Barabara ya Strabarg: Kielelezo cha ujinga wetu!

Barabara ya Strabarg: Kielelezo cha ujinga wetu!

yaani barabara hii inataka watu wengi waache magar nyumbani waingie mjini kwa miguu au wapande hayo magari ya kasi ambayo ni magari ya kawaida yalikuwa haina haja ya kupoteza gharama kuweka zege zile.

Tumeona ulaya gari zinaghorofa moja na ni ndefu sana na zinapita kwenye barabara ya kawaida.
 
Ogah Ngojeni niwapatie kioja kingeni cha Mhe Magufuli. hivi sasa Benki ya Dunia inafadhili mradi uitwao Southern Africa Trade and Transport Facilitation Project (SATTFP), mradi huu ndio umetoa fedha za kufanya ukarabati barabara ya Km150 kabla ya kuingia Iringa hadi Iringa, Iringa- Mafinga na sasa Mafinga-Igawa.

Mradi huu lengo lake ni kukuza biashara na sekta usafirishaji katika nchi za kusini mwa Afrika. Nilitegemea mradi kama huu ungeanza na ukarabati wa barabara ya Dar-Chalinze ili kuunganbisha bandari ya Dar es Salaam na nchi hizo. Lakini kwa kuwa Mhe Magufuli alikwisha udangany umma kuwa waliojenga pembezoni mwa barabara ya Morogoro ni wavamizi wa barabara na Benki ya Duni haitaki kusikia poroja za aina hiyo ameishi kutumia fedhaq za mradi huo kujenga mizani ya Vigwaza tu na kuacha barabara ya Dar-Chalizne ikitafutiwa mwekezaji wa Build-Operate-Transfer.

Ni kwanini tuhangaike na BOT ilihali WB ipo tayari kutukopesha? Ni kwa sababu Mhe Magufuli anataka kulinda heshima tu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu....kwa kweli inanishangaza sana sana......kwani wale watu niliofanya nao kazi wengi wao ni wataalamu wazuri sana sana i.e. first world class engineers (e.g Mfugale, Mujwahuzi, Mar Mujungi (RIP), Dr. Mlinga etc)..... ambayo yamenisaidia sana kwenye international organizations nilizofanyia/ninazofanyia kama mshauri.....

.....Nikiwa kwneye mbali mbali kuna kitu kimoja nimekishuhudia.....i.e. Communication and Public Relations katika miradi kama hii......kila wakati Wananchi walikuwa wna kuwa briefed through Information meetings, Radio/TV Presentations.....njia hizo hizo zinatumika sana kutoa taarifa za TRAFFIC MANAGEMENT.......in one country....seven days notice to the public prior ya kuanza kazi sehmu husika na traffic managemeny ni LAZIMA....vinginevyo hakuna kuanza kazi......Mkandarasi analifahamu hilo well in advance (ipo kwenye CoC and Specs) na hivyo hana excuse ya aina yeyote ile ya kuchelewesha mradi.....
Mkuu Ogah nimefuatilia mradi huu na nimesikitishwa sana na utekelezaji wake.
Hao uliowataja wanaweza kuwa ma Eng wazuri tu,lakini hawakuhusishwa kwenye inception ya project, na ndio maana ya madudu tunayoyaona.
Mradi uliasisiwa katika ofisi za Waziri mkuu chini ya jamaa ambaye tayari ameshatimuliwa kutokana na kuboronga kupita kiasi katika kuongoza mradi.
Pesa ilatikana toka World Bank na wakandarasi wakapewa tenda chap chap bila hata ya kukamilisha kuwepo consultants wala michoro.
Hapo 10% inaelekea ilikuwa inawindwa, wakandarasi wenyewe ni hao wachina na strabag.
 
Ogah Ngojeni niwapatie kioja kingeni cha Mhe Magufuli. hivi sasa Benki ya Dunia inafadhili mradi uitwao Southern Africa Trade and Transport Facilitation Project (SATTFP), mradi huu ndio umetoa fedha za kufanya ukarabati barabara ya Km150 kabla ya kuingia Iringa hadi Iringa, Iringa- Mafinga na sasa Mafinga-Igawa.

Mradi huu lengo lake ni kukuza biashara na sekta usafirishaji katika nchi za kusini mwa Afrika. Nilitegemea mradi kama huu ungeanza na ukarabati wa barabara ya Dar-Chalinze ili kuunganbisha bandari ya Dar es Salaam na nchi hizo. Lakini kwa kuwa Mhe Magufuli alikwisha udangany umma kuwa waliojenga pembezoni mwa barabara ya Morogoro ni wavamizi wa barabara na Benki ya Duni haitaki kusikia poroja za aina hiyo ameishi kutumia fedhaq za mradi huo kujenga mizani ya Vigwaza tu na kuacha barabara ya Dar-Chalizne ikitafutiwa mwekezaji wa Build-Operate-Transfer.

Ni kwanini tuhangaike na BOT ilihali WB ipo tayari kutukopesha? Ni kwa sababu Mhe Magufuli anataka kulinda heshima tu.

whaaaaaat....mbona kuna sehemu nilisoma kuwa WB wako tayari kufadhili Dar Chalinze na kwamba kila kitu kilikuwa tayari!!

BTW......nilishiriki kwenye Feasibility Study and uandaaji ripoti iliyopelekea kupata mkopo wa hizo barabara za Iringa......nafurahi kusikia WB wanafadhili........
 
Hii nchi ni kama haina mwenyewe.sijui kama viongozi wetu hawaoni haya?mi pia imenikuta leo hii unatumia saa moja na nusu kutoka mbezi ubungomfano mzuri pale Kimara mwisho kuna kona hatari sana.sijui akina Magufuli na kelele zao hawaoni au wanasubiri waseme wakati wa kukabidhiwa barabara hii.maana zile kona tayari inasemekana watu washakufa.

Pili hii ni highway.kufungua line moja pale kimara ni adhabu kwa wananchi.hata hiyo line ina mahandaki makubwa na kuzidisha kero. Swali langu kwa wahusika hamuoni hili kwa sababu huwa mnakuwa na escorts ya police au sababu mnapita angani? Its not fair kwanza leo ni weekend kwa nini watufungie barabara?
Kile kipande cha kimara ndiyo wamechemsha kabisa! Juzi tu kuna lori limedondoka kwenye hizo kona na kuangusha conaltainer ambalo limevunja kinga za barabara. Pia magari mawili hayawezi kupita pamoja kwa sababu ni barabara nyembamba sana sehemu hiyo. Kama ulivosema wanasubiri wamalize kujenga then Magufuli atakuja na waandishi wa habari na tv camera zao na kujidai anapima upana wa barabara na kuamuru ivunjwe na kujengwa upya sehemu hiyo na kujipatia ujiko wake na watu watashangilia sana!
 
kwenye hizo kona kona za Kimara kuna siku scania mbili zilikuwa zanapishana zikaishia kuparuzana..kuna siku pia scania yenye tela ilibinuka ikauwa dereva na utingo wake..juzi tena scania likadondosha container..na tutegemee kusikia ajali nyingi zaidi na zaidi.. Kunyoosha bara bara Pale inawezekana hata kama kuna bonde.Sema tu watu wameshakula 10 parcent zao kwahiyo ela ya kugharamia pale panyooke watu washakula..siunajua watu wanapenda pesa kuliko uhai wa mwingine.. majibu ndo barabara ya morogoro road..
 
Nipo barabarani kutokea kimara kuelekea mjini. Njiani ni balaa tupu kwa sababu kuna michepuko ya barabara isiyo na alama yoyote. Nimeingia barabara moja nikaenda kama kilometa 3 nikakuta kizuizi. Ikabidi nirudi tena nilikotoka. Kilometa 3! Nikatafuta sehemu nyingine ya kuingilia na baada ya muda nikagundua nimepotea tena. Tupo wengi tunaopotea; kwani hakuna alama yoyote kuonyesha mwelekeo ni upi.

Nimechukua masaa mawili kufika maeneo ya Ubungo. Hapo nimekuta chaos! chaos! chaos! Haijulikani magari yanaelekea mwelekeo upi! Magari na malori yamekutana uso kwa uso kila mahali na kuzifunga barabara. Huwezi kuamini kuwa hii ni nchi ya kistaarabu hata kidogo. Hakuna mataa na hakuna askari wa kuyaongoza magari yanayopita ovyo na mwishowe kuyabana magari mengine. Sote tumesimama.

Najiuliza: hivi hawa wakubwa wana habari jinsi nchi inavyosulubiwa? Wana habari kuwa tumegeuzwa vichekesho? Je wana habari kuwa huko Ujerumani inakotoka kampuni haiwezekani kufanyika kitu kama hiki na wakapona? Wana habari kuwa viongozi wote waliohusika kuleta upuuzi huu wanaweza kufutwa kazi immediately? Na Uchina viongozi na watendaji waliofanya hii kandarasi ya kiwendawazimu wangenyongwa? Lakini kwetu ni business as usual. Kila kitu kiko sawa tu. Hakuna anayejali. Badala yake vinaonyeshwa vipindi vya tv kusifia huu upuuzi!

Na kinachoudhi zaidi ni kwamba huu mradi ni wa ulaji tu. Hakuna kitakachosaidia kupunguza foleni kwa kujenga barabara maalum ya mabasi yaendayo kasi. Wakubwa wetu hawajui kuwa wanaopanda magari yao binafsi hawatasubstitute magari yao kwa kupanda mabasi yanayonuka. No. Wataendelea kuendesha magari yao na foleni itaongezeka pia.

Wakati wenzetu wanajenga miundombinu ya karne ya 22 sisi tunajenga barabara maalumu ya mabasi! Mungu tusaidie! Kwani hawa wenzetu wakienda kutembea huko nje kila siku hawaoni kinachoendelea huko au alimradi wapate chao mfukoni kwa kuleta miradi aghali na ya kipuuzi isiyo na tija kwetu? Hata wao wanajua huu mradi ni danganya toto tu na ndio maana hata Prof. Tibaijuka alisema huu mradi hauwezi kuondoa foleni!

Sasa kama hata yeye anajua hivo huu mradi ni kwa faida ya nani? Kwa nini tutaabike hivi kwa mradi ambao we know for sure it is useless? Nawaonea huruma watu wangu!

Wewe sio mstaarabu na wazungu wanasema " a non civilized person". Angalia nime bold mstari uliotukana watanzania wenzako! Hako ka gari kako ka mkopo ndio kana kupa jeuri ya kutukana? kisa umepotea njia kwa ulimbukeni wako, mbona wenzako wanafuata njia kama kawaida na hawajawahi kupotea? alama zitawekwaje wakati barabara haijafikia stage ya kuwekewa alama? uliza ma injinia wa barabara watakujuza stage kwa stage na uwekaji wa alama! acha ushamba weee!:angry:
 
Mkuu kakataa WB kufadhili dar chalinze coz hawatakubali hizo porojo zake za kuesita wamiliki halali wa ardhi kuwa ni wavamizi hivyo kaiweka barabara hiyo ktk BOT
 
Ukusoma wenzako wote walivyocontribute kwenye mjadala huu utagundua kuwa hapa si mahali sahihi kwako. Elekeza nguvu zako katika kusoma vitabu ili ufit hapa. Facebook haikufundishi vizuri
 
Ukusoma wenzako wote walivyocontribute kwenye mjadala huu utagundua kuwa hapa si mahali sahihi kwako. Elekeza nguvu zako katika kusoma vitabu ili ufit hapa. Facebook haikufundishi vizuri

Sema HUKUSOMA na sio UKUSOMA! Wewe inakubidi umrudie mwalimu wako wa Kiswahili fasaha! Angalia neno nililoli "bold" katika maandishi yako.:angry:
 
Mkuu kakataa WB kufadhili dar chalinze coz hawatakubali hizo porojo zake za kuesita wamiliki halali wa ardhi kuwa ni wavamizi hivyo kaiweka barabara hiyo ktk BOT

...ni akina nani hao wamepewa hiyo BOOT contract?.......hii miradi ya PPP inabidi iwashirikishe sana wazawa......private sector ya nyumbani inabidi kuchangamkia hizi fursa za PPP........joint venture zipo kibao......muhimu ni sisi wazawa kuandaa Feasibility studies za nguvu na zenye uelekeo...si mnaona wenyewe jinsi wageni/investors wanavyokuja bongo kwa kasi........

......Serikali yetu inabidi isimamie vizuri hili suala la PPP kwa sera ambayo , itawashirikisha, itawalinda na kuwanufaisha wazawa.....
 
Sema HUKUSOMA na sio UKUSOMA! Wewe inakubidi umrudie mwalimu wako wa Kiswahili fasaha! Angalia neno nililoli "bold" katika maandishi yako.:angry:
Ungekuwa unafit forum hii ungegundua kuwa nilimaanisha "ukisoma" na wala sikumaanisha "ukusoma". Rejea ushauri wangu wa awali: rudi facebook. Huko ndiko kunakufaa.
 
Wewe sio mstaarabu na wazungu wanasema " a non civilized person". Angalia nime bold mstari uliotukana watanzania wenzako! Hako ka gari kako ka mkopo ndio kana kupa jeuri ya kutukana? kisa umepotea njia kwa ulimbukeni wako, mbona wenzako wanafuata njia kama kawaida na hawajawahi kupotea? alama zitawekwaje wakati barabara haijafikia stage ya kuwekewa alama? uliza ma injinia wa barabara watakujuza stage kwa stage na uwekaji wa alama! acha ushamba weee!:angry:
Pamoja ba comments zako, nafikiri hujamwelewa mtoa hoja hapo.
Kuna kitu inaitwa "Work scheduling and Traffic Management" hata wakati barabara inajengwa na inatumika.
Hiyo kitu muhimu sana , ingalau katika barabara ya Bagamoyo mkandarasi Konoike anajitahidi sana katika hilo.
Strabag anapwaya sana hapo, na ni kazi ya aliyempa kazi kusimamia utekelzaji wa shughuli hiyo.
 
Back
Top Bottom