Barua: Zitto akataa posho za vikao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua: Zitto akataa posho za vikao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Jun 10, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ameiandikia barua Ofisi ya Bunge kuiomba isimamishe kumlipa posho zake zinazotokana na vikao vya Bunge kuanzia juzi. Zitto ametoa ombi hilo kwa barua rasmi aliyoiwakilisha kwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah Juni 7 mwaka huu.

  Barua yenyewe hii hapo chini

  View attachment BARUA YA ZITTO KUKATAA POSHO YA VIKAO.doc
   
 2. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2011
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  A good start ila bunge litupe imprest ya hela ya kamanda zito
   
 3. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  tunataka kopy ya barua hapa na sababu zake
   
 4. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ANAESTAHILI SIFA ASIFIWE SINA BUDI KUMPONGEZA MUHESHIMIWA ZITO KWA UWAMUZI WAKE (M/MUNGU AKUZIDISHIE)

  MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ameiandikia barua Ofisi ya Bunge kuiomba isimamishe kumlipa posho zake zinazotokana na vikao vya Bunge kuanzia juzi.Zitto ametoa ombi hilo kwa barua rasmi aliyoiwakilisha kwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah Juni 7 mwaka huu.

  Katika barua hiyo, ambayo gazeti hili limefanikiwa kuiona, Zitto alisema anaamini kuwa watumishi wa Serikali na wabunge, hawastahili kulipwa posho wanapohudhuria vikao rasmi vya uwajibikaji wao wa kawaida.

  Zitto alisema kuwa posho hiyo haistahili kulipwa kwake, wabunge wengine wala watumishi wa umma kwa kuwa kuhudhuria vikao ni sehemu ya kazi zao.

  "Kwa mujibu wa Sheria ya Utawala wa Bunge (National Assembly Act of 2008) na kwa mujibu wa Masharti ya Kazi za Mbunge niliyokabidhiwa, ninastahili kupata posho za vikao, (sitting allowances) kila ninapohudhuria vikao vya Bunge na Kamati zake,"alisema Zitto na kuongeza:

  "Ni imani yangu kuwa posho ya kikao haistahili kulipwa kwa mbunge na mtumishi mwingine yeyote wa Serikali kwani kuhudhuria kikao ni sehemu ya kazi yangu,".

  Kupitia barua hiyo, Zitto ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Fedha, alieleza kwamba amekuwa akipendekeza posho za vikao hivyo ifutwe, jambo ambalo pia limo katika mapendekezo ya chama chake (Chadema) katika Bajeti ya 2011/2012.

  "Nimekuwa nikipendekeza kuwa posho hii ifutwe. Chama changu cha Chadema pia kimependekeza jambo hili katika mapendekezo yake ya Bajeti 2011/2012," alisema Zitto na kuendelea:

  "Mpaka hapo mfumo wa kulipana posho za vikao utakapofutwa, ninaelekeza kwamba stahili zangu zote za posho zielekezwe katika Taasisi ya Kigoma Development Initiative (KDI).., utaratibu huu uanze kuanzia tarehe 8/6/2011."

  Katibu wa Bunge agoma kuizungumzia
  Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alipoulizwa jana kama amepokea barua hiyo ya Zitto, alisema kuwa, yeye kama mtendaji wa mhimili huo wa Dola, anapokea barua nyingi, hivyo si rahisi kukumbuka kama barua hiyo imefika ofisini kwake.

  Lakini akasema, hata kama barua hiyo itakuwa imemfikia ofisini, kanuni na taratibu haziruhusu Bunge kutangaza habari za mtu binafsi. Alisema ofisi yake hairuhusiwi kuandika masuala binafsi ya wabunge yanayofikishwa ofisini na kwamba hilo linawezekana ikiwa mhusika (Zitto), ameruhusu lifanyike kwa maandishi.

  "...Haturuhusiwi kuandika habari za mtu. Nikiwa Katibu wa Bunge, napokea barua nyingi 'personal' (binafsi), lakini kama yeye mwenyewe amewaambieni kuwa kaleta barua hiyo, basi mwambieni pia atuandikie barua kuturuhusu na sisi ili tulitangaze hilo," alisema Dk Kashililah.

  Bajeti ya posho kulipa walimu laki moja
  Uamuzi huo wa Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, umekuja huku taarifa za utafiti wa taasisi ya Policy Forum inayojihusisha na tafiti mbalimbali za sera zikionyesha kuwa, katika mwaka 2008/2009, Serikali katika bajeti yake ilitenga Sh506 bilioni kwa ajili ya malipo ya posho.

  Kwa mujibu wa utafiti huo, ambao taarifa yake ilitolewa mwaka uliopita, fedha hizo ni sawa na mishahara ya mwaka mzima kwa walimu 109,000 ambao ni robo tatu ya walimu wote nchini.

  Kwa mujibu wa utafiti huo mwaka 2009/10 kiasi cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya posho za watumishi wa umma kilikuwa sawa na asilimia 59 ya malipo ya wafanyakazi wa ngazi ya chini .
   
 5. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  great; ila angependekeza hiyo imprest ifanye kitu gani cha maendeleo, isije ikaishia kwenye other expensis za bunge!
   
 6. m

  mzalendo2 Senior Member

  #6
  Jun 10, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  zitto huyu jamaa anafaa kuwa rais wetu 2015
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Mw. JK Nyerere is listening to us

  moral practice indeed .... well done zitto
   
 8. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  safi sana muheshimiwa mbunge ZITO
   
 9. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Amependekeza zipelekwe Taasisi ya Kigoma Development Initiative (KDI).

   
 10. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #10
  Jun 10, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Zitto aache janja yake! Anatupiga tu wananchi changa la macho. Hii Kigoma Development Initiative(KDI) ni NGO yake mwenyewe! So hizo allowance zinamrudia yeye mwenyewe!
   
 11. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #11
  Jun 10, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Good move Zitto na kuongeza credibility cdm nzima individually not as a team wazikatae then wazielekeze somewhere ili watu waone faida yake.
   
 12. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #12
  Jun 10, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Itakwenda KDI (Kigoma Development Initiative). I wish hon. Zitto long stay in the house.
   
 13. chipanga

  chipanga JF-Expert Member

  #13
  Jun 10, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 661
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60
  Uko kwenye right track mzee, kaza buti utaifikia tu target.
   
 14. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #14
  Jun 10, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Huwa wanamageuzi mnapenda kumpiga sana vijembe Zitto, lakini mkumbuke yeye ni kati ya vifaa muhimu kwenye upinzani binafsi nakukubali na kukuheshimu mapungufu ni sehemu ya ubinadamu, kaza buti Zitto umeonyesha mfano wengine waige
   
 15. L

  LAT JF-Expert Member

  #15
  Jun 10, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  jisaidie ili usaidiwe
   
 16. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #16
  Jun 10, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Poor minded!
   
 17. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #17
  Jun 10, 2011
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Sioni mantiki yoyote kwa hili. Posho ni haki yake. Jimbo kwake kuna matatizo kibao ya huduma za wananchi. Angeweza kutangaza kuwa anaelekeza posho hizo kwenye huduma za jamii jimboni kwake. Hivi kumgekuwa na ubaya gani kama angeeleza posho hizo hospitali ya jimbo lake? Asilewe sifa ingawa ana ubora.
   
 18. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #18
  Jun 10, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 886
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Huyu ni yule yule karani aliyeitisha press conference na kuanza kutoa character assessment ya maboss wake Wabunge, eti akina Lema ni vijana na wana jazba. Kwa maono yangu, huyu amelewa madaraka mpaka amepitiliza.

  Kuna usiri gani kujibu kuwa amepata au hajapata barua ya Zitto? watumishi kama hawa wametamalaki kwenye utumishi wa umma Tz na ndiyo maana nchi haiendelei hata miaka 50 baada ya kuzaliwa.
   
 19. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #19
  Jun 10, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mh. Zitto Kabwe Ameonyesha njia, wabunge wa chadema waige njia yake.
   
 20. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #20
  Jun 10, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ulitaka pesa zipelekwe WAMA?
   
Loading...