeomba watu pale grocery wamsaidie kuwakamata hao jamaa na kuwahoji?
 
Hapo nunua bastola

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Operesheni ng'oa kucha, meno na macho bila ganzi inaendelea. Je ni nani yuko nyuma ya matukio haya?
Sidhani kama bwana mdogo Kigwangala ana maujuzi haya.
Uraia wa Bashe nao uko mashakani licha ya kuwa Uhamiaji ilisha tusadikisha kuwa Bashe ni raia halali wa Tz

hawa jamaa hata ukisema ung'oe kucha uwapelekee watakataa wanataka wafanye wenyewe.mzee wa madui 11 kwani unahitaji kucha za watu wangapi ili agenda yako ifanikiwe?
 
Naona akili yangu imegoma kuikubali hadithi hii, labda kama msimuliaji/mwandishi angetahadharisha kuwa "hadithi hii ni ya kubuni tu, haihusiani na mazingira wala tukio lolote la kweli".
Haiwezekani atoke tu ofisini astukie kuwa anafuatiliwa halafu aanze kuongozana nao akiwapeleka nyumbani kwake.
 
Bashe usituharibie tz yetu.
1: una marafiki kibao usalama tena wakubwa kwa nn hukuwapigia simu?
2:huna namba za marafiki zako polisi?
3:Kwa nn hukuwapigia hata jamaa zako? Mkeo .nk?
4:E N L mzee wa mvi swahiba wako ulimjulisha kabla?
5: Wafanyakazi wenzio hasa waandamizi ungewaambia wakufuate nyuma baada ya kuhisi hatari. Acha uzushi bashe una marafiik wengi .
 
Naanza kuwa na mashaka sasa, ila bashe atambue kuwa wakati mwingine itakapokuwa kweli watu bado watajua anatania. Kwanini asipige simu hata kwa watu wengine anaowaamini wajaribu kuwa nae karibu kujua hao ni nani? Hainijii akilini kusema eti hata baada ya kupark grocery bado alishindwa kusoma namba ya gari? Hata jamaa zake walioikuta gari pale pale wakati wanatoka kwake na kawasimulia yote ina maana hawakuwasha taa kuona namba ya hiyo gari? Naona sinema inachezwa hapa, some people are forcibly looking for public symphathy for their political good, let us be pretty careful please....
 
Mbona kama hii habari ya kutungwa? Janja ya kutaka kuuza magazeti yenu Uchwara,
 
Rwakatare huyu

Hawa Jamaaa wana akili za Kipoyoyo,kwa muda wiki mbili sasa wamekuwa waki iandama Chadema nadhani ni makusudi ili wajiteke waseme ni Chadema At Work.

Hivi huyu hata silaha hana? Anaogopa nini sasa? Kuanzia sinza hadi mwenge anafuatiliwa hana number ya pOlisi ya doria? Mbona pikipiki na defender za diria zinakuwa nyingi tu usiku? Si achukue number zao na siku ikitokea hivyo awapigie ili waweze kuwa ambush hao Magaidi ?
 
Rwakatare huyu

Kwa hiyo unataka kusema anatoa order toka mahabusu? Acha hizo, I guess wote bado tunasubiri ukweli.

Ila Duh inabidi awe na bodigadi sasa maana wana chama cha Malafi watamtafuta tena tu.
 
hii stori mbona ipo kama imechonwa vile. muda wote ufuatiliwe halafu ushindwe kutoa taarifa polisi. ina maana Bashe hana contact za watu ambao wangeweza kujua hiyo noah wakati anaelekea kwake. maanake isije ikawa ni alibi ya kutaka huruma ya watu. lazima hii taarifa tuipokee kwa tahadhari kubwa. la mwisho kwani Bashe yeye mbaya wake si mmoja tuu na anamfahamu na alikwishamtaja kule Dodoma labda angempigia simu na kumuuliza vipi mzee.
Hata mimi napatwa na mashaka na habari hii hasa ukiona alivyolishughulikia suala hili.
Siku kadhaa zilizopita tulisoma jinsi Bashe na Kibanda walivyofuatiliwa wakati wakitoka ofisini. Baada ya muda Kibanda akavamiwa na kujeruhiwa. Halafu leo Bashe anagundua kuwa anafuatiliwa na gari mbili halafu anakwenda kusimama kwenye glosary ili asome namba za hayo magari.
Ni kweli ni muhimu kujua namba lakini kwa insticts za kawaida kwa mwanadamu anayejikuta katika hali kama hii kujiokoa ndiko kunakuwa suala la kipaumbele na si kuanza kuwachunguza adui zako.
Kwa nini wakati alipofika kwake akawasimulia wageni yaliyomkuta na asitafute msaada wa vyombo vya dola? Ana namba ya Nchimbi, 0mwema na Kova lakini hakutaka kuwasiliana nao.
Nadhani unahitajika ufafanuzi ili kuifanya habari iaminike zaidi


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kama alifuatwa muda wote huo na yeye kama mhusika na chombo cha habari ana njia nyingi tu za mawasiliano na vyombo vya usalama, kwa nini hakufanya hivyo?
 
Bashe ni usanii huo, yuko kazini kuendesha propaganda dhidi ya Membe wakati huohuo akimfagilia EL
 
Wa Tz Tuache unafiki matukio haya yapo TZ na tukubali Kuwa serikali au inayapuzia au imeshindwa mbinu na hawa magaidi.h
UBinafsi wetu ndio utafanya vitendo hivi vya kiovu vindelee.

Leo kwa kibanda, kesho BAshe na keshokutwa yaweza Kuwa Kwako.

TUache ushabiki wa kisiasa tuweke utaifa Mbele na ubinadam.
Kwa kifupi Tz inatisha sana sasa hivi, kwani vitendo vya ute kaji nyara na kuteswa vinazidi kupamba moto Siku hadi Siku!
 
Sinema nyingine hii.Kwani Lwakatare yuko nje kwa dhamana?Bashe bashe!unataka kukimbia kivuli chako mwenyewe!Nafikiri kigwangala atakuwa amecheka sana baada ya kusoma habari hii.
Nunua dawa ya ganzi utembee nayo ndani ya gari.Jamaa huwa hawatumii ganzi
 
Last edited by a moderator:
Mambo madogo sana haya wananchi tukiamua kushughulika nao.tatizo ni hili naliongea mara kwa mara humu,wapo wananchi wa aina hii wenye uthubutu wa kula sahani moja na serikali?
 
Bashe kapika SINEMA hii ili ku-draw attention ya watu.Kwanza amejuaje kama wanakuja kumteka?Je kama lengo ni kumpiga risasi na kuishia, wangempata vizuri aliposhuka hapo glossary.Ni ishara gani zilizoonyesha kwamba wanamfuata ili wamteke?
Kama alifuatwa muda wote huo na yeye kama mhusika na chombo cha habari ana njia nyingi tu za mawasiliano na vyombo vya usalama, kwa nini hakufanya hivyo?
 
Back
Top Bottom