Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Status
Not open for further replies.

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,281
1,195
Mimi nadhani ili kuilinda credibility ya forum hii naomba tupunguze ushabiki ktk mijadala kama kweli tunajadiliana kwa maslahi ya nchi.

Barua iliyopo mbele yetu inahusu malamiko kwa katibu mkuu wa ccm ya kutokubaliana kwa Mh Malima na uamuzi wa spika kuhusu kesi yake na Mengi.

Mtu ahitaji kuwa rocket scientist kuona kuwa ktk uamuzi ule Mh spika amejichanganya sana kama ilivyowekwa abundantly clear na Mh Malima mwenyewe.

Spika kuamua kuchukua uamuzi based on the (dissenting views) was a disaster but to make the matter even worse it has come to our knowledge that even those co called dissenting viewers one of them she was not even attending the proceedings!. Nakubali kuwa kuna Hansard na mtu anaweza akapata kumbukumbu za vikao but katika hili Bi Mkubwa Mama Malecela could do better kwa kuhudhuria vikao na ku air her views. Ikumbukwe hapa kamati ilikuwa inafanya kazi yake kimtindo wa mahakama kwa kuwaita mashahidi na kufanya cross examination na mashahidi hao. Nadhani Bi Mkubwa angekuwa good contributor kwenye hili badala kujifungua ndani na mzee Malecela na kuandika ripoti yenye kutilia shaka.

Kibaya zaidi ni kuwa, kama Mh Malima alivyodai ktk barua yake ilitakiwa ile ripoti ijadiliwe na bunge zima kwa sababu ile ni kamati ya Bunge na sio kamati ya Spika. Badala yake Spika nae akajifungia ndani na Mama Margaret Sitta ( kama alivyofanya mzee Malecela na Mama Anne ) akaandika ripoti nyingine badala ya ile ya kamati na akaenda "kuwasomea" wabunge kwani hawakupewa nafasi ya kuijadili hiyo "makeshift" ripoti. Uendeshaje wa bunge kibabe namna hii ndio unaopelekea wengi kupoteza imani na mzee huyo alieingia kwa mbwembwe na kujibodoa kuwa atafanya kazi kwa "speed na standards"

Lakini hata kama Mh Malima kama dissenting views zinavyo suggest atakuwa amekosa Spika alitakiwa amuadhibu kulingana na kanuni za Bunge haya mambo ya kutumia "busara zangu" zinanituma niwaite na niwasuluhishe zinatutia shaka sana sisi waumini wa demokrasia, na haya mambo ya kuitana chemba ndio mianya ya rushwa yenyewe hiyo tunayoipigia kelele kila uchao. Fedha za Umma Milioni 100 zimetumika leo unatuambia "busara zangu" zinanituma niwaite niwasuluhishe!

Naamini matumizi ya lugha chafu hayaruhusiwi humo, na kitendo cha kumwita Mh Kilaza nadhani ilikuwa abit below the belt, hata hivyo ktk hiki kama kuna kilaza basi ni huyu Mh Spika. Akiwa ni graduate wa Law he should be do better than that and indeed my faith on him is wearing thinner and thinner.

Mzee ES umekuwa ukisisitiza time and again kuwa Mh Malima ni mfanyakazi wa Manji. Tumetaka ushahidi hatujapata but umekuwa ukirudia tena na tena na sasa Mzee Mwanakijiji nae amejiunga ktk hilo au ndio ule msemo " create a lie, repeat it several times and then people will accept it to be the truth".

Nimejaribu kuangalia ktk CV ya Malima kama ilivyo ktk web ya Bunge sikuona hilo labda nirudie tena kukuomba Mzee ES kwa kuwa wewe una source nyingi na personally unawajua waheshimiwa wengi tusaidie ktk hilo na utupe ushahidi wa Mh kuajiriwa na Manji. Nilichofanikiwa kukiona mimi baina 2002 - 2005 alikuwa anafanya private consultancy, swali je miongoni mwa wateja wake alikuwa ni Bw Manji? and if so, does it amount to call someone kuwa ameajiriwa nae?

Kama nilivyotangulia kusema awali, mijadala hii kama inalenga kujenga nchi basi tuweke jazba na chuki pembeni. Suala hili lishakuwa balaa kwa taifa hili maana baada zile milioni 100 tulidhani yamekwisha kumbe badala ya kushuhudia the beginning of the end, kumbe we have merely see the end of the beginning!.

Mungu ibariki Tanzania
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,178
2,000
watu ni wagumu kuelewa na naona najumuishwa tena bila watu kuangalia nilichoandika. Mimi nimeshangaa kuona Malima anaitwa mfanyakazi wa Manji. Soma jibu langu maana hata sija edit nisije kuambiwa nimebadilisha nimetumia a qualifier "kama ni kweli" maana yake sina uhakika kama ni kweli!!!
 

Kitila Mkumbo

Verified Member
Feb 25, 2006
3,350
2,000
Masatu: great, that is it. Lakini kuna watu humu wanatumia forum to vent their long held frustrations and anger!
 

Kalamu

JF-Expert Member
Nov 26, 2006
873
0
Masatu, kuna wengine humu watahitaji utoe ushahidi kuhusu Mama... nani? alivyojifungia ndani na Mzee... yupi yule? wakati wanaandika 'a dissenting view' kuhusu ripoti. Ushahidi mwingine unaodaiwa ni ule wa mzee spika kujifungia ndani na waziri Sita, nao wakiandika hekima za busara.

Ni dhahiri sasa kuwa katika bunge letu; na ninahisi kwa kiasi kikubwa kuwa katika CCM yenyewe mambo sio shwari tena. Kutahitajika pawe na ufundi mkubwa katika kurekebisha hali ili iwe shwari tena. Hapa ndipo mwenyekiti atahitajiwa kutumia busara zake zote alizojifunza tangia hizo enzi za 'uTANU youth league' Kutuliza kwa muda kwa njia za kawaida za ku-appease hazitasaidia kitu.
 

Tabasamu

Senior Member
Nov 27, 2006
136
0
Masatu,
Credibility iharibike kwa sababu watu wamejadili waraka wa Malima kwenda kwa Makamba? Bila kumng'unya maneno hili suala wengine wetu tulikwisha sema tangu huko mwanzo ni suala la kipuuzi kabisa na kwa sababu hiyo aliyelianzisha (Malima) alikuwa ni mpuuzi kwenda bungeni na kuanza kuhoji kitu kama hicho tena akijua ni uongo.
Kulia lia anakokufanya sasa kunazidi kumwonyesha alivyo mbunge wa ovyo ovyo
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,876
2,000
Hivi niwekeni sawa .Habari hii ni Bungeni na Makamba ni Katibu Mkuu wa CCM what is the connection na mambo ya Bunge ?
 

Kyaruzi

Member
Mar 23, 2007
83
0
Well said Masatu. The whole thing is mess from ccm, bunge lao, spika wao wapinzani in short ni kichefuchefu tu.

By the way Masatu nimependa usemi wako ur "faith on him is wearing thinner and thinner" Ninyi watu KLF mna taabu sana (joke)
 

Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
1,213
1,250
The so called Mengi and Manji sagas should be trashed somewherelse Not in our Parliament anymore! we 're extremely tired with the scenario because it worth nothing to taxpayers and it cost too much to the fellow citizens!
 

Nungwi

Senior Member
Sep 9, 2006
196
0
Malima si Kiliza ana shule ya nguvu na si ya kubabaisha alitakiwa awe waziri kamili. wazee tuache chuki.
 

Nungwi

Senior Member
Sep 9, 2006
196
0
Masatu.
umetulia sana kichwa kama Professor Warioba wa Mzumbe university bila shaka wewe ni product ya kiona mbali(professor Warioba), kwa jina tu inaonesha umetoka mkoa wa Professor Warioba.
keep it up.
 

Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
1,213
1,250
Malima si Kiliza ana shule ya nguvu na si ya kubabaisha alitakiwa awe waziri kamili. wazee tuache chuki.
Angekuwa na shule hii kesi yake ya madai angeipeleka mahakamani na si Bungeni kupoteza muda wa wananchi na fedha za walipa kodi kwa ajili ya ugomvi wa matajiri wawili.....................Hii ni shule ya wapi? Kuna matatizo mangapi yanawakabili wananchi wa mkuranga tu pekee yake mbona hajayapelekea hoja au swali bungeni anakaa kumjadili mengi na vyombo vyake vya habari Hii inamsaidia nini mwanamkuranga au Mtanzania kwa ujumla,Hizo Million zilizopotea kwa kuleta utata kwake bungeni zingepelekwa pale Muhimbi wangapi wangepata vitanda aua vyandarua,Elimu yake ukomo wake ni wapi? He has to stop Now!.............................. Tumechoshwa..............wanataka malumbano wapeleke kortini au sehemu nyingine na mwenye haki atapata huko na siyo Bungeni ,Bungeni wapeleke mijadala inayohusu watanzania walio wengi na kwa faida ya wanaowawakilisha!Tena Afadhali wangekuwa wanatoka jimboni mwake tungesema wapiga kura wake wamemtuma!
 

Mwanagenzi

JF-Expert Member
Sep 11, 2006
690
1,250
KNKCU,
Ukisema hivyo, huoni hata huko mahakamani kuna mlundikano wa kesi mpaka mahabusu wanagoma? Kwa nini tusipunguze kesi zisizo na kichwa wala miguu ili kesi nyingine kama vile za "mauaji bila kukusudia" nk, zikashughulikiwa haraka??
 

Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
1,213
1,250
KNKCU,
Ukisema hivyo, huoni hata huko mahakamani kuna mlundikano wa kesi mpaka mahabusu wanagoma? Kwa nini tusipunguze kesi zisizo na kichwa wala miguu ili kesi nyingine kama vile za "mauaji bila kukusudia" nk, zikashughulikiwa haraka??
Hii ni kesi ya madai ya kawaida...............................Kesi kama hii kurundikana huko mahakamani ni bora kuliko kugharimu muda na Mamilioni ya fedha kuwajadili matajiri wawili kwa gharama ya watanzania,Je hiyo fedha ingetumika kulipia masaa ya ziada ya majaji na mahakimu wakaongeza muda wa usikizaji kesi si afadhali ingekuwa bora....................Kuliko kulipa kamati ya kuwajadili matajiri wawili!
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,876
2,000
nungwi unasema Malima kasoma sana na alipashwa kuwa waziri kamili ? uwaziri kumbe ni kusoma sana na si post ya kisiasa ? Kwa nini sasa asipewe na yeye kasoma? Shule ipi hiyo ya kujkenga majungu ? Hebu weka CV ya huyu mpuuzi hapa tuone shule inavvyompa shida hata kujisaidia mwenyewe .Kama kusoma ni huo basi watoto wangu nawaondoa shule .
 

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,172
2,000
duh usifanye hivyo Murangira, huyu bwana kasoma ila tuseme elimu haijamkomboa au tuseme "he learns but doesnt think"
maana kusoma pekee bila ya kudigest ulichokisoma ni sufuri
 

Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
1,213
1,250
Hapa Hakuna cha kusoma wala nini analolifanya halifanyi kwasababu amesoma au hakusoma, bali anafanya kwasababu ana msukumo wa kufanya hivyo...............!
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom