Barua: Zitto akataa posho za vikao

Barua: Zitto akataa posho za vikao

Watu mbwana wakikosa habari zakuleta imnyamaze kuliko kuwachafua viongozi imara wa chadema

Mimi wala sishangai nilijua ghiliba za CDM siku nyingi kuna baadhi ya mambo wanayapeka kisiasa zaidi hawasemi kweli.

Kabla cjajibu hii hoja ya chama chetu au chama changu nisaidieni huyu mleta hoja ninani kama cyo masaburi ninauwakika na wabunge wangu cyo vilazi kama ccm kwanza msipende kuwachafua akina mbowe lema wenje mnyika lissu halima mdee msigwa n.k wewe mleta hoja acha siasa za maji taka hicho chanzo chako kitakuwa cha jeiro na nape na nakitakuwa kina tumia masaburi

Mkuu kama unatenda haki ungejibu hoja. CHADEMA walikuja na hoja nzuuuri ya kukataa posho lakini tukaambiwa kuwa walikutana kwenye mkutano wao wa ndani wakashindwa kuelewana ikabidi wajichukulie posho kimyakimya. Ila cha kushangaza ni kwamba kwenye vyombo vya habari wanajifanya kwamba hataki posho!! KAma hawazitaki posho si wangefanya kama Zitto. Hapa inaonekana Zitto peke yake ndiye anayeishi kwa anayoyaamini. Katika suala la POSHO CHADEMA IMEKUWA KAMA MAVI YA MBUZI!! IMEKUWA VIPANDE VIPANDE!! Huu ni unafiki tu!!

Mbona wabunge wa CDM wapo humu hawalitolei maaelezo hili. Waje waseme kwenye kile kikao walikubaliana wasichukue posho au vp?

poshooooo. Niungane na wale wanaosema ilikuwa ni kushawishi kuzifuta posho za vikao. hata walipoomba pesa hizo ziingizwe kwenye bajeti line ya halimashauri zao, bado waligomewa kama sijasahau. Waliopendekeza pesa hizo walikuwa ni wabunge kutoka kigoma-NCCR+CDM.

posho wanaweza kuendelea kuzichukua, kwani wasipozichukua ccm, wataiba

Wakubwa nisaidieni, Mimi ni new comer ktk JF. Naomba nifundishwe namna ya kuweka avatar, kuchukua mchango wa mwana JF kwa lengo la kupongeza, kuhoji na kucoment.

Pia nifundisheni namna ya kuanzisha mada, na namna ya kuedit profile yangu.

ntanguliza shukrani,

Mbona wabunge wa CDM wapo humu hawalitolei maaelezo hili. Waje waseme kwenye kile kikao walikubaliana wasichukue posho au vp?

Naona wewe unataka kuigawa CHADEMA. Suala la posho ni tete hakika nakuambia si Regia Mtema au Mnyika atajitokeza humu na kuongelea kuhusu posho. Ukitaka kuwashika pabaya CHADEMA wewe ongelea posho tu basi!!

Wakubwa nisaidieni, Mimi ni new comer ktk JF. Naomba nifundishwe namna ya kuweka avatar, kuchukua mchango wa mwana JF kwa lengo la kupongeza, kuhoji na kucoment.

Pia nifundisheni namna ya kuanzisha mada, na namna ya kuedit profile yangu.

ntanguliza shukrani,

Mtafute asiyeonekana!! Kweli ni nyuuukama!!

nina swali dogo tu kwa aliyeanzisha hii topic,hivi wakiacha kuchukua hizo posho unajua zitaenda kwa nani?na ulielewa vizuri mantinic ya huo mjadala wa posho na kama uliuelewa hauoni kwamba wewe si mkweli kaka jamii hii?

Mi naomba tujiridhishe kwanza kwa kuwa na habari za uhakika kabla ya kuanza mashambulizi
Kuna aina ngapi za posho zinatolewa bungeni na ni vigezo gani vya kupata aina ya posho husika
Ni namna gani twaweza pata data zauhakika kuwa wabunge wote wamepata hizo posho isipokuwa hao wa2 tu?
Je bunge limeshatoa taarifa kwa umma kuwa wabunge wote wamechukua posho za aina zote?

Wanasiasa kigeugeu...chadema kigeugeu...,naye mbowe kigeuge..tundu lusu kigeugeu...mnyika kigeugeu....lema kigeugeu....wenjekigeugeu...chadema..unapomwamini mwanasiasa mwishowe anakugeukia.
Hata kama wangeacha hizo posho zingeishia mikononi mwa wajanja na zinsinge mnufaisha mtanzania wa kawaida.

Hata ukiangalia ofisi ya bunge imefanya mchezo wa kisiasa kutoa taarifa hii. Ilitaka Chadema waonekane kuwa wanafiki wakati wabunge wengi wa CCM wanapinga kuondolewa kwa posho za wabunge. That should be the issue na wala si unafiki wa Chadema. Sasa suala limegeuka kuwa Chadema badala ya kujiuliza ni kwa nini CCM inashikilia wapewe posho na kwamba hizo posho hazitoshi, ziongezwe.

Poor Jasusi..

Hili la posho mbona dogo sana. Hawa jamaa wa CHADEMA zile nafasi za VITI MAALUM nyingi wamegawia dada zao, wake zao wa zamani, mabinti zao, hawara zao, wafuasi na wasaidizi wao wa karibu,......

Whoever said Politics is a dirty game and Never Trust Politicians hakukosea kabisa

Napenda nifafanue masuala kadhaa hapa.
Moja, sisi kama Kambi ya Upinzani inayoundwa na CHADEMA tulikwishaamua kwamba posho za vikao sio stahili sahihi kwa Mbunge. Mnadhimu Mkuu wa Kambi alikwishaandika kwa Spika wa Bunge kutaka kutenganisha fomu za mahudhurio na fomu za posho. Mbunge wenje pia katika moja ya michango yake alisema Bunge litengenishe fomu hizi mbili.
Kuhusiana na mimi kama an indivual MP, nilipewa kazi na chama kama Waziri kivuli Fedha na tangazo la posho alilitoa Naibu wangu ndugu christina Lissu. Mie nikalitolea ufafanuzi kwa vyombo vya habari. Wabunge wa CCM wakaanza kunishambulia na kusema ni unafiki kwamba ninatangaza posho zifutwe ilhali nazichukua. Nikamwandikia Spika barua kuwa posho zangu ziende kwenye charity org jimboni kwangu. Hili nalo likaonekana kama ni unafiki pia. Nikaamua kuzikataa kabisa. Hivyo toka tarehe 8 Juni mimi sipokei posho ya vikao. Njia ninayotumia ni kutosaini mahudhurio Bungeni ili wasipate sababu ya kunilipa.
Sasa kuna mchangiaji hapa kasema usiposaini ndani ya siku tatu unaadhibiwa. Kanuni inasema Mbunge asipohudhuria MIKUTANO mitatu ya Bunge anakuwa amejifukuza ubunge. Tutofautishe mikutano na VIKAO. Kikao ni kila siku na mkutano ni session nzima, mfano session iliyopita ilikuwa ni mkutano wa 4 wa Bunge nk.
Sasa, ikitokea sitasaini pia katika mkutano wa 5 na wa 6 wanaweza kuanza mchakato wa kunifukuza Ubunge. Lakini je mchakato huo utategemea karatasi za mahudhurio tu? Kwa mfano, nikiwa Bungeni ninauliza swali au kuchangia hoja, hansard inarekodi kuwa nilikuwepo Bungeni. Karatasi ya mahudhurio inaonyesha sikuwepo Bungeni. Audio na video records zinaonyesha nilikuwepo Bungeni, watanifukuza kwa vigezo vipi?
Katika harakati lazima ni lazima kuchallenge rules ili zibadilike. Nadhani katika hili tutafanikiwa.
Hivyo, wabunge wa chadema sio wanafiki kwani tayari wameandika rasmi kutaka fomu tofauti za kujaza mahudhurio. Pili, Zitto hasaini kama njia ya kutoa changamoto kwa rules. Lakini pia ninaamini kwa dhati kabisa kwamba posho ya kikao (sitting allowance) sio stahili halali (legitimate?)Kwa mbunge anayelipwa mshahara kwa kazi ile ya kukaa na kutunga sheria, kuisimamia serikali na kuwakilisha wananchi.

Asante kwa ufafanuzi

Naona wewe unataka kuigawa CHADEMA. Suala la posho ni tete hakika nakuambia si Regia Mtema au Mnyika atajitokeza humu na kuongelea kuhusu posho. Ukitaka kuwashika pabaya CHADEMA wewe ongelea posho tu basi!!
Bora Mh. Zitto amesikia kilio changu amekuja hapa kuelezea nini kimetokea
Napenda nifafanue masuala kadhaa hapa.
Moja, sisi kama Kambi ya Upinzani inayoundwa na CHADEMA tulikwishaamua kwamba posho za vikao sio stahili sahihi kwa Mbunge. Mnadhimu Mkuu wa Kambi alikwishaandika kwa Spika wa Bunge kutaka kutenganisha fomu za mahudhurio na fomu za posho. Mbunge wenje pia katika moja ya michango yake alisema Bunge litengenishe fomu hizi mbili.
Kuhusiana na mimi kama an indivual MP, nilipewa kazi na chama kama Waziri kivuli Fedha na tangazo la posho alilitoa Naibu wangu ndugu christina Lissu. Mie nikalitolea ufafanuzi kwa vyombo vya habari. Wabunge wa CCM wakaanza kunishambulia na kusema ni unafiki kwamba ninatangaza posho zifutwe ilhali nazichukua. Nikamwandikia Spika barua kuwa posho zangu ziende kwenye charity org jimboni kwangu. Hili nalo likaonekana kama ni unafiki pia. Nikaamua kuzikataa kabisa. Hivyo toka tarehe 8 Juni mimi sipokei posho ya vikao. Njia ninayotumia ni kutosaini mahudhurio Bungeni ili wasipate sababu ya kunilipa.
Sasa kuna mchangiaji hapa kasema usiposaini ndani ya siku tatu unaadhibiwa. Kanuni inasema Mbunge asipohudhuria MIKUTANO mitatu ya Bunge anakuwa amejifukuza ubunge. Tutofautishe mikutano na VIKAO. Kikao ni kila siku na mkutano ni session nzima, mfano session iliyopita ilikuwa ni mkutano wa 4 wa Bunge nk.
Sasa, ikitokea sitasaini pia katika mkutano wa 5 na wa 6 wanaweza kuanza mchakato wa kunifukuza Ubunge. Lakini je mchakato huo utategemea karatasi za mahudhurio tu? Kwa mfano, nikiwa Bungeni ninauliza swali au kuchangia hoja, hansard inarekodi kuwa nilikuwepo Bungeni. Karatasi ya mahudhurio inaonyesha sikuwepo Bungeni. Audio na video records zinaonyesha nilikuwepo Bungeni, watanifukuza kwa vigezo vipi?
Katika harakati lazima ni lazima kuchallenge rules ili zibadilike. Nadhani katika hili tutafanikiwa.
Hivyo, wabunge wa chadema sio wanafiki kwani tayari wameandika rasmi kutaka fomu tofauti za kujaza mahudhurio. Pili, Zitto hasaini kama njia ya kutoa changamoto kwa rules. Lakini pia ninaamini kwa dhati kabisa kwamba posho ya kikao (sitting allowance) sio stahili halali (legitimate?)Kwa mbunge anayelipwa mshahara kwa kazi ile ya kukaa na kutunga sheria, kuisimamia serikali na kuwakilisha wananchi.
Kwa hiyo inamaanisha wabunge wa CDM wamelazimishwa kuchukua posho. Maana ukisign tu inapelekwa moja kwa moja bank,
kazi kweli kweli hii ishu ya posho

Mimi wala sishangai nilijua ghiliba za CDM siku nyingi kuna baadhi ya mambo wanayapeka kisiasa zaidi hawasemi kweli.
Ninavyo jua mimi lengo lao ilikuwa si kufuta sitting allowance za wabunge tu bali za watumishi wote wa umma wakiwemo wabunge sasa kama hilo halijafanikiwa unamwachia nani hizo pesa....

Back
Top Bottom