Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na Balozi wa Ujerumani nchini waitembelea JamiiForums

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
Leo, Februari 28, 2024, JamiiForums imetembelewa na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Christine Grau, pamoja na Thomas Terstegen, ambaye ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania

Ujumbe wa Mabalozi hao umepata nafasi ya kukutana na Watendaji wa JF na kuona shughuli mbalimbali za Taasisi ikiwa ni pamoja Programu 8 zinazotekelezwa.

20240228_192925.jpg
20240228_192928.jpg
20240228_192934.jpg
20240228_192937.jpg
20240228_192949.jpg
20240228_192952.jpg
 
Ninachowafurahiaga ma IT ni kwamba, huwa hawana complications, wanavaa very simple, wengine utakuta amebeba kibegi kama mwanafunzi kina laptop yake chini ana raba za kawaida tu hajali, ila mambo yao ni makubwa sana.

Ona tu JF walivyounganisha watu hadi sisi wengine tunapata nafasi ya kukumbushana na watu Neno la Mungu. Mungu awabariki sana.
 
Ndio Ukoloni mamboleo huo.

Pamoja na kuitangaza JF kimataifa, which is a good thing, nadhani, kama wengine walivoona, kuwepo na umakini mkubwa sana.

Tusije tukajisauau kusukuma ajenda zilizo na maadili ya Kiafrika, tukaendeleza ajenda za Ukoloni mamboleo.

Nawaza tu, hivi mabalozi wetu wakiwa nje huwa wanatenbelea Jamiiforums za huko?

Ahsante kwa Taarifa.
 
JamiiForums inazidi kuwa chombo tajwa zaidi nyumbani na kimataifa.

Kongole kwa JamiiForums kuongoza katika kuhabarisha umma mpana kwa njia ya Kisasa zaidi na kuwa tegemeo kwa wengi
 
Back
Top Bottom