nkosikazi
JF-Expert Member
- Mar 11, 2010
- 361
- 337
Nipo barabarani kutokea kimara kuelekea mjini. Njiani ni balaa tupu kwa sababu kuna michepuko ya barabara isiyo na alama yoyote. Nimeingia barabara moja nikaenda kama kilometa 3 nikakuta kizuizi. Ikabidi nirudi tena nilikotoka. Kilometa 3! Nikatafuta sehemu nyingine ya kuingilia na baada ya muda nikagundua nimepotea tena. Tupo wengi tunaopotea; kwani hakuna alama yoyote kuonyesha mwelekeo ni upi.
Nimechukua masaa mawili kufika maeneo ya Ubungo. Hapo nimekuta chaos! chaos! chaos! Haijulikani magari yanaelekea mwelekeo upi! Magari na malori yamekutana uso kwa uso kila mahali na kuzifunga barabara. Huwezi kuamini kuwa hii ni nchi ya kistaarabu hata kidogo. Hakuna mataa na hakuna askari wa kuyaongoza magari yanayopita ovyo na mwishowe kuyabana magari mengine. Sote tumesimama.
Najiuliza: hivi hawa wakubwa wana habari jinsi nchi inavyosulubiwa? Wana habari kuwa tumegeuzwa vichekesho? Je wana habari kuwa huko Ujerumani inakotoka kampuni haiwezekani kufanyika kitu kama hiki na wakapona? Wana habari kuwa viongozi wote waliohusika kuleta upuuzi huu wanaweza kufutwa kazi immediately? Na Uchina viongozi na watendaji waliofanya hii kandarasi ya kiwendawazimu wangenyongwa? Lakini kwetu ni business as usual. Kila kitu kiko sawa tu. Hakuna anayejali. Badala yake vinaonyeshwa vipindi vya tv kusifia huu upuuzi!
Na kinachoudhi zaidi ni kwamba huu mradi ni wa ulaji tu. Hakuna kitakachosaidia kupunguza foleni kwa kujenga barabara maalum ya mabasi yaendayo kasi. Wakubwa wetu hawajui kuwa wanaopanda magari yao binafsi hawatasubstitute magari yao kwa kupanda mabasi yanayonuka. No. Wataendelea kuendesha magari yao na foleni itaongezeka pia.
Wakati wenzetu wanajenga miundombinu ya karne ya 22 sisi tunajenga barabara maalumu ya mabasi! Mungu tusaidie! Kwani hawa wenzetu wakienda kutembea huko nje kila siku hawaoni kinachoendelea huko au alimradi wapate chao mfukoni kwa kuleta miradi aghali na ya kipuuzi isiyo na tija kwetu? Hata wao wanajua huu mradi ni danganya toto tu na ndio maana hata Prof. Tibaijuka alisema huu mradi hauwezi kuondoa foleni!
Sasa kama hata yeye anajua hivo huu mradi ni kwa faida ya nani? Kwa nini tutaabike hivi kwa mradi ambao we know for sure it is useless? Nawaonea huruma watu wangu!