MTANZANIA620
Member
- Jun 20, 2023
- 96
- 111
SAMIA NA MAPINDUZI YA BANDARI ZA TANZANIA
Kuna uwekezaji ambao unaonekana kwenye majengo, magati, reli na mitambo. Lakini kuna uwekezaji mwingine ambao thamani yake kubwa haionekani mara moja kwa macho, ni uwekezaji unaobadilisha namna nchi inavyounganishwa na biashara ya kikanda, namna mizigo inavyosafirishwa na namna uchumi unavyotengeneza ajira na mapato.
Ndivyo tunavyoweza kuutazama uwekezaji unaoendelea katika bandari za Tanzania chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. Kwa mujibu wa taarifa za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Serikali imewekeza zaidi ya Shilingi trilioni 10.08 katika miradi 22 ya ujenzi, upanuzi na maboresho ya bandari nchini.
Serikali imeeleza kuwa uwekezaji huu ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha miundombinu ya usafiri wa majini na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara na usafirishaji katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini.
Mpango huu umepelekea uwezo wa TPA kuhudumia shehena kuongezeka kutoka tani milioni 18.67 mwaka 2021/22 hadi tani milioni 39.898 mwaka 2026/27 ongezeko la zaidi ya mara mbili.
Kigoma kutoka Bandari ya Mkoa hadi lango la Maziwa Makuu. Bandari ya Kigoma inatoa picha nzuri ya maana ya uwekezaji huu.
Kwa mujibu wa taarifa ya TPA, uwekezaji wa zaidi ya Sh bilioni 100 umefanywa katika bandari ya Kigoma na umepelekea ongezeko la shehena inayohudumiwa na Bandari ya Kigoma kutoka wastani wa tani 200,000 hadi tani 815,285.
Mafanikio haya ni ishara kwamba bandari inapokuwa na miundombinu, vifaa, huduma na muunganiko mzuri wa usafirishaji, eneo linaloizunguka linaweza kubadilika kutoka kuwa mwisho wa safari na kuwa lango la biashara.
Serikali pia inaendelea kuboresha gati la mizigo, gati la abiria, jengo la abiria na barabara ya kuingia na kutoka bandarini. TPA imeeleza kuwa miradi hiyo inalenga kuongeza uwezo wa kuhudumia mizigo, kuimarisha biashara ya kikanda na kuongeza ushindani wa Bandari ya Kigoma.
Na hapa ndipo umuhimu wa Kigoma unapoonekana. Kigoma iko kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika, ikitazamana na masoko ya mikoa ya Rukwa na Katavi pamoja na Nchi jirani za DRC, Burundi na Zambia. Serikali imeeleza kuwa maboresho ya miundombinu hiyo yanalenga kuiwezesha Kigoma na Tanzania kuhudumia masoko hayo na kuimarisha Ushoroba wa Kati.
Kwa hiyo, uwekezaji katika bandari ya Kigoma haupaswi kutazamwa kama uwekezaji wa bandari moja pekee. Ni sehemu ya mfumo mpana wa uchumi kuanzia Dar es Salaam – SGR - Tabora – Kigoma – Meli Ziwa Tanganyika – masoko ya Maziwa Makuu.
Tanzania ina nafasi ya kipekee kijiografia. Ina bahari, maziwa, reli, barabara na mipaka inayoiunganisha na masoko makubwa ya DRC, Zambia, Burundi, Uganda, Rwanda mpaka Afrika ya Kati. Lakini jiografia inakuwa na faida ya kiuchumi pale inapounganishwa na miundombinu yenye ufanisi.
Hapo ndipo uwekezaji wa Serikali ya Awamu ya Sita katika bandari, reli na miundombinu ya usafirishaji unapopata uzito. Kigoma inapoimarika, Ziwa Tanganyika linafunguka zaidi.
SGR inapoendelea kuelekea magharibi, ushoroba wa kati unaimarika.
Bandari ya Dar es Salaam inapokuwa na ufanisi zaidi, nchi zisizo na bandari zinapata njia mbadala ya biashara.
Bandari kavu zinapoboreshwa, msongamano unaweza kupunguzwa na mizigo kusogezwa karibu zaidi na walaji na wazalishaji kwa haraka na gharama nafuu zaidi.
Na biashara inapoongezeka, fursa ya ajira, uwekezaji na mapato huongezeka pamoja nayo.
Tanzania inapojenga bandari, reli na njia za biashara kwa wakati mmoja inajenga nafasi yake katika ramani ya biashara ya Afrika. Katika uchumi wa karne hii, nchi inayoweza kusafirisha bidhaa kwa haraka, kwa gharama nafuu na kwa uhakika ndiyo yenye uwezo mkubwa zaidi wa kuvutia biashara na uwekezaji katika viwanda. Huo ndio uzito wa uwekezaji wa leo na mapinduzi katika bandari za Tanzania unaofanywa na Shujaa Mkimya Dkt Samia Suluhu Hassan.