BASATA yawafungia Diamond Platnumz na Rayvanny kufanya onesho lolote. Tamasha la Wasafi lafutiwa kibali. 'Nyegezi' yawaponza

Inaeleza kuwa wakina Diamond wamevunja Sheria lakini hakuna kitungu Cha Sheria kilichoainishwa.
Inawafungia kwa muda usiojulikana, hii ni hukumu ambayo haipo kwenye Sheria yoyote ile.
Walisikilizwa lini?
Basata wamewafungia ndani na nje, je Sheria zao zinafanya kazi nje ya nchi?
Je wamejiuliza Ni kumbi na maeneo mangapi yanapiga huo wimbo?
Dr.Tulia anajua maana ya maadili? Wabunge wetu wanajua maana ya maadili? Waliruka majoka Burundi na akuna aliyekemea
 
Ndio ubaya wa kuwa na viongozi ambao hawajawai ata kuwa madansa wa mziki kwenye taasisi ya mziki km basata
 
Huu ni uamuzi wa chuki na kutaka kumshusha mtu mweny akili timamu hawezi kufanya ujinga huu kuufungia show huku akijua wazamini kibao wanaendesha biashara zao
pia hizi show zinafanyika usiku ambapo watoto hawaruhusiwi nilitegemea basata wataangalia hili
 
Nafikiri mtu au watu walioiandika hii Barua hawakuzisoma Kanuni za BASATA vizuri..
Wameandika barua lakini hawakukariri kifungu cha kanuni kilichovunjwa..
Kanuni yoyote ya BASATA ikivunjwa kuna adhabu zifuatazo..

30. –(1) chama, kikundi, asasi au mtu yeyote atakayebainika kuvunja au kukiuka kifungu chochote cha Kanuni hizi anaweza kuchukuliwa hatua zifuatazo:
(a) Kutozwa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini (Sh. 50,000/=)
(b) Kufutiwa usajili
(c) Kusimamishwa kuendesha hughuli za sanaa
(d) Kuzuiwa kujishughulisha na kazi za sanaa kwa kipindi kisichopungua miezi sita

(e) Kuzuiwa kujishughulisha na kazi za sanaa maisha, kwa kubainika kujihusisha na vitendo vya kupokea au kutoa rushwa.

Hakuna neno au kifungu kinachosomeka 'Kufungiwa' katika kanuni hizo..
Soma kifungu cha 30(1)d
 
Sasa mbona wamesema muda usiojulikana
Hicho kifungu kipo very technical...unafungiwa muda usiopungua miezi sita...inaweza kuwa miezi 7,12....ama muda wwte kuzidi miezi 6...ila hakunaga adhabu isiyo na ukomo that is unlawful....hapo wamechemka
 
Ukiachia kuwafungia, hizi mamlaka zilipaswa kuwapeleka mahakamani.

Hatuwezi kua na watu wanaodharau mamlaka zilizopo kisheria na wakaachwa.

Usishangae muda mfupi ujao hawa watu wakaanza tena kufanya maonyesho, bashite akiingilia kati haichukui muda.
Baraza gani na wakati wasanii wanaishi huani shenzi type eboooooh!!!
 
Huyu daimondi na wenzake wakiachiwa waendelee na ukosefu wa maadili wanao ufanya hakika kizazi chetu kitapoteza kabisaa maadili, anapaswa achukuliwe hatua kali zaidi ya hiyo hata ikiwezekana afikishwe mahakamani, hutuwezi kuwachekea wakati maadili ya watoto yanaharibika kutokana na nyimbo zake,tunataka wasanii wanao heshimu na kujali MAADILI ya jamii yake sio kama anavyo fanya huyu dimondi
 
Ivi ule waraka wa kufungia nyimbo unasemaj?
Nyimbo ilifungiwa kwenye vyombo vya habari pekee au hadi kwenye matamasha!
 
Iyo ndio tanzania

Anapondea shirika la ndege, shirka pendwa na JPM sasa unafikil watamuacha hiv hivi.
 
Back
Top Bottom