Bandari ya Bagamoyo haiwezi kujengwa DP World akiwa kinara wa bandari zote za Tanganyika

Kalamu

JF-Expert Member
Nov 26, 2006
7,689
8,869
Ujuha wetu ni kuendelea kudanganywa kwamba ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo tutauanza hivi karibuni; kama tunavyozimwa akili na kutengwa kwa Bajeti ya kazi hiyo kulikowasilishwa na Waziri Mbarawa Bungeni.

Hivi hawa watu hata kudanganya waziwazi hawana uwezo nako?

Au sasa watageuza habari na kueleza kwamba huo nao ni mradi atakaoushughulikia DP World?

Naona huyu DP World atakuwa ameteka akili zetu zote. Uaminifu wa kiasi hiki kwa nchi nyingine kukuendeshea maisha ya nchi yako namna hii siyo rahisi kukiona mahali kwingine popote duniani.
 
Bandari ya Bagmoyo ikijengwa utatokea mgogoro kama ule wa Doraleh Contena terminal ya Djibouti na DPWorld.
 
Back
Top Bottom