Siku zote tunapopata cheo tujififunze kuomba kama Sulemani, yeye alipopewa cheo cha ufalme wa Israeli na wazee wa Israeli alikwenda mbele za Mungu akamwambia Mungu, mimi ni mchofu na sina chochote pasipo wewe na jamii hii nayotakiwa kuiongoza ni kubwa mno, naomba unijalie mimi mja wako ufahamu, maarifa na hekima ili nijue namna ya kuingia na kutoka mbele ya jamii hii (2Nya 1:7-12).