Full Blood Picture
JF-Expert Member
- Jan 7, 2021
- 3,890
- 7,889
Wanabodi
N.B:Wakati bandiko hili linaandikwa kumbe tayari CJ。Prof. Ibrahim Juma ameisha staafu rasmi na Jaji Mkuu mpya ameisha teuliwa, hivyo hoja ya CJ Prof. Ibrahim Juma is by passed by events!
1. Utangulizi
Binadamu hatufanani, kuna watu ni wenye bahati, very fortunate, wengine wako kama Midas touch!, everything they touch turns to gold. Mimi ni mmoja wa watu hao very fortunate!. Kati ya Wakuu 3 wa Mihimili yetu 3, ya Serikali Bunge na Mahakama, Wakuu wa Mihimili 2 ni Waalimu wangu!.
2. Mkuu wa Mhimili wa Mahakama, Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, ndiye alikuwa Dean wangu, wakati nikiwa mwanafunzi wa Sheria pale FoL ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, wakati huo akiwa kijana akiwa Dr. Ibrahim Juma.
3. Mkuu wa Mhimili wa Bunge, Spika wa Bunge, Dr. Tulia Akson, ndiye mwalimu wangu wa Kipindi changu cha kwanza, somo la kwanza, siku ya kwanza ya masomo, wakati huo akiwa TA, binti mdogo, sasa ndie Mkuu wa Mhimili wa Bunge Spika wa Bunge
4. Kitendo cha kufundishwa na waalimu wawili,waliokuja kuwa wakuu wa mihimili,sio jambo dogo,wakati wengine wanaogopa kumkabili Jaji Mkuu, CJ,kutokana na uhimili wake,mimi kama mwanafunzi wake,ninaweza kumwambia lolote kwasababu kwangu huyu sio Jaji Mkuu tuu,kwangu mimi, huyu ni yule yule mwalimu wangu na Dean wangu,Dr Ibrahim Juma, pale FoL.
5. The same applies to Dr. Tulia,japo anaheshimika na kuogopwa kwa uhimili wake,kwangu huyu ni yule yule TA aliyenifundisha,hivyo nakuwa niko free kumwambia lolote kama hivi
View: https://youtu.be/ZM_D9HAPi5M?si=yTiMm7f27zM4NhZQ
6. Kitu cha kwanza muhimu kabisa katika taifa lolote ni watu, wananchi ndio wenye nchi na kila kitu kilichomo, wananchi wameweka katiba yao ya jinsi ya kuendesha mambo yao,hivyo ukiondoa watu,wananchi,kitu muhimu cha pili ni katiba,ndio kila kitu!。
7. Hawa wananchi wenye nchi wameipa katiba ukuu wa kila kitu,hakuna aliye juu ya katiba. Katiba ndio sheria mama, sheria nyingine yoyote inayokinzana na katiba,inakuwa ni sheria batili!。
8. Katiba ya JMT,imetoa haki mbalimbali za kikatiba,na kisheria za kisiasa,kiuchumi na kijamii.
9. Haki kuu mbili za kisiasa ni haki ya kuchagua na haki ya kuchaguliwa。
10. Haki ya kuchagua inatekelezwa kwa haki ya kupiga kura kwa uhuru wa kuchagua viongozi unaowaoenda kwa mujibu wa ibara ya 5。
11. Haki ya kuchaguliwa inatekelezwa haki ya uhuru wa kugombea nafasi yoyote ya uongozi toka serikali ya mtaa hadi serikali kuu kwa mujibu wa Ibara ya 21 ya katiba.
12. Rais wa JMT, na mihimili yote mitatu ya Serikali,Bunge na Mahakama, ni zao la katiba, na wote wako chini ya katiba,ila wote kwa nyakati tofauti wamekuwa wakijiinua juu ya katiba!。
13. Serikali imekuwa ikitunga miswada batili kinyume na katiba,mmoja wa miswada hiyo ni muswada wa sheria ya uchaguzi iliyopita!
14. Bunge likatunga sheria batili,Mhimili wa Mahakama Kuu,inazibatilisha hizo sheria batili,serikali ikagoma。
15。 Serikali ikafanya mabadiliko batili ya katiba,ikauchomekea ubatili huo ndani ya katiba yetu!
16. Mahakama Kuu ikashikilia msimamo,mabadiliko hayo ya katiba ni batili na sheria ya uchaguzi ni batilifu!
17。 Mahakama ya Rufani ikazibariki kwa kujinyenyekeza chini ya mhimili wa Bunge,kulibembeleza Bunge ndio liuondoe ubatili huo!。
18. Bunge licha ya kuamriwa na mahakama,kuuondoa ubatili huo, haija uondoa ubatili mpaka leo!。
19. Matokeo yake,katiba yetu bado ina ubatili,sheria mpya ya uchaguzi ina ubatili ule ule ulioshabatilishwa na mahakama!
20. Hata sheria iliyounda Tume Huru ya Uchaguziu,INEC
ni batilifu kwasababu katiba inaitambua Tume ya Uchaguzi NEC.
Hitimisho
Mimi kama mwanafunzi wa Dr Tulia Akson,namuomba mwalimu wangu,kabla ya kuvunjwa kwa Bunge hili,nakuomba mwalimu TA wangu, Tulia Akson,ambaye sasa ni Dk na Spika wa Bungre la JMT,tunaomba Bunge lako lifanye minimum reforms za katiba kuwatendea Watanzania haki ya kuchagua na kuchaguliwa kwa kuuondoa ule ubatili wa sheria ya uchaguzi,na kuihalalisha INEC!
Mungu Mbariki Spika Dr Tulia Aweze!
Mungu Libariki Bunge Liweze!
Mungu Ibariki Tanzania。
Paskali
Leo mzee wa kunyoa kiduku uzee umemwaga material. Uwe unaandika namna hii ukiwa balanced kwa ajili ya wananchi na siyo kwa ajili ya chama fulani.