Baraza Jipya La Mawaziri hili hapa

Nahisi usingizi!!ngoja tu nikalale.Ila hongera Mama Kabaka.Naona Butimba ilikukomaza kwelikweli

Majita ukihisi usingizi hapa ni jamvini mkuu unasema why .Tupe nasi siri ya kuhisi usingizi tuone kama tunaweza kuungana .
 
danganya totoo tuu hana jipya,hata tusitegemee loloto ekwenye issue ya BOT,kwanza PCB ndo watakao chunguza, pili sidhani kama riport itawekwa hadharani hana jipya ,anay way amalize term yake tumtoe 2010
 
Mbona naskia Sophia Simba ni mzigo na uwezo is limited? Je ni sawa kumpa wizara nyeti kama ya rushwa?

1. Kwa taarifa yako, ile wizara iko chini ya Rais sio Simba au mtu mwingine. Waziri ofisi ya Rais ni Msaidizi tu.

2. Boss waa PCCB na Usalama wa Taifa ni Rais mwenyewe.

3. Waziri wa Utawala bora yupo tu kwa ku-manage budget na vitu vichache chache... kama tume ya maadili ambayo pia hu-ripoti kwa Rais moja kwa moja...

4. Nakubaliana nawe kwamba sitamani kuona huyu mama kama waziri but I have nothing i can do.
 
Ukitaka kujua ni kwanini watu wanaquestion, angalia perfomance ya wizara ya ujenzi tangu magufuli aondoke, na baada ya muda mfupi uangalie tena wizara ya Ardhi itakavyokuwa, the qustion is, kama aliiweza ya ujenzi kwanini ahamishwe? Kama ya Ardhi ameiweza kwanini anahamishwa? What about Membe ina maana yeye ndiye ameiweza zaidi wizara ya mambo ya nje?

BongoLander:

Na kuelewa unasema nini. Lakini mawaziri wa-serve at the pleasure of the President na sio wananchi. Na kuna uwezekano mkubwa Magufuli ni Exceptional katika jamii yetu na sio rule.
 
Nahisi usingizi!!ngoja tu nikalale.Ila hongera Mama Kabaka.Naona Butimba ilikukomaza kwelikweli

Butimba ipi, Chuo cha Walimu ama Magereza? Kuna tofauti kubwa hapo, kama alikuwa ni mfungwa ama mwalimu.
 
MzalendoHalisi
Ngoja tuone Mama Simba hapo alipowekwa kwani huyu mama nasikia kabla hajajiunga na siasa alikuwa polisi mwenye cheo cha juu tu.
Na utendaji wake kikazi ulikuwa mzuri
 
Nimesoma between the lines.... Wizara ya Africa Mashari pia imepewa Mzanzibar kama Ilivyo wizara ya Mambo ya Nje

Hili ni Jambo jema kwetu sisi wa Zanzibar... Muungano... Daiiii....ma!!!!
 
Nimesoma between the lines.... Wizara ya Africa Mashari pia imepewa Mzanzibar kama Ilivyo wizara ya Mambo ya Nje

Hili ni Jambo jema kwetu sisi wa Zanzibar... Muungano... Daiiii....ma!!!!

I dont think so---Kamala sio mzanzibar..... huyu ni mbunge wa Nkenge, Kagera.
 
.

PS: Inaonekana JK hata hakuwahi kusoma report ya kile kilicholetekeza wizara ya elimu na elimu ya juu kutenganishwa. Angesoma hata utangulizi wake tu asingezirudisha wizara hizi kuwa pamoja hasa kwa kipindi hiki ambako mahitaji na matakwa ya wizara hizi hayashabihiani.

Unajua wakati mwingine ukiwa huna information unaamini ulichonacho ndio BEST.


Kenya na Uganda wana Wizara moja ya Elimu!!! Naomba nikusaidie na hii ya Uganda

Pia kuwa makini kidogo kusikiliza yote kwa makini. Wizara hii ina Manaibu wawili...

1. Kabaka --- ambaye atashughulikia elimu ya juu....
2. Mahiza --- Ambaye atashughulikia elimu ya awali, primary, Sekondari na Ufundi
3. Kila wilaya itakuwa na maafisa Elimu wawili... wa awali na primay... na wa Sekondari na Ufundi... details will follows... later
 
I dont think so---Kamala sio mzanzibar..... huyu ni mbunge wa Nkenge, Kagera.

Jamaa atakuwa kasoma list tofauti labda aliyo nayo ni ya Karume kama naye kavunja baraza . Ama kweli akili ni nywele na kila mmoja ana zake .
 
Ni Wizara gani hazijaguswa kabisa?
1. Afya na Ustawi wa Jamii (Mwakyusa)

2. Mambo ya Nje (Membe)

3. Miundo Mbinu (Chenge)

Hii inamaanisha utendaji wao unaridhisha?

A:
NB Why Afya?

Takwimu za maambikizo ya Ukimwi Tz ktk hii National Campaign inayoendelea ambapo watu zidi ya million 3 wamepima inaonyesha maambukizo mapya yamepungua toka 7% (2004/05) to 5% yaani kupungua kwa asilimia 28 (28%)! Angalia hata UN recent data over Tanzania wamebadilisha juzi tu kuonyesha Life Expectance Tz ni miaka 54 Mwanamke na 51 mwaname na population ni 40.4 milion!

http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/country_profiles/1072330.stm

Je hii kupungua kwa maambukizo mapya ya ukimwi ni moja ya mafanikio ya Mwakyusa na Dr. Kigoda kutoguswa?

B: Foreign

Tz kupata nafasi kuongoza AU na ujio wa Bush imeimpandisha chart JK akaona asimguse Membe kwa sasa?

C: Barabara

Why Chenge? Nothing new with Chenge!!!!!!????????
 
Natumaini mheshimiwa Raisi alikuwa na sababu na muda wa kutosha kutafakari na kuamua nani na nani awatumie katika kuleta maisha bora kwa kila mtanzania na nani amuondoe katika baraza.

Siamini na sipendi sana msemo unaozidi kuwa maarufu kuwa ILIKUWA NI KAZI NGUMU SANA KUAMUA NANI AWE KWENYE BARAZA! Msemo huu kwangu una implication mbaya...! Raisi hatakiwi kuchagua baraza la mawaziri ili kumfurahisha mtu au kumzawadia mtu. Huwezi kumwacha mtu mbovu kwa kuogopa lawama eti kwa sababu kuna fisadi mmoja atakosa "ulaji". Mbona CVs za watu zinajuliakana, achievements zao zinaeleweka, na ufisadi wao haujajificha? Rais anajua ni mikakati gani ipo kuleta hali nzuri kwa wananchi na anajua ni mawaziri wenye sifa gani anawahitaji kutekeleza hiyo mikakati. Kwa nini kazi ya kuchagua baraza ni ngumu? Au CCM imejaa vilaza!!??? (I am sorry)

Baraza la mawaziri ni chombo muhimu sana kwa Rais mwenyewe, serikali, na taifa kwa ujumla. Hili ni kama mkusanyiko wa mikono, miguu, akili, na zana zote ambazo Rais anaweza kuzitumia kutatua matatizo na kufikia matarajio ya wapiga kura wake. Nionavyo mimi ni kuwa hii ni 2nd chance kwa JK baada ya kufeli kwenye 1st chance. Natumaini alitumia uwezo wake wote kuchagua Baraza la mwanzo lakini "say bahati mbaya" uchaguzi wake ulikuwa ZERO. Matarajio yetu ni kuwa Baraza jipya ni moja ya mkakati wake wa kujirekebisha na kurudi kwenye muelekeo uliokuwa umepotezwa. Kuna uwezekano mkubwa Mheshimiwa Rais ametumia busara zake zote na akili zake zote na za akiba kuchagua na kupanga Baraza jipya. Sisi wananchi tunalipokea baraza jipya kwa MATUMAINI; inawezekana tusiwe na imani sawa na ya kutosha kwa baraza jipya lakini tuna imani na uchaguzi na upangaji wa JK. Lakini wakati huohuo mheshimiwa raisi lazima ajue assessment inayofanywa na wananchi juu ya utendaji wa baraza la mawaziri at the same time ni assessment ya utendaji wa Rais. Baraza lililopita liliboronga; wananchi tunajua lile baraza halikushuka kutoka mbinguni... alilichagua Rais mwenyewe!

Ni ngumu sana kujua kama mabadiliko haya katika baraza Mheshimiwa rais ameyafurahia au amelazimika tu kwa sababu ya kelele za wananchi na JF katika kumkoma nyani giladi! Kwa mtazamo wangu ni kuwa mabadiliko ya Waziri mkuu na baadhi ya mawaziri kumetokea very late ukizingatia muda ambao wananchi wamepiga kelele. Ni ngumu sana kujua sababu za kuchelewa kuchukua hatua kwa kiasi hicho lakini ni matumaini yetu wananchi kuwa Mheshimiwa Rais this time atakuwa SEREOUS KWA NIABA YETU kwa kuchukua hatua haraka pale inapojulikana kuna tatizo katika mawaziri wake.

Siku zote inahitaji moyo na ujasiri katika kuleta mabadiliko na mageuzi katika nchi. Woga, aibu, ushikaji, na mazagazaga mengine ni maadui wakubwa sana katika kujenga jamii iliyo bora na iliyostaarabika.

Sisi kama wananchi tungependa kuona KAZI inafanyika na Taifa linasonga mbele katika maendeleo kiuchumi n.k. Majina ya watu hayatuvutiii wala hayana faida yoyote kwetu. Sina sababu ya kumpongeza wala kumlaumu Jk kwa baraza jipya. Ni uwezo na matunda ya kazi zao ndio tunayoangalia. Ni TIME tu ndio itasema whether I should CONGRATULATE the new cabinet au KOMANYANI-GLADI kama kawa. Najua kuna watanzania wengi sana wanaishi katika dhiki kubwa ndani ya nchi yetu yenye utajiri mwingi. Najua kuna wilaya na vijiji ambavyo watu wanaishi kama ni wakimbizi au watu wasio na kwao. Hii inauma na inakera sana. Hii sio karne ya kuwa na mawaziri wanaoishia kufanya ziara kwa wananchi masikini kila siku kwa kutumia magari ya kifahari utadhani wanaenda kutembelea wadudu mbugani bila kufanya chochote kubadili hali ya maisha ya hawa ndugu zetu.

Tunataka mawaziri wenye vitendo na sio midomo iliyojaa kelele na hekaya za kale. Tunataka viongozi wenye VISON na wanaofanya kazi kwa malengo. Tunataka viongozi wennye busara, akili, na uchungu wa nchi na wananchi waliowapa hizo dhamana za uongozi. Lazima wawe ni viongozi wanaojua wanatutoa wapi wanatupeleka wapi. Tumechoka kuendelea kuwa watumwa na mzigo kwa mataifa mengine duniani.


Mungu ibariki Africa, Mungu Ibariki Tanzania
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom