Bashe anusurika kutekwa

Bashe anusurika kutekwa

Rwakatare na Ludovic naona wanataka kumshikisha adabu msomali
 
Bado wanaendeleza mipango yao ya kupanga mauaji na mateso?
 
JUMAMOSI, MACHI 30, 2013 01:07 NA MWANDISHI WETU, DAR

WIMBI la viongozi wakuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, kuendelea kuwindwa na watu wasiofahamika, limeendelea kushika kasi, baada ya usiku wa kumkia jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Hussein Bashe, kunusurika kutekwa.

Tukio hilo, lilitokea juzi usiku wakati Bashe alipokuwa akitoka ofisini kwake Sinza Kijiweni, akielekea nyumbani kwake Mbezi.

Akizungumzia tukio hilo, Bashe alisema wakati anaondoka ofisini kwake kwa gari lake, alianza kufuatiliwa kwa nyuma na magari mawili, likiwamo aina ya NOA ambalo hata hivyo hakufanikiwa kujua lilikuwa na watu wangapi.

“Kama kawaida nilishinda ofisini kwa ajili ya majukumu yangu ya kazi na muda wa kutoka ulipowadia, niliondoka kurudi nyumbani.

“Awali wakati navuka geti la pale ofisini, sikuwa na shaka yoyote, lakini kadri nilivyozidi kuendelea na safari yangu, niliona nyuma nafuatiliwa na magari mawili ambayo yalikuwa yakiendeshwa kwa tahadhari.

“Nilipofika Mwenge ile NOA ilikuwa bado iko nyuma yangu, sasa nikaanza kupatwa na wasiwasi, nikajua hapa kuna jambo.

“Moyoni niliendelea kumuomba Mungu, huku nikijiuliza maswali mengi hawa jamaa ni akina nani, kwa kweli sikupata jibu zuri.

“Nilipofika Mbezi, niliona yale magari yanazidi kunisogelea, kwa hiyo, nikaamua kuongeza kasi na wao wakazidi kuja tu.

“Wakati niko Mbezi jirani na njia panda ya kwenda kwangu, gari moja lilinipita kwa kasi na kuendelea mbele.

“Unajua kuelekea kwangu pale kuna barabara kama tatu ambazo zote unaweza kuzitumia na zikakufikisha hadi nyumbani kwangu,” alisema Bashe na kuongeza:

“Nilichokifanya nilipita barabara ya kwanza na wao wakapita barabara ya pili na ghafla nilikutana nao uso kwa uso, wakati huo naelekea kwangu na kibaya zaidi, gari lao walizima taa kubwa na kuacha ndogo.

“Walivyona gari langu, walinipiga taa kuashiria wanakata kona, lakini cha ajabu walinifuata nyuma na hapo nikaanza kujua sasa nafuatiliwa.

“Nilichokifanya sikwenda nyumbani moja kwa moja, bali niliamua kupaki gari kwenye grosari moja iliyoko jirani na kwangu.

“Baadaye niliamua kuondoka ili niwazunguke kwa nyuma nisome namba za gari lao, lakini sikufanikiwa kwa sababu taa za nyuma zilikuwa zimezimwa,” alisema Bashe.

Kwa mujibu wa Bashe, baadaye aliingia nyumbani kwake na kuwakuta wageni ambao alikaa nao hadi saa sita usiku baada ya kuwasimulia tukio lilivyokuwa.

“Sasa basi, wakati jamaa zangu hao wanaondoka kurudi kwao, walikuta lile gari pale pale njiani, wakanipigia simu, kwamba lile gari nililowasimulia linawafuatilia.

“Nikawaambia wageuze gari lao ili wasome namba, lakini hawakufanikiwa hata kidogo kwa sababu wale jamaa walishtuka na kuamua kutimua.

“Kwa hiyo, nilichokifanya nilikwenda pale Polisi Kawe na kutoa taarifa ambapo nilipewa RB yenye namba KW/RB/2899/2013,” alisema.

Machi 6, mwaka huu, Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alitekwa na kuteswa na watu wasiofahamika.

Katika tukio hilo, Kibanda alitobolewa jicho la kushoto, alipigwa kichwani na kitu chenye ncha kali na kunyofolewa kucha. Kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini ambako anaendelea na matibabu

Muongo tu...itawezekanaje ugundue unafuatiliwa tokea sinza ukae kimya.Kwa nini hukupiga simu polisi kuwa unafuatiliwa wangeweza kuwahi na kuwakamata mapema.Ulisubiri ufike kwako ili iweje?halafu utashindwa kusoma namba za nyuma wakati zinang'aa usiku....hao jamaa zako walishindwaje kuchukua namba za gari kwanza badala yake wakakimbilia kukupigia simu,unasema eti wakakimbia na bado pia wameshindwa kuchukua namba?

Bashe acha maigizo ya kitoto
 
Yote haya kisa urais haya malizaneni tu'
 
Pole sana bwana bashe,nazani sasa anza kujifua ili ung'olewe bila kusikia maumivu makali....mbaya wenu wandishi mnamjua...nawatajiasasa...polisi...na ccm hii lakini kwani ugomvi wako na membe ulifika wapi?
 
Mmiliki wa new habar 2006 ni Rostam azizi! swahiba wa dhaifu! Lets wait and see.......still loading.....
 
Yaani kufuatiliwa kote huko akashindwa kusoma Namba za gari.
Aaache uongo huyo Msomali
 
"Nilichokifanya nilipita barabara ya kwanza na wao wakapita barabara ya pili na ghafla nilikutana nao uso kwa uso, wakati huo naelekea kwangu na kibaya zaidi, gari lao walizima taa kubwa na kuacha ndogo.

"Walivyona gari langu, walinipiga taa kuashiria wanakata kona, lakini cha ajabu walinifuata nyuma na hapo nikaanza kujua sasa nafuatiliwa.

Ina maana hao Jamaa baada ya Kupishana nao wali kula U-turn, mbona hakuna Correletaion hapa, amekutana nao Uso kwa Uso, wakampiga Taa (sijui indicator) kuonesha wanakata kona)
Ghafla wakaanza kumfuatilia kwa Nyuma, Huyu Msomali itabid arudi kwao aisee, ni Muongo ajabu

"Nikawaambia wageuze gari lao ili wasome namba, lakini hawakufanikiwa hata kidogo kwa sababu wale jamaa walishtuka na kuamua kutimua.
Yaan hao jamaa walishtuka kuwa Ndugu zake Bashe wanataka Kusoma Number za Gari Lao, Duu, huu ni uongo Mtakatifu aisee.

My take
Haieleweki kuwa Target ilikuwa ni Bashe au Wageni wake
Namshauri Bashe aache Siasa za kutaka kuhurumiwa, atulie alambishwe Dawa, hapa Sio Somalia
 
Hapa Bashe atawadanganya baadhi ya manazi wa Chadema na wapenda majungu wa CCM tu.

Huhitaji degree kujua kwamba hii habari ni ya kutunga.
 
Operesheni ng'oa kucha, meno na macho bila ganzi inaendelea. Je ni nani yuko nyuma ya matukio haya?
Sidhani kama bwana mdogo Kigwangala ana maujuzi haya.
Uraia wa Bashe nao uko mashakani licha ya kuwa Uhamiaji ilisha tusadikisha kuwa Bashe ni raia halali wa Tz

Kwani huyu Bashe hawezi kuwa mmoja kati ya maadui kumi na moja waliotangazwa? Kama ni mmoja wao basi hana sababu ya kumtafuta mchawi wake!!!
 
tunakoelekea sasa itabidi tutembee na dawa za ganzi ili ikitokea kutekwa unawaomba kwanza watekaji walau sekunde 1 ugonge doz yako kisha waendelee na process zao.

Watz wote bila kujali vyama vyetu tuko hatari,hakuna kiongozi wa juu mwenye dhamira ya dhati yakutaka sisi raia wa kawaida tuwe na maisha bora,kazi nikuwindana tu nakufitiniana tu
 
Mtzamo wangu hamna kitu hapo! Wanawin public sympathy, kibanda wamemfix wenyewe na wanayeyusha jamii iamini ni mtu x
 
Wahah!! Mkamateni bashe na nape na Ritz kama kuna mtu atang'olewa tena kucha . Hitakaa itokee tena.
 
Ushahidi kuwa kibanda walimfix ni article ya juzi ya zitto ambayo sidhan kibanda angeruhusu mambo ya mwaka juzi yarudiwe
 
Genge la watoa meno na kucha ni usalama wakishirikiana na miungu watu flani, ila hawaamini kama Mungu yupo, hebu tusubir
 
Mimi wala sishangai tena. Hizi ni sakarakasi za wanasiasa wa CCM wanaowania urais 2015 na wafuasi wao, waandishi wa habari walionunuliwa na hizo kambi za kuwania urais, polisi na usalama wa taifa, chini ya uongozi dhaifu wa Kikwete
 
JUMAMOSI, MACHI 30, 2013 01:07 NA MWANDISHI WETU, DAR

WIMBI la viongozi wakuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, kuendelea kuwindwa na watu wasiofahamika, limeendelea kushika kasi, baada ya usiku wa kumkia jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Hussein Bashe, kunusurika kutekwa.

Tukio hilo, lilitokea juzi usiku wakati Bashe alipokuwa akitoka ofisini kwake Sinza Kijiweni, akielekea nyumbani kwake Mbezi.

Akizungumzia tukio hilo, Bashe alisema wakati anaondoka ofisini kwake kwa gari lake, alianza kufuatiliwa kwa nyuma na magari mawili, likiwamo aina ya NOA ambalo hata hivyo hakufanikiwa kujua lilikuwa na watu wangapi.

“Kama kawaida nilishinda ofisini kwa ajili ya majukumu yangu ya kazi na muda wa kutoka ulipowadia, niliondoka kurudi nyumbani.

“Awali wakati navuka geti la pale ofisini, sikuwa na shaka yoyote, lakini kadri nilivyozidi kuendelea na safari yangu, niliona nyuma nafuatiliwa na magari mawili ambayo yalikuwa yakiendeshwa kwa tahadhari.

“Nilipofika Mwenge ile NOA ilikuwa bado iko nyuma yangu, sasa nikaanza kupatwa na wasiwasi, nikajua hapa kuna jambo.

“Moyoni niliendelea kumuomba Mungu, huku nikijiuliza maswali mengi hawa jamaa ni akina nani, kwa kweli sikupata jibu zuri.

“Nilipofika Mbezi, niliona yale magari yanazidi kunisogelea, kwa hiyo, nikaamua kuongeza kasi na wao wakazidi kuja tu.

“Wakati niko Mbezi jirani na njia panda ya kwenda kwangu, gari moja lilinipita kwa kasi na kuendelea mbele.

“Unajua kuelekea kwangu pale kuna barabara kama tatu ambazo zote unaweza kuzitumia na zikakufikisha hadi nyumbani kwangu,” alisema Bashe na kuongeza:

“Nilichokifanya nilipita barabara ya kwanza na wao wakapita barabara ya pili na ghafla nilikutana nao uso kwa uso, wakati huo naelekea kwangu na kibaya zaidi, gari lao walizima taa kubwa na kuacha ndogo.

“Walivyona gari langu, walinipiga taa kuashiria wanakata kona, lakini cha ajabu walinifuata nyuma na hapo nikaanza kujua sasa nafuatiliwa.

“Nilichokifanya sikwenda nyumbani moja kwa moja, bali niliamua kupaki gari kwenye grosari moja iliyoko jirani na kwangu.

“Baadaye niliamua kuondoka ili niwazunguke kwa nyuma nisome namba za gari lao, lakini sikufanikiwa kwa sababu taa za nyuma zilikuwa zimezimwa,” alisema Bashe.

Kwa mujibu wa Bashe, baadaye aliingia nyumbani kwake na kuwakuta wageni ambao alikaa nao hadi saa sita usiku baada ya kuwasimulia tukio lilivyokuwa.

“Sasa basi, wakati jamaa zangu hao wanaondoka kurudi kwao, walikuta lile gari pale pale njiani, wakanipigia simu, kwamba lile gari nililowasimulia linawafuatilia.

“Nikawaambia wageuze gari lao ili wasome namba, lakini hawakufanikiwa hata kidogo kwa sababu wale jamaa walishtuka na kuamua kutimua.

“Kwa hiyo, nilichokifanya nilikwenda pale Polisi Kawe na kutoa taarifa ambapo nilipewa RB yenye namba KW/RB/2899/2013,” alisema.

Machi 6, mwaka huu, Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alitekwa na kuteswa na watu wasiofahamika.

Katika tukio hilo, Kibanda alitobolewa jicho la kushoto, alipigwa kichwani na kitu chenye ncha kali na kunyofolewa kucha. Kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini ambako anaendelea na matibabu

Udhalimu huu una mwisho wake, hawa watekaji sijui ndo wanaahadi ya kuishi milele?! Pole ndugu
 
..urais mzuri,"at the expense of other peoples life" .......
 
Back
Top Bottom