Jasusi;2423506]Hata ukiangalia ofisi ya bunge imefanya mchezo wa kisiasa kutoa taarifa hii. Ilitaka Chadema waonekane kuwa wanafiki wakati wabunge wengi wa CCM wanapinga kuondolewa kwa posho za wabunge. That should be the issue na wala si unafiki wa Chadema. Sasa suala limegeuka kuwa Chadema badala ya kujiuliza ni kwa nini CCM inashikilia wapewe posho na kwamba hizo posho hazitoshi, ziongezwe

Wakuu, Tatizo ninaloliona na mchezo wa siasa unaochezwa na serikali vizuri sana.
Tunakumbuka bunge liliwahi kutoa taarifa kuwa masilahi ya bunge ni siri yao. Inapotoka taarifa kuwa wabunge wote isipokuwa Zitto ni kutoa siri zile zile walizokataa kutueleza kwa kisingizio cha siri za wabunge. Sasa Kwanini taarifa hii imetoka leo?
Tunakumbuka wiki nzima imegubikwa na suala la Jairo hasa jinsi serikali ilivyomkingia kifua na kumdhalilisha Waziri mkuu. Joto ndani ya bunge limekuwa kubwa ingawa makosa yalifanywa na wabunge wenyewe kukasimu kazi zao kwa seriakali na kukataa matokeo.
Hata hivyo jamii imeonekana kuguswa sana na jambo hili na kumweka Rais na Katibu mkuu kiongozi katika wakati mgumu sana wakipingwa na kila kada, wanataaluma,viongozi wa jamii, wastaafu n.k.
Serikali ikachomeka suala la mh Zitto kuchukua rushwa CHC. Zitto akaweka wazi na masharti yaliyomweka Mkulo pagumu. Hoja ikafa.
Wiki hii hii serikali ikashauri suala la Arusha lijadiliwe, CCM kwa kupitia Nape na Mkama wakaligeuza kama tatizo la Chadema.
Sasa wamekuja na hili la posho.
Hii yote ni kutaka ku 'divert' attention ya public kutoka kwa aibu ya Jairo ili mjadala upotee kwa kuchomeka mijadala isiyo na uhusiano.
Tunavyozidi kulijadili kwao ni mafanikio. Let us stick to our guns. Ikulu, PS and Katibu mkuu wamendhalilisha PM. Rais na Katibu mkuu kiongozi wamebofoa! Waseme ukweli waache mambo ya CHC, Posho n.k hayo tunayajua, tunalotaka maelezo ni hili la 'best friend wao Jairo'