BASATA yawafungia Diamond Platnumz na Rayvanny kufanya onesho lolote. Tamasha la Wasafi lafutiwa kibali. 'Nyegezi' yawaponza

Nimekumbuka kale kawimbo alikotoa kipindi Roma ametekwa .. Bora nikae kimya...kweli usikae kimya ukijua wewe hayajakukuta
 
Diamond hawashitaki tu hawa Basata ,waendelee na shoo tu mpaka.kesi ya msingi isikilizwe
 
Nafikiri mtu au watu walioiandika hii Barua hawakuzisoma Kanuni za BASATA vizuri..
Wameandika barua lakini hawakukariri kifungu cha kanuni kilichovunjwa..
Kanuni yoyote ya BASATA ikivunjwa kuna adhabu zifuatazo..

30. –(1) chama, kikundi, asasi au mtu yeyote atakayebainika kuvunja au kukiuka kifungu chochote cha Kanuni hizi anaweza kuchukuliwa hatua zifuatazo:
(a) Kutozwa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini (Sh. 50,000/=)
(b) Kufutiwa usajili
(c) Kusimamishwa kuendesha hughuli za sanaa
(d) Kuzuiwa kujishughulisha na kazi za sanaa kwa kipindi kisichopungua miezi sita

(e) Kuzuiwa kujishughulisha na kazi za sanaa maisha, kwa kubainika kujihusisha na vitendo vya kupokea au kutoa rushwa.

Hakuna neno au kifungu kinachosomeka 'Kufungiwa' katika kanuni hizo..
 
Tatizo letu wabongo ni wivu, nahis kuna mijitu huko basata inamwonea diamond wivu, hivi wataifungiaje nyimbo wakati ishasambaa mitandaoni??
 
Nyie acheni hizi movie ni political spinning kuwatoa kufuatilia tamko la la zito kukoncentrate na upuuzi wa diamond open ur minds think outside the box.....diamond ataperform kama kawaida Kenya......

.hizo ni pollitics tactics kuwatoa kwenye mswaada wa maana kuanza kudiscuss ujinga
 
Tatizo hawa watoto wanakosa nidhamu ktk kiwango cha juu sana....sana sana sana,ni nani aliyekuwa anajua kama kuna siku mtu kama Manji Yusuf angawekwa gerezani kama ilivyokuwa kipindi kile?

Nani aliyewahi hata kuhisi tu kwamba hawa wawili Rugemalila na mwenzake Seth kuna siku wangewekwa kizuini pasiwepo wakuwatoa?lazima tuishi tukiangalia nyakati,sasa wakati usiojulikana ni muda gani huo?

Wanaweza kupotea kwenye ramani wajiangalie sana,kufungiwa kwao asilaumiwe mtu yeyote ni ujinga wao na utoto wanaouendekeza umewafikisha hapa.
Kwanza angalia waliomzunguka kuanzia manager wake wote la saba. Wenzao kina Rooney la saba lakini wana wasomi wa kuwashauri. Kina David Beckham la saba wamezungukwa na watu wa maana. Kina Diamond kama kina Ebuoye
 
Lakini diamond ana hatari ya kuporomoka kimuziki kama ataendekeza nyimbo zipate promo kwa kuimba matusi. Nyimbo kama Lala salama aliyoimba zamani zilibebwa na sauti nzuri. Sasa aliyemdanganya kuibukia matusi ni nani sijui. Hats Kwangwaru ni ovyo ingawa ndio inaongoza kwa view wengi Kyle you tube. Kijana amefika peak yake sasa graph yake itaanza kushuka . Hata sauti yake inakwaruza sasa hivi labda vocal cords amezioverwork kwa show nyingi zinakaribia kugoma. Hata Celine Dion aliwahi kufanyiwa operation huko nyuma kwa sababu kuimba sana zinastretch mno au labda kama anakunywa pombe Kali ndio anaziharibu kabisa. Walio karibu naye wamshauri hakuna mwanamuziki anayekaa kileleni kwa zaidi ya miaka kumi naye inakaribia. Kwa sababu kwenye kundi lake (wasafi)sasa hivi kuna vijana wanamzidi melody nzuri ya sauti Harmonize na Rayvanny wakiongoza .Uzuri diamond si mbinafsi anaweza akavuta miaka na wasafi yake. Nye
 
daharau gni izo n utov upi w nidham waliofnya..
Nipo hapa najiuliza, au kapiga huo wimbo kwenye show za hapa ndani..? BARUA haijajitosheleza mkuu wangu

Mi nahisi ni mwendelezo wa kuongeza watakao ishi kama mashetani.

Ila dogo naye akome ... kipindi kile watu wanalialia yeye anasema 'bora mi nikae kimya' wacha akae kimya vizuri.
 
Hawa vijana lazima walilewa na kuamua kuimba kwa makusudi hao wanaojiita mameneja walikuwa wapi mpaka wanamziki wao wanaimba vilivyokatazwa na mamlaka husika ,huku ni kujaribu kupima nguvu ya Baraza ,nachojiuliza tamasha lilikuwa zuri alitengeneza platform ya wasanii wengine kupata pesa ,sasa wamepigwa stop ,nani atakaye waombea msamaa wakati wanafanya makosa ya makusudi
 
Inaeleza kuwa wakina Diamond wamevunja Sheria lakini hakuna kitungu Cha Sheria kilichoainishwa.
Inawafungia kwa muda usiojulikana, hii ni hukumu ambayo haipo kwenye Sheria yoyote ile.
Walisikilizwa lini?
Basata wamewafungia ndani na nje, je Sheria zao zinafanya kazi nje ya nchi?
Je wamejiuliza Ni kumbi na maeneo mangapi yanapiga huo wimbo?
Dr.Tulia anajua maana ya maadili? Wabunge wetu wanajua maana ya maadili? Waliruka majoka Burundi na akuna aliyekemea
 
Back
Top Bottom