Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,178
2,000
yeah.. isipokuwa pale mtu anapomzushia mtu mwingine mambo na hayuko tayari kuomba radhi au kuadmitt amekosea...
 

DAR si LAMU

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
2,933
1,500
ina maana hii issue ni tone la mvua kwenye ndoo...na mvua yenyewe ndio inakujanyesha au inaanza!?

kama ni hivi itakuwa balaa!
 

DAR si LAMU

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
2,933
1,500
Kweli sasa Spika amekuwa laughing stock....

nadhani hatuyajui mengi yanayoendelea behind the scene! uamuzi alioutoa umejaa maswali mengi[achana na kutowaridhisha watu]ambayo ni mazito,mazito kama ki[y]ama.

si mbali mbingu zitaanza kufunguka na mafunuo kuonekana!
 

Mkira

JF-Expert Member
May 10, 2006
425
195
Dunia kuna mambo?

Humu katika hii Forum siku hizi ni ushabiki tu!!!

Wamefanikiwa kwa hilo.

Hivi ni kweli mzee mzima kama yule spika tena mbele ya wabunge na vyombo vya habari bila aibu ALISEMA UONGO ETI KUWA KATIKA MAISHA YAKE YOTE HAJAWAHI KUSIKITISHWA KAMA ALIVYOFANYIWA NA MALIMA?

JE NI KWELI?

HATA HAJAWAHI KUFIWA NA NDUGU ZAKE WA KARIBU?


HUO NI UONGO BUNGENI
 

Zanaki

JF-Expert Member
Sep 1, 2006
545
195
labda yeye anaongelea kusikitishwa na wewe unaongelea kushikwa na majonzi.Unaweza kusikitika kuwa timu yako imefungwa labda anaongelea kusikitika huko
 

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,808
1,250
Sikumbuki ni gazeti gani, kati ya MTANZANIA na Mwananchi, waliandika Dau alikwenda, badala ya kusema kuhusu Malima aliyoyasema Bungeni, alianza kujitetea kuhusu ununuzi wa maghala kwa Quality Group, na kusema kwamba walioandika THISDAY na KULIKONI walimuonea, kwani utaratibu ulifuatwa. Akaulizwa, Malima alikuita kuwa shahidi wake, ama kuja kujisafisha? akasema yy anajaribu kuonyesha mfano wa jinsi Mengi anavyotumia vyombo vyake vibaya, akaulizwa sasa kesi ni MALIMA KUSEMA ITV INATUMIA DAKIKA MBILI KWA RAIS NA WAZIRI MKUU WAKATI MENGI ANATUMIA DAKIKA KUMI, kuna uhusiano gani na NSSF KUNUNUA MAGHALA? hayo ndio maelezo ya DAU sawa na alivyokwenda Mke wa Mahalu aliyesema mume wake kaonewa na THISDAY Kwa kumsingizia kuwa ameiba pesa wakati serikali imemrudisha tu nyumbani aje kupangiwa kazi nyingine. (ILIKUA KABLA YA KUFIKISHWA MAHAKAMANI)
 

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,281
1,195
Ukweli katika kesi hii Spika ametumia ubabe sana katika maamuzi yake.

Ripoti ya kamati kakataa kuiweka hadharani anadai ni ripoti ya Spika! wakati huo huo anachomoa yale anayaona yanamfaa na kutuambia mfano wa hili ni hao mashahidi.

Anapotuambia mashihidi walioletwa na Mh Malima hawahusiani na kesi anatuburuza tukubaliane na yeye kibubusa, kwani hatujui hadidu za rejea za kamati ( Terms of reference ) kwa kuwa ripoti hatuna.

Tukumbuke mgogoro huu umeanza pale Mh Malima alipokuwa akichangia hotuba ya wizara ya Utamaduni miongoni mwa aliyoyasema ni haya:


Quote: from Hansard[/B]

