Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,998
Kwa: Katibu Mkuu

Chama cha Mapinduzi


Yah: Uamuzi wa Spika wa Bunge kuhusu suala la
Mheshimiwa, Malima (Mb) na Bwana Mengi Mwenyekiti wa
IPP


Suala lilitajwa hapa juu la husika

Mheshimiwa Katibu Mkuu, siku ya tarehe 8 Februari
2007, Mheshimiwa Samwel Sitta (Mb) Spika wa Bunge
aliwasilisha kwenye Bunge uamuzi wake kuhusu suala
hhili lililotajwa hapa juu. katika shauri hilo Spika
wa Bunge alifikia uamuzi kwamba nimeliongopea Bunge
kwa mujibu wa kanuni na 50 ya Kanuni za Bunge. Aidha
amefikia uamuzi kwamba kwa makusudi nililenga
“kamuathiri” Mengi kwa kumchhonganisha na viongozi wa
kitaifa. Mwisho, katika kukutafuta ufumbuzi wa suala
hili Spika wa Bunge, ameamua kutukutanisha mimi na
Bwana Mengi ili kutafuta “suluhu” baina yetu kwa
manufaa ya jamii.

Pamoja na kutambua wajibu wangu kama Mbunge kwa Bunge
lenyewe, Spika na Chama changu ninashindwa kuafikiana
na maamuzi haya na utekelezaji wake kw akuwa naona
hayalingani na ukweli wa matamshi yangu Bungeni ya
tarehe 2 Agosti 2006, uamuzi huo haukunitendea haki
kama Mbunge na ulilenga kwa dhahiri kumpendelea Bwana
Mengi, na katika kuufikia ninaamini kwamba haukupatiwa
taratibu za kuufikia ambazo zisingezingatia manufaa ya
Chama, kuliko ulivyo sasa hivi.

Aidha naomba niseme kwamba Spika alipeleka suala hili
mbele ya Kamati ya Bunge ya Kinga, Maadili na Madaraka
ya Bunge, ili apatiwe ushauri. Kwa kauli yake mwenyewe
amekiri kwamba kamati haikuniona na kosa lolote,
sikusema uongo na nilikuwa sahihi katika mchango
wangu.

Katika uamuzi wa Spika anasema :

“1.1.11 Kabla sijatoa maamuzi yangu, napenda
kuwashukuru kwa dhati Mheshimiwa Mwenyekiti Juma S.
Nh’unga na Waheshimiwa wajumbe wote wa Kamati ya Haki,
maadili na madaraka ya Bunge kwa umakini wao na kwa
kutumia utaratibu wa haki katika kuchunguza na
hatimaye kukamilisha kazi yao na kutoa ushauri wao
kwangu. Muda waliotumia na gharama zake visingwezea
kuepukwa.”

“6.0 TAARIFA NA USHAURI WA KAMATI YA KINGA, MAADILI NA
MADARAKA YA BUNGE

6.1 Baada ya Kamati ya Kinga, Maadili na Madaraka ya
Bunge kukamilisha uchunguzi wake, iliwasilisha taarifa
yake kwangu pamoja na taarifa ya maoni tofauti
(dissenting views) ya wajumbe wake wawili.

6.2 Katika taarifa hiyo, kamati ya kinga, maadili na
maadili na madaraka ya Bunge kamati iliridhika kuwa
Mhe. Adam K. A. Malima (Mb), hakusema uongo ndani ya
Bunge, na kwamba hakukuwa na uthibitisho wowote kuwa
ana maslahi binafsi na kile laichokisema Bungeni.

6.3 Kwa matokeo hayo, kamati ilishauri Bw. Reginald
Mengi aarifiwe kuhusu matokeo hayo ya uchunguzi wa
kamati, na pia Mengi ashauriwe kuwa makini katika
matumizi ya vyombo vya habari, hasa vile
anavyovimiliki.

6.4. Aidha, kamati ilishauri kuwa, Mhe. Malima ajibiwe
maombi yake ya Mwongozo wa Spika kuwa, alipokuwa
anachangia Bungeni tarehe 2 Agosti, 2006, alikuwa
sahihi kulingana na misingi ya Katiba, Sheria na
Kanuni za Bunge, na kwamba, akipenda afuate taratibu
zaidi za kisheria, kwa kuwa, kushambulia mchango wa
mbunge mmoja mmoja wakati anatekeleza majukumu yake ya
kikatiba si halali na mhusika wa kutenda kosa hilo
anaweza kushtakiwa mahakamani.”

Baadae katika Uamuzi huo huo anasema;

“7.2.7 Matokeo hayo ya uchunguzi wa kamati hiyo ya
Bunge yanaonesha wazi kuwa matamshi ya Mhe. Malima
hayakutimiza masharti niliyoyataja kwenye aya ya
5.4.2.1 hapo juu, yaani kwamba, yamevunja na kukiuka
masharti na matakwa ya Kanuni ya 50 (1) ya kanuni za
Bunge (Toleo la 2004) ambayo, pamoja na mambo mengine
inapiga marufuku Mbunge yeyote kusema uwongo Bungeni.

7.2.8 Kwa uelewe mzuri, kanuni hiyo inatamka kwamba:-
“Ni marufuku kabisa kusema uwongo Bungeni. Kwa sababu
hiyo, Mbunge yeyote anapokuwa akisema Bungeni,
atawajibika kuwa na hakika kwamba, maelezo anayoyatoa
ni sahihi, na siyo mambo ya kubuni au ya kubahatisha
tu;”…17

mheshimiwa Katibu Mkuu hapa utaona wazi kwamba pana
mgongano wa matamshi. Kwanza spika anasema kamati
imefanya kazi makini iliyozingatia taratibu, pili
anasema kamati ambayo inafanya maamuzi yake kwa mujibu
wa taratibu imeamua kwa wingi yaani consensus kwamba
sikufanya kosa lolote, tatu, kwenye 7.2.7 anasema tena
uchunguzi wa kamati hiyo hiyo, unaonyesha wazi kwamba
matamshi yangu yamekiuka kanuni na (50). Kwa maana hii
licha ya kazi ya makini ya gharama kubwa ya kamati ya
haki, maadili na madaraka Spika ameona maoni na
maamuzi ya kamati hayakao sahihi, isipokuwa kauli za
ushauri tofauti za Mheshimiwa Ole Sendeka ambaye
alikuwa kwenye kamati na alipata nafasi ya kuniuliza
maswali yake yote aliyekusudia, na Anne Kilango
Malecela ambaye amewasilisha pia ushauri tofauti wa
kamati hali ya kwamba yeye hakuhudhuria kabisa vikao
vya kamati hata siku moja kwa muda wa wote ambao mimi
na mashahidi wengine wote tulihudhuria na kuhojiwa na
kamati na hivyo nashindwa kuelewa Spika amepokea vipi
ushauri tofauti wa mjumbe ambaye hakuwepo kabisa.

