Bashe anusurika kutekwa

Bashe anusurika kutekwa

Dah.. kwa mtindo huu inabidi tung'oe kucha na meno tuvifungie majumbani maana inaonyesha wanavitafuta sana, sijui ni baada ya kumaliza tembo!!??
 
Plate number kutoifahamu hata kwa kutumia ubunifu?????????? Huu ni usanii tu.
 
'Ninao maadui 11,kati yao wamo waandishi wa habari wawili.Hawa watakimbia nchi 2016 baada ya uchaguzi mkuu' Mheshimiwa fulani(napenda meno,kucha na macho yangu) kwenye kipindi cha 'dakika 45'ITV.
Labda upo kwenye hiyo 1st 11 mzee. Kila mmoja wetu awe na hadhari.
 
'Ninao
maadui 11,kati yao wamo waandishi wa habari wawili.Hawa watakimbia nchi
2016 baada ya uchaguzi mkuu'
Mheshimiwa
fulani(napenda meno,kucha na macho yangu)
kwenye kipindi cha 'dakika 45'ITV.
Labda upo kwenye hiyo 1st 11 mzee. Kila mmoja wetu awe na
hadhari.

me me m meno yangu kwenye mi embe
 
hii stori mbona ipo kama imechonwa vile. muda wote ufuatiliwe halafu ushindwe kutoa taarifa polisi. ina maana Bashe hana contact za watu ambao wangeweza kujua hiyo noah wakati anaelekea kwake. maanake isije ikawa ni alibi ya kutaka huruma ya watu. lazima hii taarifa tuipokee kwa tahadhari kubwa. la mwisho kwani Bashe yeye mbaya wake si mmoja tuu na anamfahamu na alikwishamtaja kule Dodoma labda angempigia simu na kumuuliza vipi mzee.

Haswaa!
hii tunapigwa kamba
 
JUMAMOSI, MACHI 30, 2013 01:07NA MWANDISHI WETU, DAR

WIMBI la viongozi wakuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, kuendelea kuwindwa na watu wasiofahamika, limeendelea kushika kasi, baada ya usiku wa kumkia jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Hussein Bashe, kunusurika kutekwa.

Tukio hilo, lilitokea juzi usiku wakati Bashe alipokuwa akitoka ofisini kwake Sinza Kijiweni, akielekea nyumbani kwake Mbezi.

Akizungumzia tukio hilo, Bashe alisema wakati anaondoka ofisini kwake kwa gari lake, alianza kufuatiliwa kwa nyuma na magari mawili, likiwamo aina ya NOA ambalo hata hivyo hakufanikiwa kujua lilikuwa na watu wangapi.

“Kama kawaida nilishinda ofisini kwa ajili ya majukumu yangu ya kazi na muda wa kutoka ulipowadia, niliondoka kurudi nyumbani.

“Awali wakati navuka geti la pale ofisini, sikuwa na shaka yoyote, lakini kadri nilivyozidi kuendelea na safari yangu, niliona nyuma nafuatiliwa na magari mawili ambayo yalikuwa yakiendeshwa kwa tahadhari.

“Nilipofika Mwenge ile NOA ilikuwa bado iko nyuma yangu, sasa nikaanza kupatwa na wasiwasi, nikajua hapa kuna jambo.

“Moyoni niliendelea kumuomba Mungu, huku nikijiuliza maswali mengi hawa jamaa ni akina nani, kwa kweli sikupata jibu zuri.

“Nilipofika Mbezi, niliona yale magari yanazidi kunisogelea, kwa hiyo, nikaamua kuongeza kasi na wao wakazidi kuja tu.

“Wakati niko Mbezi jirani na njia panda ya kwenda kwangu, gari moja lilinipita kwa kasi na kuendelea mbele.

“Unajua kuelekea kwangu pale kuna barabara kama tatu ambazo zote unaweza kuzitumia na zikakufikisha hadi nyumbani kwangu,” alisema Bashe na kuongeza:

“Nilichokifanya nilipita barabara ya kwanza na wao wakapita barabara ya pili na ghafla nilikutana nao uso kwa uso, wakati huo naelekea kwangu na kibaya zaidi, gari lao walizima taa kubwa na kuacha ndogo.

“Walivyona gari langu, walinipiga taa kuashiria wanakata kona, lakini cha ajabu walinifuata nyuma na hapo nikaanza kujua sasa nafuatiliwa.

“Nilichokifanya sikwenda nyumbani moja kwa moja, bali niliamua kupaki gari kwenye grosari moja iliyoko jirani na kwangu.

“Baadaye niliamua kuondoka ili niwazunguke kwa nyuma nisome namba za gari lao, lakini sikufanikiwa kwa sababu taa za nyuma zilikuwa zimezimwa,” alisema Bashe.

Kwa mujibu wa Bashe, baadaye aliingia nyumbani kwake na kuwakuta wageni ambao alikaa nao hadi saa sita usiku baada ya kuwasimulia tukio lilivyokuwa.

“Sasa basi, wakati jamaa zangu hao wanaondoka kurudi kwao, walikuta lile gari pale pale njiani, wakanipigia simu, kwamba lile gari nililowasimulia linawafuatilia.

“Nikawaambia wageuze gari lao ili wasome namba, lakini hawakufanikiwa hata kidogo kwa sababu wale jamaa walishtuka na kuamua kutimua.

“Kwa hiyo, nilichokifanya nilikwenda pale Polisi Kawe na kutoa taarifa ambapo nilipewa RB yenye namba KW/RB/2899/2013,” alisema.

Machi 6, mwaka huu, Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alitekwa na kuteswa na watu wasiofahamika.

Katika tukio hilo, Kibanda alitobolewa jicho la kushoto, alipigwa kichwani na kitu chenye ncha kali na kunyofolewa kucha. Kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini ambako anaendelea na matibabu

kila kitu ugaidi tutajuaje kama aliiba mke wa mtu au amemrusha mtu pesa
 
Sasa huyu bashe, kuendesha gari kutoka bamaga mpaka mbezi bado umeshindwa kushika numba? uemkutana nao uso kwa uso bado ukashindwa kupiga hata picha? We mwandishi wa aina gani?...Job true true....
 
Sote tunajua ni nani adui wa Bashe,haihitaji phd(only kama aliyoyasema bashe ni ya kweli)

"waandish wawili wa habari"...jiandaeni kuhama nchi 2016(hapa jamaa ana maana ya yeye akishakuwa Rais!!!!!!!!!!!!!!)
 
Wanaendelea kama kawaida hawana wa kuwakemea
 
Huu ni usanii mkubwa sana wa kutaka kutufanya wananchi hatuna akili,hizi ni mbinu chafu kabisa za kisiasa zinazojaribu kuwajengea wananchi imani kua kiongozi fulani hafai,ikumbukwe kwamba Bashe yupo kwenye kundi fulani linalopigania ucku na mchana kufa na kupona kuwania urais 2015,sasa wanataka kumpaka mpinzani wao mkubwa matope kwamba yeye ndiye yupo nyuma ya ugaidi huu.
Na kama kuna kosa kubwa ambalo alishawahi lifanya mpinzani wao huyo ni kutangaza ana maadui 11 ambao atawashughulikia ifikapo 2016(nadhani baada ya kushika nchi) sasa wanatumia maneno (kauli) yake hiyo kuwaaminisha wananchi kwamba huyu mtu hafai (MTU WA VISASI) japo ni kwa kuwatesa ikibidi kuwaua wale ambao wanadhani ni maadui wake,napenda kuwapa taadhari wale wote wanaojijua wapo kwenye ile "list" ya mheshimiwa huyo wanaweza wakatekwa kuteswa hata kuuwawa kwa malengo ya kumporomosha mtu katika medani ya kisiasa(Haya ni maoni yangu tu)
Haya yaweza tokea kati sasa hadi uchaguzi mkuu upite.
 
Kutoka sinza hadi tegeta unapoishi wewe ni umbali mrefu sana. Je wakati unafatiliwa nawe ukajua hilo ulimpigia nani simu ili akusaidie? Na kwa hadhi yako unafahamiana na viongozi wengi hata wa kwenye vyombo vya dola. Don ful us
 
Sasa huyu bashe, kuendesha gari kutoka bamaga mpaka mbezi bado umeshindwa kushika numba? uemkutana nao uso kwa uso bado ukashindwa kupiga hata picha? We mwandishi wa aina gani?...Job true true....

maswali ya msingi sana hayo nami nimejiuliza na kumuuliza pia. Inakuwaje njia pekee ya kujihami iwe ni kuingia bar badala ya kupiga simu kwa watu muhimu wakusaidie? Pengine ingekuwa ni siku ya arobaini ya mwizi, bashe ameshindwa kutusaidia
 
Lakini pia ikumbukwe kuwa ukweli wa wanasiasa ni pale atakapokwambia mama yako ni mwanamke.
 
JUMAMOSI, MACHI 30, 2013 01:07 NA MWANDISHI WETU, DAR

WIMBI la viongozi wakuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, kuendelea kuwindwa na watu wasiofahamika, limeendelea kushika kasi, baada ya usiku wa kumkia jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Hussein Bashe, kunusurika kutekwa.

Tukio hilo, lilitokea juzi usiku wakati Bashe alipokuwa akitoka ofisini kwake Sinza Kijiweni, akielekea nyumbani kwake Mbezi.

Akizungumzia tukio hilo, Bashe alisema wakati anaondoka ofisini kwake kwa gari lake, alianza kufuatiliwa kwa nyuma na magari mawili, likiwamo aina ya NOA ambalo hata hivyo hakufanikiwa kujua lilikuwa na watu wangapi.

“Kama kawaida nilishinda ofisini kwa ajili ya majukumu yangu ya kazi na muda wa kutoka ulipowadia, niliondoka kurudi nyumbani.

“Awali wakati navuka geti la pale ofisini, sikuwa na shaka yoyote, lakini kadri nilivyozidi kuendelea na safari yangu, niliona nyuma nafuatiliwa na magari mawili ambayo yalikuwa yakiendeshwa kwa tahadhari.

“Nilipofika Mwenge ile NOA ilikuwa bado iko nyuma yangu, sasa nikaanza kupatwa na wasiwasi, nikajua hapa kuna jambo.

“Moyoni niliendelea kumuomba Mungu, huku nikijiuliza maswali mengi hawa jamaa ni akina nani, kwa kweli sikupata jibu zuri.

“Nilipofika Mbezi, niliona yale magari yanazidi kunisogelea, kwa hiyo, nikaamua kuongeza kasi na wao wakazidi kuja tu.

“Wakati niko Mbezi jirani na njia panda ya kwenda kwangu, gari moja lilinipita kwa kasi na kuendelea mbele.

“Unajua kuelekea kwangu pale kuna barabara kama tatu ambazo zote unaweza kuzitumia na zikakufikisha hadi nyumbani kwangu,” alisema Bashe na kuongeza:

“Nilichokifanya nilipita barabara ya kwanza na wao wakapita barabara ya pili na ghafla nilikutana nao uso kwa uso, wakati huo naelekea kwangu na kibaya zaidi, gari lao walizima taa kubwa na kuacha ndogo.

“Walivyona gari langu, walinipiga taa kuashiria wanakata kona, lakini cha ajabu walinifuata nyuma na hapo nikaanza kujua sasa nafuatiliwa.

“Nilichokifanya sikwenda nyumbani moja kwa moja, bali niliamua kupaki gari kwenye grosari moja iliyoko jirani na kwangu.

“Baadaye niliamua kuondoka ili niwazunguke kwa nyuma nisome namba za gari lao, lakini sikufanikiwa kwa sababu taa za nyuma zilikuwa zimezimwa,” alisema Bashe.

Kwa mujibu wa Bashe, baadaye aliingia nyumbani kwake na kuwakuta wageni ambao alikaa nao hadi saa sita usiku baada ya kuwasimulia tukio lilivyokuwa.

“Sasa basi, wakati jamaa zangu hao wanaondoka kurudi kwao, walikuta lile gari pale pale njiani, wakanipigia simu, kwamba lile gari nililowasimulia linawafuatilia.

“Nikawaambia wageuze gari lao ili wasome namba, lakini hawakufanikiwa hata kidogo kwa sababu wale jamaa walishtuka na kuamua kutimua.

“Kwa hiyo, nilichokifanya nilikwenda pale Polisi Kawe na kutoa taarifa ambapo nilipewa RB yenye namba KW/RB/2899/2013,” alisema.

Machi 6, mwaka huu, Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alitekwa na kuteswa na watu wasiofahamika.

Katika tukio hilo, Kibanda alitobolewa jicho la kushoto, alipigwa kichwani na kitu chenye ncha kali na kunyofolewa kucha. Kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini ambako anaendelea na matibabu

...........Yaani kwa mbinu zote kutoka sinza had kwako hukuweza kupata mbinu ya kusoma namba za hzo gari? ungewapigia watu wa boda boda wangekufanyia kazi hiyo......
 
Yaani wang'oe watu kucha bila ganzi....halafu tena wanatoa) hahahaha.this is tanzania,
 
Ni heri sie malofa wenye vibarua vya 500,000 kwa mwezi tunaishi kwa raha kuliko matajiri wanaoishi kwa hofu kila siku,

Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
 
Back
Top Bottom