Mheshimiwa Spika, naomba niseme yafuatayo kuhusu Sekta ya Habari:-
Mheshimiwa Spika, Tanzania imepiga hatua kubwa sana katika maendeleo ya
Sekta hii katika sehemu zote TV, Radio, Magazeti katika kipindi kifupi sana. Pia,
naamini kuwa Vyombo vya Habari vinafanya kazi katika mazingira mazuri
yanayowaruhusu kutekeleza majukumu yao kwa uhuru bila kubughudhiwa na Mamlaka. Lakini pia lazima tukubali kwamba uhuru wa kutoa habari una mipaka. Una viwango! Huwezi kwa sababu ya kumiliki Vyombo vya Habari ukatumia nafasi hiyo kwa ajili ya kudhalilisha Watanzania wenzako kwa kusema maneno ya uongo, au kwa kutoa habari zinazopotosha kwa makusudi. Utoaji wa habari ni huduma ya jamii. Naomba maelekezo ya kina, Muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habariuliotajwa na Mheshimiwa Waziri Ibara ya 19 ya hotuba yake itakuwa tayari, itakamilika lini? END

Kwa msingi huo basi ikiwa hao Mahalu na Dua wameenda kuthibitisha hilo (if terms of references says so) then hilo halina tatizo hapo ni mahala pake hasa na ndio maana hata Judge Warioba nae alikuwa ni shahidi wa Malima ktk kesi hii sidhani na yeye angekubali kuchukuliwa "msukule" kwenda kutoa ushuhuda wa jambo lisilo endana na kesi.

Ndio maana gazeti la Mwananchi la juzi limemkariri Mbunge mmoja akisema ripoti ya kamati ina mambo mengi na Spika anakwepa kuiweka hadharani.

Ili kuondokana na minonong'ono hii aweke vitu hadharani including na Hansard za vikao vya kamati ili sisi tulioliwa Mil 100 tujue pumba na mchele.

Mgogoro umetumia Mil 100 halafu anatujia na mitishamba ya busara, ushauri nasaha, sijui kumpuuza ni adhabu, kanisononesha yote ni kutaka public sympathy.

Kama ni ushauri nasaha au busara angezitumia ktk kesi ya Mh Zitto ambaye is only 30 years old kuliko huyo Malima ambaye ni over 40 years. Hakumsamehe Mh Zitto mpaka alipoenda kumwangukia ofisini kwake. Huyu Malima kwa makusudi kabisa kampuuza na kumwacha mzee anahangaika kupiga simu kutwa nzima. Huyu sio wa kupuuzwa huyu ni wa kuadhibiwa sawasawa.

Busara zilikuwa wapi wakati anamtoa Mh Amina Chifupa Bungeni kwa sababu tu hakuvaa Gloves! Busara zilikuwa wapi alipowatoa wabunge waislam na vibaraghashia vyao. Kwanini asitoe "ushauri nasaha" hapo ili Waheshimiwa hao wasifanye makosa hayo tena. Tena ushauri nasaha huu ungekuwa hauna gharama kuliko huu wa Malima
 

Mugongo Mugongo

JF-Expert Member
Nov 8, 2006
223
0
Zitto mkubwa mbona umeingia mtini baada ya uamuzi wa Spika? Halafu mshikaji wako Spika anadai unamprintia debates hapa JF. Nakupongeza kwa hilo manake unafanya hapa papate wasomaji wa calibre ya juu. Keep it up!
 

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,555
0
Sikumbuki ni gazeti gani, kati ya MTANZANIA na Mwananchi, waliandika Dau alikwenda, badala ya kusema kuhusu Malima aliyoyasema Bungeni, alianza kujitetea kuhusu ununuzi wa maghala kwa Quality Group, na kusema kwamba walioandika THISDAY na KULIKONI walimuonea, kwani utaratibu ulifuatwa. Akaulizwa, Malima alikuita kuwa shahidi wake, ama kuja kujisafisha? akasema yy anajaribu kuonyesha mfano wa jinsi Mengi anavyotumia vyombo vyake vibaya, akaulizwa sasa kesi ni MALIMA KUSEMA ITV INATUMIA DAKIKA MBILI KWA RAIS NA WAZIRI MKUU WAKATI MENGI ANATUMIA DAKIKA KUMI, kuna uhusiano gani na NSSF KUNUNUA MAGHALA? hayo ndio maelezo ya DAU sawa na alivyokwenda Mke wa Mahalu aliyesema mume wake kaonewa na THISDAY Kwa kumsingizia kuwa ameiba pesa wakati serikali imemrudisha tu nyumbani aje kupangiwa kazi nyingine. (ILIKUA KABLA YA KUFIKISHWA MAHAKAMANI)

kwa nini tuandikie mate wakati wino upo?

nadhani kuwa zipo Hansards za Bunge zipo online na nirahisi kujua Dr Dau alisema nini kwenye kile kikao
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom