Balozi wa Uswisi nchini Tanzania atembelea ofisi za JamiiForums

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,689
218,192
Taarifa iliyosambazwa na viongozi wa JF inasema kwamba, Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Didier Chassot ametinga kwenye ofisi za JF kwa lengo la kukutana na baadhi ya watendaji wa taasisi hiyo, akiwemo Mkurugenzi, Maxence Melo.

JF inasimamia mtandao wa JamiiForums.com, unaoongoza kwa kutoa uhuru wa maoni barani Africa. Balozi amefika JF kwa lengo la kuona namna ya kuendeleza uhusiano mwema baina Uswisi na JF.

Taarifa zaidi zinaonyesha kwamba Uhusiano wa ubalozi huo na JF unatimiza miaka 10 sasa.

Jamiiforums.jpeg

Ofisi za JamiiForums zilizopo Kawe, Dar es Salaam

jamiiforums JF.jpeg

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo akiwa kwenye picha ya pamoja na balozi wa Uswiss nchini, Didier Chassot

09CED776-BFC9-4724-9111-A0AEABB3E07D.jpeg

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo akimuelekeza jambo balozi wa Uswiss nchini, Didier Chassot

3..jpg

Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo akibadilishana mawazo na Balozi Didier Chassot.

2..jpg
1..jpg


Wafanyakazi Jamiiforums.jpeg

Baadhi ya watendaji wa JamiiForums wakiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi Didier Chassot.​

Mungu ibariki JF
 
Nimevutiwa zaidi na "maua" ya kwenye kikombe cha chai!

Dah!

Hawa wafanya kazi wa JF ni vijana wadogo sana; au ni 'interns', au wanafunzi wanaotembelea ofisi hiyo?

Hii 'uniform' ya 'vimau' inahitaji ubunifu zaidi.

Kwa hiyo tuseme hawa mabalozi wa nchi mbalimbali hufuatilia mijadala inayoendelea hapo JF? Mbona wengi wao ni Mabeberu tu, hakuna waswahili wenzetu walio na 'interest' ya waswahili wenzao?
 
Hivi 12:44 AM ni usiku au asubuhi?
Usiku wa 'manane', kabla hata ya alfajiri. Sijui kama hiyo itasaidia kujibu swali!
Hakika.

Hususani hapa TZ, ndiyo media inayoongoza Kwa kusema Ukweli na Uwazi.

Siyo kama Ile luninga, inayojiita ya Ukweli na Uwazi, kumbe yenyewe imeegemea kwenye kutoa propaganda tu za Chama tawala😎
Umenifanya niutambue ukweli ambayo ndiyo kwanza nauona.

Ni mzaha usioelezeka kulinganisha TBC na JF.
Pangekuwa kuna haki, bajeti inayopangwa kila mwaka kwa kuendesha TBC, ingestahili wapewe JF.
 
Back
Top Bottom