Kwanza nakupongeza sana kwa kuyatenda uliyoyasema.
Lakini hii haiondoi ukweli kuwa Wabunge wenzako wa CHADEMA wameshindwa kutembea kwenye maneno yao, wameendelea kuchukua posho walizosema kuwa "ni malipo haramu" na wakaenda mbali zaidi kuziita kuwa ni "wizi", siamini kama mtu makini anaweza kuendelea kuchukua malipo ya wizi.
Hii inaonyesha kuwa Wabunge wengine wa CHADEMA hawakuwa serious na hili, waliongea tu ili kupata point kisiasa, wangekuwa wapo serious wangeweza kusimama kwenye maneno yao, na kufanya ulivyofanya, na ata pale mikutano mitatu itakapoisha bila kusaini katarasi ya maudhurio, ingekuwa ni mtihani mkubwa zaidi kwa Bunge kuwachukulia hatua kwa Wabunge woote wa Chadema kuliko Mbunge Mmoja, na kama wangewachukulia hatua, hilo lingekuwa bonge ya turufu ya kisiasa kwa CHADEMA.
Tunachokipata hapa ni kuwa Wabunge wengine wa CHADEMA kama ilivyo kwa Shibuda wanazipenda hizi posho, lakini tofauti yao na Shibuda ni kuwa wao wanaongea wasiyoyaamini "kinafiki" kwa kisingizio cha "karatasi ya mahudhuri"wakati Shibuda yupo wazi.
Narudia tena....
WABUNGE WOOTE WA CHADEMA WANAOENDELEA KUCHUKUA POSHO NI WANAFIKI, ZITTO KAONYESHA NJIA, WALIO NA NIA YA DHATI YA KUANZISHA MCHAKATO WA KUZIFUTA POSHO HIZI WAIGE MFANO WAKE, wahenga walisema Matendo Hukidhi Haja MAridhawa Kuliko Maneno...