Ikumbukwe kati ya wasanii walioshiriki kumuingiza Jiwe Magogoni ni Diamond Platnumz, Simba, Chibu D Chibu Dee ama Dangote. Kwa kutumia kipawa chake cha kuimba alilisifu Jiwe kwa nyimbo na mapambio hadi likaibuka mshindi.
Siku chache baada ya uchaguzi, Tundu Lissu alikuja na ile nadharia ya Dikteta Uchwara. Katika kipindi hiki ni wachache tu walimuelewa Lissu, lakini sasa asilimia nyingi ya watanzania zaidi hata ya takwimu za TWAWEZA wanakubaliaba na hili.
Tutakubaliana kuwa siku Lissu alilitangaza jiwe kuwa ni rais wa ajabu alisherehesha na maneno ya Mchungaji wa kale wa Ujerumani, Martin Niemoller kuwa utawala zandiki humfikia kila mmoja kwa wakati wake ni vyema kuungana na kuukabili mapema kabla haujaota mizizi.
Leo mjana Diamond na Rayvanny wamefungiwa kushiriki sanaa kwa mida usiojulikana. Ni pigo kwao, ni pigo kwa familia, ni pigo kwa sanaaa na pia ni pigo kwa uchumi unaozidi kudoroa wa taifa. Poleni sana wasafi.
Lakini ni sharti tujue kuwa Ujerumani ya kale na Tanzania ya leo ni sawa. TUUNGANE SASA.