Mheshimiwa Katibu Mkuu, hivyo basi kwa kuzingatia haya
niliyoeleza hapa juu naomba nisema yafuatayo;
(i) Sikubaliani na uamuzi huo wa Spika wa Bunge wa
kufikia maamuzi kwa tafsiri ya taathira
(interpretation by implication of statement) hali ya
kwamba matamshi yangu Bungeni yako wazi na hayahitaji
kupewa tafsiri ya taathira, na pia sikubaliani na
uamuzi huo ambao umefanywa kwa msingi wa vilelezo au
vigezo ambavyo sivyo vilivyotumika kwenye kamati na
wala havikuzingatia msingi wa hoja.
(ii) Spika ametumia Kanuni na 4(2) kufanya maamuzi
yake. Lakini kanuni ya Bunge 88 (1), (3), (5), (6),
(7), (9), na (11) zinaweka utaratibu wa uwazi wa
kupokea taarifa ya kamati ya kudumu na kuiwasilisha
kwa Bunge ili ijadiliwe na iridhiwe na Bunge. Spika
kwa sababu ambazo hakuoainisha hakuona umuhimu wa
kuruhusu mjadala wa Wabunge kwa suala lenye uzito wa
namna hii na badalå yake akaona busara yake pekee yake
itatosha kuamua masuala nyeti ya kinga na haki za
wabunge. Hivyo sielewi kwanini hakutumia utaratibu wa
utawala bora na demokrasia ya kibunge (good
governance and parlmentary democracy) unaotuamulia
masuala mengine yote ya kamati na ya Bunge kila siku.
(iii) Sheria ya haki, kinga na madaraka ya Bunge, 1988
haisemi kwamba sisi kama Wabunge ni bora kuliko
wananchi, na tuko juu ya sheria. Bunge lenyewe ndilo
lililotunga sheria hiyo na sisi Wabunge ndiyo
tunawajibika mwanzo kuiheshimu. Ama kwa upande wangu
sikusema hivyo wala sikusema jambo lolote ambalo kwa
taathira linaweza likatafsiriwa hivyo, na hivyo sielei
kwanini Spika ametumia mifano ya kuonyesha kwamba
matamshi yangu yamevukia mipaka ya kinga “kama
kumsingizia Padri ujambazi” wakati wa kulinganisha
suala hili.
(iv) Suluhu ni muafaka unaotafutwa kwa kuridhia pande
mbili baada ya kubainika tofauti zao na chanzo cha
tofauti hizo, na ambayo (suluhu hiyo) inalenga
kuepusha hatari ya pande hizo mbili kuendelea kugombea
na kuleta athari kwa wengine wasiokuwa wao au hata
pamoja na wao. Mimi sina ugomvi na Mengi na nimelisema
hilo na nimelirudia kwenye kamati mara kadhaa.
Nilikuwana tatizo na makadiro ya wizara na kama ni
ugomvi basi itakuwa baina yangu na Waziri, Mhesh.
Muhammad Seif Khatib kwa kuwa nilikuwa nimekusudia
kuzuia mshahara wake. Baada ya kupata maelezo na
kutosheka kama ulikuwa ugomvi basi huo ulishamalizika
bila ya kuhitaji kupatanisha. Ugomvi wa Mengi labda ni
wake kwangu mimi.
(v) Ni imani yangu kwamba kama kwa mujibu wa Spika
suala hili lilikuwa linashamirisha “makundi
yaliyochomoza ambayo yameonekana kuibua masuala ya
udini, rangi na tofauti za kipato katika jamii,” na
kwa kuwa mimi sikuona ushahidi wowote wa kuunga mkono
suala hili la makundi ndani ya kamati, ndani ya Bunge
na kwa kuwa mimi ni Mbunge wa jimbo wa Chama ambacho
hakikubaliani na matabaka ya aina yoyote yale, na
mwanajamii ndani ya jamii ya watanzania, siridhiki na
maelezo hayo yaliotumika kama kigezo cha kutafuta
suluhu.
(vi) Kwa kiasi kikubwa haya yote yanahusu Wabunge wa
CCM kwani ndio tulio wengi ndani ya Bunge (asilimia
85), na kamati ya Maadili ina wabunge 13 wa Chama
chetu kati ya jumla ya wabunge 15. Kwamba Wabunge
wawili na Spika mwenyewe hawakuona sababu ya kuleta
jambo hili linalotuanika hadharani, kwenye utaratibu
mzuri ambao ndio unajenga mshikamano na umoja miongoni
mwetu, ni j ambo la kushangaza na ambalo linanipa
mashaka makubwa. Kwa kuwa sijaona taarifa ya kamati
kwa Spika, ya ushauri tofauti (dissenting views) za
Waheshimiwa Ole Sendeka na Anne Malecela, siko tiyari
kuukubali uamuzi wa Spika ambao kama alivyosema msingi
wake ni ‘dissenting views’ hizo.

Mheshimiwa nawasilisha uamuzi wangu wa kuukataa uamuzi
Spika wa kuhudhuria kikao cha usuluhisho na Mengi.
Badala yake, na kwa kuwa suala hili sas linahusu
viongozi wawili, mmoja mjumbe wa kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama, na mwingine Mbunge
wa CCM nawasilisha suala hili kwako ili lipatiwe
ufumbuzi ndani ya taratibu za uongozi wa Chama cha
Mapinduzi, ambao ninaamini uongozi una busara pana ya
viongozi wenye ujuzi na uzoefu wa kufanya maamuzi
yenye kuzingatia maslahi ya Chama chenyewe na Taifa
kwa ujumla.

Mheshimiwa Katibu Mkuu, ninaambatanisha taarifa yangu
yenye vielelezo ya matokeo ya ndani ya Kamati ambayo
ndiyo Waheshimiwa Ole Sendeka na Anne Malecela
walitumia wakati wanawasilisha maoni yao kwa Spika.
Ninaamini yataonyesha bila ya kuhitaji tafsiri za
taathira kwamb mijadala ndani ya kamati ilikuwa ya
uwazi na ambayo ilizingatia taratibu zote, na hivyo
kulikuwa hakuna haja ya Spika kupuuzia ushauri
aliyepewa na wengi na kuchukua maamuzi ya wachaçhe
ambayo yanaonekana yametawaliwa na misingi ya ubinafsi
kinyume na maadili, heshima na nidhamu ya wabunge wa
Chama cha Mapinduzi.

Kanuni za Kamati ya Wabunge wa CCM;
9(a). Kila mjumbe binafsi wa kamati ya Chama anapaswa
wakati wote ule ambapo anakuwa Mbunge, ahakikishe
kwamba tabia yake na mwenendo wa maisha yake kwa
ujumla haukiletei aibu na fedheha au kukipaka Chama
matope.

Mheshimiwa Katibu Mkuu, nawasilisha nasubiri muongozo
wa Chama.

Naomba kuwasilisha,
Kidumu Chama cha Mapinduzi


Nakala kwa
Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi

Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa, Mb
Mweyekiti wa Kamati ya Wabunge wa CCM Waziri Mkuu
Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni

Mheshimiwa Ali Ameir Mahommed, Mb
Katibu
Kamati ya Wabunge wa CCM.

Mwisho.
 
Bunge letu lina upuuzi mwingi kiasi kuwa naona ugumu wa kumwelewa Mheshimiwa Malima. Ugonvi wake na Mengi ndio uliosababisha kuundwa kwa kamati ambayo baadaye ilisemekana imepewa rushwa ili kuzima kesi hiyo. Kuanzia hapo ukweli wa jambo lenyewe umekuwa mgumu kueleweka; kwa hiyo makala ya Mheshimiwa Malima hapo juu siichukulii kwa uzito wowote ule.
 
Kid!
The fact is wewe mtoto ulisema uongo PERIOD. hayo mambo ya mwamvuli sijui taratibu za kibunge na chama chako ni huko huko. Wananchi mchele tumekwishauona na pumba tumeziona.

UKILAZA wako usitake kutupotezea KODI za sisi wananchi na MUDA wetu.

Wananchi wa mkuranga they deserve more than issue yako na Mengi. behave yourself boy, kwani hizo "busara pana" unazotafuta ukijumlisha na UONGO wako = PUMBA mbele ya sisi wananchi!

Onyo:
Hakuna busara pana wala fupi!!, usituharibie lugha yetu maridhawa, BUSARA NI BUSARA period it is either mtu ANAYO au HANA.

Kwa wanaotaka kuficha maovu ndio husema "busara pana"
 
tetesi ni kuwa baadhi ya viongozi wa CCM wanakumbuka Malima alitoka NRA chama ambacho "inadaiwa" marehemu baba yake alisaidia kukiunda. Pia inadaiwa Bw. Malima alibebebwa na CCM licha ya kupata kura chache za maoni wakati wa mchakato wa kutafuta wagombea. Je, akibanwa yuko tayari kuchomoka CCM? au lile jinamizi mashuhuri la "nidhamu ya chama" litamuuma na yeye?
 
"busara pana" ndio iliyompitisha, sasa anataka kutumia huo huo upuuzi wa "busara pana" ili kuhalalisha UONGO wake!!, akichomoka tu kaisha!, hana jeuri hiyo
 
Mwanakijji,

Adam Malima, ni mfanyakazi wa Manji licha ya ubunge wake hiyo ni fact, ina maana asipokuwepo bungeni ni mkurugezni katika ofisi za Manji, hakuna la ajabu,

Mzee Ogah,

Maneno mazito hayo bro, keep it up!
 
"busara pana" ndio iliyompitisha, sasa anataka kutumia huo huo upuuzi wa "busara pana" ili kuhalalisha UONGO wake!!, akichomoka tu kaisha!, hana jeuri hiyo


Ogah

Nakubaliana na wewe kabisa...Huyu mkosa busara Malima hana jeuri hiyo kabisa...atabaki hapohapo CCM akichezea hela za walipa kodi kwa hili suluhisho la kishenzi dhidi yake na Mengi. Wakakti huo huo anakula tena kiulaini kutoka kwa Manji...wananchi wa Mkuranga huyu ndiye mbunge mliyemchagua awawakilishe bungeni...aibu tupu.
 
Ogah

Nakubaliana na wewe kabisa...Huyu mkosa busara Malima hana jeuri hiyo kabisa...atabaki hapohapo CCM akichezea hela za walipa kodi kwa hili suluhisho la kishenzi dhidi yake na Mengi. Wakakti huo huo anakula tena kiulaini kutoka kwa Manji...wananchi wa Mkuranga huyu ndiye mbunge mliyemchagua awawakilishe bungeni...aibu tupu.
Hivi mengi,manji na adam...............SASA INATOSHA Kama wanalazaidi wafikishane mahakamni bungeni si sehemu ya kujadili watu wachache kwa manufaa yao na kuchezea fedha ya walipa kodi.Kama kuna mtu anamadai zaidi sehemu ya madai kama hayo ni kwenye mhimili mwengine napo ni Mahakamani.
 
Yebo Yebo!
Hivi sisi wananchi unafikiri wakati mwingi huwachagua viongozi bali mara nyingi huwa tunachaguliwa viongozi watuongoze na matokeo yake ndiyo haya huwa hawajali maslahi yetu wanajali maslahi ya wale waliowapitisha ili watuongoze.
 
tetesi ni kuwa baadhi ya viongozi wa CCM wanakumbuka Malima alitoka NRA chama ambacho "inadaiwa" marehemu baba yake alisaidia kukiunda. Pia inadaiwa Bw. Malima alibebebwa na CCM licha ya kupata kura chache za maoni wakati wa mchakato wa kutafuta wagombea. Je, akibanwa yuko tayari kuchomoka CCM? au lile jinamizi mashuhuri la "nidhamu ya chama" litamuuma na yeye?
Hawezi kufurukuta huyu walimuweza baba yake na analielewa hilo kuliko mtu mwengine yeyote ataendelea kucheza ngoma iliyozoeleka na wengi.....................!
 
Huyu Malima jeuri yake anaitoa kwa EL.Inasemekana kuwa EL na Spika sasa hivi ni maadui wa waziwazi.Pia inasemekana kuwa JM kajiunga na Spika kuwa na kambi against EL.Lakini pia wabunge wengi wa CCM hawana imani tena na Spika na hii inatokana na kampeni za kichinichini zinazopigwa na EL na watu wake against Spika.
 
Jambo limezaaa jambo na Mungu hamfichi mnafiki . Muda wote nimekuwa najiulizaa if Mzee Es was real for Spika Sitta and why ? Kabla jogoo hatawika Zanaki kasema John Malecela yuko na Spika na sasa nime elewa makelel ya Es ya kumpamba spika . Asante sana .

Nimjavyo mimi huyu jamaa akitetea kitu si bure lazima awe na maslahi binafsi na leo majibu wana JF mmeyapata .
 
Ogah
Nasikitika mawazo yako yanalenga kwenye chuki zaidi za kebehi bila kutafakari yaliyosemwa na Malima. Maneno kama 'ukilaza' nk yanathibitisha ulivyo na chuki na mbunge huyu kijana. Nilitegemea kama ungekwenda kwenye details za yaliyozungumzwa kwenye barua ya Malima badala ya kuonyesha dhahiri chuki yako. Anyway naamini kama kesi inafika patamu na tutaona nani mkweli baina ya Malima, Mengi na Sitta.
Mwanakijiji
Umekuwa ukijipachika jia la mzee ila mchango wako katika hili nauona pia uko kiushabiki. Kwa mfano sioni sababu ya kuanza kuleta historia ya Malima baba mtu na NRA na mkwara kama eti akifukuzwa atakwenda wapi. Mwanachama hufukuzwa kwa hoja na si kwa kuwa alitokea upinzani. Tafadhali behave vizuri.
Mwisho nampongeza Mh Malima kwa ujasiri wa kuweza kumuandikia Spika jibarua lile. Hawa ndo vijana wanaotakiwa enzi zile za ndiyo mzee zimekwisha.
Kingwele now in Tz.
 
Murangira rafiki yangu,

Won't you spare this guy?, akichangia tuu ni JM unamtaja, why? we use our nicknames, no exposure is needed. Why cant you just remain silent if you have nothing to add to this thread??

Naomba rafiki yangu tena wa kule kule kwetu, umuache huyu jamaa, tunamuhitaji kama tunavyokuhitaji wewe hapa JF.

FD
 
Kingwele, miye nimetoa mawazo ya watu wengine kuhusu hili.... vyanzo ambavyo vimenipatia barua hiyo ndio ambavyo vimeleta hoja hiyo ya kuunganisha historia ya Malima na NRA. Ila hili la kuwa Malima alikuwa/au bado ni mfanyakazi wa Manji sikulijua. Kama ni kweli, basi it makes a lot of sense! He has nothing to lose na mgogoro wake na Mengi then unaonekana kwa kutumia mwanga mkubwa zaidi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom