Barabara ya Strabarg: Kielelezo cha ujinga wetu!

Barabara ya Strabarg: Kielelezo cha ujinga wetu!

Mwenye akili hasifii ujinga.kuna wehu wengne wanacfu sn kazi ya hyu babu hao completly ni wapanda daladal na ht ndoto za gari kw fikra zao potofu naona waendelee kulala huenda wakamalizia kuota.mkuu hamna cku nlokacrika km nilivyotoka cnza najua naingia mabibo sokoni one tme afu naendelea na mambo mengne nikajikuta turn yangu ni kituo kabla ya usalama imagne km c umaskin wa fikra ni nn vp km ingekuw ni mgonjwa anatok one way kuelekea pengne?ilichukua miezi na miezi kufungua hko kanjia still ni worse.

Usitukane wengine kwa kuwa Mungu amekujaalia kupata hicho kijigari chako cha Tshs Milioni 3 si wote wenye uwezo huo! pia Watanzania ndio wanaongoza kuwa na madereva wasio na ujuzi pamoja na Leseni haza wewe Leseni hauna na ndiyo maana ajali nyingi huwa zinatokea Dar kwa kutozingatia sheria za Barabarani kila mtu mwenye kijigali anataka kuwahi tu matokeo ndo hayo. Watanzania wenzangu pia tujifunze kutumia usafiri wa umma wenzetu wazungu wanafanya hivyo baada ya kubaini kuwa ni hasara kubwa kila mtu anaeenda Mjini kutumia usafiri binafsi ila sisu tunasikia fahari kwenda na IST yako Ofisini ili kila mtu akuone kuwa unausafiri wakati unaishi nyumba ya kupanga na kila siku unanyanyasika kwa jambo hili. Pia wakazi wa Dar hawana utaratibu wa maisha kwa utafiti uliofanyika Wakazi wa Dar wanaongoza kwa kuchafua mazingira na mifuko yao ya Rambo kwa kuitupa kila sehemu bila kujali na hasa kwenye mito jambo ambalo si sahihi, pia Wakazo wa Dar wanaongoza kwa kulalamika na kujiona wao ndo Tanzania ila wengine si Tanzania acheni tabia zenu za ajabu ajabu!
 
Umekuja na hasira zote ni kwa kuwa ulipotea njia?

Nyie si ndo hao mliosomeshwa na hii nchi halafu mmekaa tu kulalamika, kwani hamkuona hizo brbr toka zamani?

Watu wengine hambebeki; fanyeni na nyie tuone;
 
Umekuja na hasira zote ni kwa kuwa ulipotea njia?

Nyie si ndo hao mliosomeshwa na hii nchi halafu mmekaa tu kulalamika, kwani hamkuona hizo brbr toka zamani?

Watu wengine hambebeki; fanyeni na nyie tuone;

Duh!!!!! Kweli ukinywa maji ya bendera unajitoa mpk ufahamu.
 
Vurugu ziliziopo Dar es Salaam ni kushindwa kwa mfumo wa uongozi,inabidi kutengeneza mfumo mpya! Dar imeelemewa na foleni za barabarani, uchafu,ujenzi holela,makelele yasiyo ratibiwa kutoka ktk nyumba za Ibada,Bar na Kumbi za Starehe,ujambazi,ukosefu wa maji safi na salama,miundombinu ya majitaka,nk! Lakini kuna watu wengi kuanzia RC,DCs,Wakuregenzi wa Manispaa,Mameya,nk ambao wanalipwa lakini hawana kazi ya maana wanafanya!
hii ndo BRN na DAR tuitakayo ili muelewe vizuri tukisema CCM ni mizigo msiendelee kukataa
 
Tatizo ni wakazi wa dar. Wakazi wa dar wao wanaona pesa ndio maendeleo ivyo kujidai kuwa wako bussy kutafuta pesa pasipo kufuatilia miundo mbinu imekaaje. Hakuna asiejua kuwa dar ndio kila uchafu kinapatikana. Maji shida, foleni ndio usiseme, takataka, magereji kukaa ovyo ovyo. Nilitegemea wakazi wa dar ndio wangekuwa kielelezo ya watanzania kwa kuisimamia serikali ifanye kazi za kimaendeleo lakini wao wanasema wanatafuta pesa. Wakazi wa dar wanawaona wenzao wa mikoani wanapoandamana kudai maji, umeme au usafiri kupanda wanawaona wajinga. Katika dunia hii miji mikubwa ndio chachu ya maendeleo halafu mikoa inafuata. Serikali ikileta usanii ni mgomo wa nguvu na huduma itapatikana. Je unafikiri wakazi wa dar wangeungana pamoja wakaandamana kwa amani kudai maji wangeteseka kwa miaka yote hiyo. Acha mle vumbi kwani mnatafuta pesa. Mnafikiti mtazikwa na pesa
 
Umekuja na hasira zote ni kwa kuwa ulipotea njia?

Nyie si ndo hao mliosomeshwa na hii nchi halafu mmekaa tu kulalamika, kwani hamkuona hizo brbr toka zamani?

Watu wengine hambebeki; fanyeni na nyie tuone;
TUnasubiri 2015 baada ya uchaguzi CDM itaanza kuonesha JIJI la Dar linatakiwa kuwaje CCM tupisheni tuwaoneshe
 
Pro-Chadema kupinga kila kitu Strabarg wanafanya kazi mazingira yanawasumbua.
Ritz kila anayepinga sio cdm, ila hata mimi sikubaliani na lawama zinazotolewa na watu wengi kwa mkandarasi, tatizo kubwa ni serikali yetu siku zote imekuwa ikipitwa na kasi ya wananchi, miundombinu hiyo ilipaswa kujengwa miaka 15 iliyopita. Hata huko Ujerumani wanakolinganishia ujenzi haufanyiki kwenye mazingira magumu namna hiyo, jiji zima halina plan barabara moja ikifungwa hakuna mbadala.
 
  • Thanks
Reactions: Pai
Tatizo lako mleta thread una stress nyingi kichwani mwako,nipe jiji duniani ambalo halina foleni,nipe jiji duniani ambalo miundombinu yake haipanuliwi,mradi wa mabasi yaendayo kasi,ni wa historia ya tangu rais wa kwanza,michoro yake na kila kitu vilikuwepo,serikali ya awamu ya nne imekuja katika utekelezaji tu wa kile ambacho awamu tatu hazikufanya,ni sawa na daraja la kigamboni,michoro yake ipo toka jk.nyerere akiwa rais,kikwete kaja kutekeleza,punguza stress,soma vitu uvijue,na sii thread za kuandika ukiwa kwenye foleni.
Yawezekana hujanisoma vizuri. Hii si foleni. Hii ni zaidi ya foleni. Nimesema hii ni chaos. Haya ni machafuko barabarani. Ni vurugu tupu.
Mimi nimetembea miji mingi mikubwa duniani na hakuna kitu kama hiki tulichonacho dar. Ni ukosefu wa akili ndicho kilichopo.
Miji mikubwa kama Tokyo yenye wakazi milioni 20 haina foleni hata robo ya kwetu kama unataka kuongelea foleni. Huko kuna matreni yapitayo juu. Nenda Malaysia. Nenda Singapore. Nenda Athens. Kote huko ni barabara za juu yaani flyovers na hakuna foleni.
Hoja yako kuwa hii ni miradi iliyobuniwa enzi za Nyerere huoni kuwa baada ya miaka yote hii kupita basi mahitaji yetu yamebadilika? Ndio maana nimeuliza kwenye uzi wangu kuwa miaka hii karne hii unaongelea mabasi yaendayo barabara maalumu? Miji inatumia electric trams na maglev. Maglev ni treni liendalo juu kwenye mono rail. Nimeliona Tokyo mwaka 1990! Leo unajenga barabara ya mabasi! Mungu aturehemu tu
 
Kwanza barabara ya morogoro road ni nyembamba sana, hata kuna muda ukiwa unataka kulipita gari kubwa mfano lorry, kama ukiwa ubavuni na mumefika kwenye corner inabidi mwenye gari dogo utulie maana ukiendelea unawezatolewa kwenye njia...

Pia barabara haina emergency exist mfano gari likikuharibikia mitaa ya rombo itabidi ulisukume mpaka ubungo ndio lihame njia.....

Alaf ujenzi ni wakusuasua sana, maana njia ambayo ipo busy dar nzima kama hiyo ilitakiwa ujenzi wake huwe waakili ya hali ya juu.....wafanye kazi usiku na mchana, sasa wenyewe usiku wanalala

Hapo ndio mtaelewa kwanini walifukuzwa kenya, hawa strabag wangebaki kenya zile flyover na thika road (highway) wangevisikia kwenye bomba

Asa unataka kuovertake lorry kwenye kona we dereva wa wapi?? khaa
 
Mimi kinachoniua ni zege linalomwagwa....cost for nothing...wangetengenza rami fresh wakapaka rangi ikawa njia ya mabadi tu....alafu barabara ya magari mengine wameibana sana wakati eneo nje ya barabara lipo...sijui plan zingine zikoje, .miaka 50 ijayo wataotindua hilo zege kubadili plan (may be kuweka rails) watakuwa na kazi....Mungu atusaidie kwa kweli.....
 
It is broken, it can't be fixed, it must be replaced.

Nimekuwepo huko nchini kwetu kwa kipindi cha miezi miwili (kuishia jana). Nimeona maajabu.

Kwa wale ambao wanadhani tutaweza kubadilika kwa kufanya marekebisho kwenye huu utawala wa CCM, niseme mnaota ndoto za mchana. Ni lazima kutimulia mbali serikali ya CCM.

 
Tatizo lako mleta thread una stress nyingi kichwani mwako,nipe jiji duniani ambalo halina foleni,nipe jiji duniani ambalo miundombinu yake haipanuliwi,mradi wa mabasi yaendayo kasi,ni wa historia ya tangu rais wa kwanza,michoro yake na kila kitu vilikuwepo,serikali ya awamu ya nne imekuja katika utekelezaji tu wa kile ambacho awamu tatu hazikufanya,ni sawa na daraja la kigamboni,michoro yake ipo toka jk.nyerere akiwa rais,kikwete kaja kutekeleza,punguza stress,soma vitu uvijue,na sii thread za kuandika ukiwa kwenye foleni.

Acha kutetea upuuzi ww
 
Barabara hiyo ikikamilika itahitaji madereva kuwa makini zaidi kuliko umakini uliokuwepo barabara ile ya awali...

La hasha kutakuwa na ajali ndogo ndogo nyingi sana kutokana na ufinyu wa barabara labda malori na mabasi ya mikoani yatafutiwe njia nyingine...
 
Magufuli siyo mtaalam walaumuni Tanroads ndiyo wataalam.

Kama ni kulaumiwa washalaumiwa sana. Magufuli anafanya nini sasa kama hata kuwaamrisha tu tanroad waweke vibao na alama hawezi. Mtu unaweza kuingia barabara kuu kutokea feeder road ukatembea hata 3km hujaona kibao cha speed, but ukikutana na trafic wanakupiga fine kwa sababu hukuona kibao kilochopo 5km nyuma!. Hilo nalo Magufuli hana utaalamu nalo?!!!
 
  • Thanks
Reactions: ral
Pro-Chadema kupinga kila kitu Strabarg wanafanya kazi mazingira yanawasumbua.

Ritz, sio kila kitu ukiangalie ki-CHADEMA CHADEMA.....ile barabara haina sehemu ya kuchepuka kama gari imeharibika au kushusha abiria...hata daladala zikishusha abiria zinalazimika kusimama katikati ya lane ya kushoto.....
 
as long as huu mradi ni mabasi na yatakua yanaendeshwa na watu/madereva ambao ndio hawa hawa sidhan kama kuna sababu yoyote ya kuamini kua foleni zitapungua!!!
 
Asa unataka kuovertake lorry kwenye kona we dereva wa wapi?? khaa

Mkuu hii barabara ilivyo, kuna mahali zina kona kama 'toleo' kutokea kwenye barabara ya mabasi yaendayo kasi. Kwa hiyo dereva anayeendesha lane ya kulia (yaani ya ndani) anakutana na kona hii. Hivyo kama kushoto kwake kuna lori, lazima asimame ili kumuacha mwenye lori aende, kwa sababu wa kulia akilazimika kufuata muundo wa kona, lori haliwezi kumuacha....

Nafikiri hii ndio concern ya saimon111 kama sijakosea...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom