Bandari yawafuata wafanyabiashara 100

Bandari yawafuata wafanyabiashara 100

Yule jamaa kachanganyikiwa haelewi anachotakiwa kufanya kwa sababu ya kukurupuka na kujifanya mjuaji wakati hajui lolote
Ata uwe nani ukizaliwa "kanda ya matetemeko" ukija mjini lazima utakuwa limbukeni na mshamba tu..ndio kinachomsibu Mtukufu atakaa sawa tu.. time will tell
 
Nina hamu hata nimsikie akitamka neno Bandari tu, hivi karibuni. Maana hata neno Sukari silisikii tena kinywani mwake, japo hali bado ni mbaya mtaani bei ni kuanzia 2500 na kuendelea.
Mkuu ule mweleka wa sukari ulikuwa mbaya.. yaani Bwana Kassim ndio alitia huruma jioni moja anatangaza serikali imeingiza sukari wakati sisi tupo bandarini hatukuona huo mzigo, ule ugawaji wa sukari kwa mikoa sijui uliishia wapi..Tokea siku ile nilimdharau sana Ndugu Kassim Mjaaliwa nikajua hatuna mtu
 
PM amesema wamekutana na serikali ya DRC na imewahakikishia kuwa mizigo yote itapitishwa hapa huku wakisahau kuwa serikali sio inayoamua mizigo ipitie wapi bali ni wafanyabiashara binafsi! Bahati mbaya sana karibia ya 70% wafanyabiashara wa TZ sehemu anayobanwa kulipa ushuru stahiki si rafiki kwao!
Ndugu Kassim Mjaaliwa mara nyingi huwa hajui anachoongea.. alisema atakuwa Ubuyu City mwezi wa nane hadi leo yupo mjini anaweka foleni tu.. kuongea bila ya kufikiri kwanza ni jambo baya sana
 
[emoji12] [emoji12] tatizo ni lugha ngumu wanazotumia hata sukari mpaka leo imeshindikana kushuka bei jambo LA kwanza ni kukaa NA wafanya biashara kuongea nao mkubaliane si kuwabeza NA kuitumia lugha za ajabuajabu nguvu itumike pale tu inapohitajika
Sio kama kanuna, sura yake ndo ilivyo.
Hata penseli inakuwa na ufutio pale unapokosea unafanya masahihisho. Wewe pia ukikosea hatukuchukii tunakukumbusha unajirudi na maisha yanaendelea.
 
Sio kama kanuna, sura yake ndo ilivyo.
Hata penseli inakuwa na ufutio pale unapokosea unafanya masahihisho. Wewe pia ukikosea hatukuchukii tunakukumbusha unajirudi na maisha yanaendelea.
Umekosea sukari

Umekosea tena NA tena

Ulimi ni kiungo kidogo sana unaponza kichwa [emoji111] [emoji111] [emoji111] [emoji111]
 
amewafuata tena wakwepa kodi ina maana ile kauli yetu waende huko kwa wakwepa kod wenzao imekaaje inabid na sisi wafanya biashara tuwe na msimamo wetu had atengue kauli yake.
 
Mimi binafsi nawashangaa sana hao viongozi wa Mamlaka ya Bandari kwa uamuzi huo wa kuwafuata wafanyabiashara hao . Kama ni kweli basi wataalam wetu mnashida KUBWA sana: kwa nini nasema hivi....
1. Katika sakata hili kwanza kuna dhana ya kukosa uzalendo na nchi yako.... Wafanya biashara hawa kwa kukosa uzalendo wanatumia bandari za nchi za Jirani lengo ni kuikomoa Serikali iliyopo madarakani .... Wakati huohuo hawa jamaa familia zao na jamaa zao wapo humu nchini na wakati huo huo nao wanadai kuwa huduma zitolewazo na Serikali ni duni .Hapo ndipo tunapotofautiana na Jirani zetu wa Kenya, wenzetu hao hata pawepo na mgongano mpana ndani ya Taifa lao... Daima hawatahujumu masirahi mapana ya Taifa lao...... YOU TANZANIAN WAKE UP acheni Ubinafsi uliotukuka kiasi hicho

2. Nyie viongozi wa TPA mnachokifanya ni kosa kubwa sana katika mfumo .... Leo unania nzuri ya kukaa na hao jamaa zetu...... Lakini eleweni Mswahili ni Mswahili tu na mtu Binafsi ni Binafsi tu...... Kesho mtakuja na mpango mpya wa kuboresha Bandari yetu..... Kama maboresho haya madogo tu imekuwa hivi! Je hayo mengine mapya mtakapohitaji kufanya CHANGES..... Watahamia nchi Jirani tena na itabidi kuwafuata tena na kuwabembeleza?
Kazi Kwenu....: ila kama lengo ni kulipana Posho za vikao na Safari za kuwafuata wadau wasilolitakia mema Taifa lao fanyeni.....
 
Umekosea sukari

Umekosea tena NA tena

Ulimi ni kiuno kidogo sana unaponza kichwa [emoji111] [emoji111] [emoji111] [emoji111]
Ulimi si kiuno, ni kiungo. Kiuno kinaanzia mwisho wa tumbo kushuka chini kidogo
 
Mifumo yenu iimarishe kwanza na ndipo mfanye hili mnalotaka kufanya.
Mimi naamini mfumo utakapoimarishwa mtu atafuata tu Kanuni zenu na ndipo ataamu kufuata kanuni au mfumo au kama hawezi atoke....:: full stop siyo hii ya kubembelezana.... Na Siasa zinachanganywa humohumo - KWA sababu baba Yao kakosa Kura basi na Wachaga wote wamesusia Bandari..... Acheni hizo
 
Back
Top Bottom