Tamasha la Utamaduni na Utalii lazinduliwa Bariadi

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
Tamasha kubwa la kimataifa la utamaduni na utalii linalojulikana kama Lake Zone Cultural and Tourism Festival limezinduliwa Bariadi Mkoani Simiyu.
IMG-20240316-WA0008.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mh. Anna Gidarya (katikati) akizindua rasmi Tamasha la kimataifa la Utamaduni na Utalii maarufu kama Lake Zone Cultural and Tourism Festival linaloandaliwa na Kilimanjaro One Travel and Tours. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Christina Emmanuel, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mohamed Hatibu, Afisa Maendeleo ya Vijana, Zena Mchujuko, Afisa wa Baraza la Sanaa la Taifa, Gabriel Awe na wageni wengine.

Uzinduzi huo umefanywa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.DK Yahaya Nawanda aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mh. Anna Gidarya na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali, wadau wa utamaduni na Utalii kutoka katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na mikoa jirani.

Mkuu huyo wa Mkoa aliipongeza kampuni ya Kilimanjaro One Travel and Tours kwa kubuni tamasha hili la Utamaduni na Utalii kwa Kanda ya Ziwa na kuamua lifanyike katika Mkoa wa Simiyu.
IMG-20240316-WA0006.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Kilimanjaro One Travel and Tours, Christina Emmanuel akizungumza wakati wa tukio hilo la uzinduzi.

Alisema utamaduni ni jambo kubwa la kujivunia na ni lazima uenziwe na kunendelezwa kwa nguvu zote kwa sababu ni urithi tuliopokea kutoka kwa babu zetu, hivyo na sisi hatuna budi kuuendeleza.

Amesema Tamasha hili litasaidia sana kutangaza utamaduni wa mkoa wa Simiyu kupitia shughuli mbalimbali zitakazofanyika na hivyo kuufanya mkoa ufahamike zaidi ndani na nje ya nchi.
IMG-20240316-WA0009.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mh. Anna Gidarya akifurahia moja ya burudani wakati wa uzinduzi huo.

“Nimearifiwa kuwa leo ni uzinduzi tu ili tupate kionjo cha kinachotarajiwa kufanyika mwezi wa saba 2024 ambapo kutakuwa na tamasha kubwa la siku tatu mfulululizo na litahusisha watu zaidi ya 7,000 wakiwemo washiriki wa maonyesho,”

“Hii ni hatua kubwa na ni fursa kwa washiriki kufanya biashara na kujifunza mambo mbalimbali wakati wa tamasha,”

“Hivyo, sekta ya utalii wa utamaduni itakuwa kwa sababu wageni wote watakaokuja watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya mkoa wetu na kujionea vivutio mbalimbali vikiwemo vya utamaduni,”amesema Mkuu wa Mkoa Dkt. Nawanda.

Ametoa wito wa maandalizi ya tamasha hilo kubwa kufanyika mapema ili kupata washiriki wengi kutoka ndani na nje ya nchi.

Vilevile amewapongeza waandaaji kwa kuuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya SIta za kuhakikisha utamaduni wetu unatangazwa na kuufanya kivutio kikubwa cha watalii wa ndani na nje ya nchi.

“Napenda kutoa wito kwa wadau mbalimbali, wakiwemo watu binafsi, mashirika, taasisi na makampuni kujitokeza kudhamini tamasha hili kubwa katika Kanda ya Ziwa na nchini kwa ujumla ili lifanyike kwa ukubwa unaostahili na kukuza utamaduni na utalii wetu hapa nchini,” amesema kuunga mkono ufanyikaji wa tamasha hili kwa hali na mali,”
IMG-20240316-WA0007.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mh. Anna Gidarya akizungumza wakati wa tukio hilo la uzinduzi

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na waandaaji wa tamasha hili kuhakikisha linafanyika kila mwaka na kuwa chachu ya maendeleo kiutamaduni na kiuchumi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kilimanjaro One Travel and Tours Christina Emmanuel amesema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo ambayo inajihusisha na masuala ya utalii na utamaduni kuandaa tamasha hili ambalo tunaamini litakuwa na muitikio mkubwa kwa wakazi wa Simiyu na mikoa ya jirani.

“Tamasha hili linatarajiwa kufanyika mwezi wa saba na ninayo furaha kukufahamisha kuwa litafanyika kwa siku tatu mfulululizo Julai 5, 6 na kilele chake kitakua Julai 7 ambapo pamoja na mambo mengine tunategemea kuwa na maonyesho mbalimbali ya masuala ya utamaduni na utalii katika Uwanja wa Halmashauri na kuwavutia washiriki na watazamaji zaidi ya 7000 kwa siku hizi tatu. Pia litakuwa na vionjo mbalimbali ikiwemo ngoma inayohusisha makabila ya Wagika na Wagulu,” ameongeza.
IMG-20240316-WA0005.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mh. Anna Gidarya akifurahia moja ya burudani wakati wa uzinduzi huo.

Ametoa wito kwa wafanyabiashara, makampuni, taasisi na mashirika kujitokeza na kuunga mkono kama njia moja wapo pia ya kuiunga mkono Serikali katika kuutangaza utamaduni na utalii wa nchi yetu.

Naye Afisa wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA) Gabriel Awe amewasifu waandaaji kwa kuandaa tamasha hilo katika kuendeleza utamaduni na Utalii hapa nchini, akitoa wito kwa wadau wengine kuliunga mkono tamasha hilo kwa hali na mali.

“Ni tamasha kubwa la aina yake ambalo sisi kama Watanzania tunapaswa kujivunia kuwa hili ni tamasha la kwetu kwa maendeleo ya utamaduni na utalii wetu,”

“Hivyo ni vema wadau wakajitokeza na kuhakikisha linakuwa tamasha kubwa zaidi na kuvutia watu kutoka mataifa ya nje kujua thamani ya utamaduni na utalii wetu hapa nchini,”amesema Awe
 
Back
Top Bottom