Balozi wa Uingereza, Sarah Cooke atembelea Makao Makuu ya JamiiForums

Vizuri sana. Wenye busara wanaona jinsi JF inavyochangia elimu pana na demokrasia Tanzania.

Ni muhimu kuwe na sehemu ya JF ambayo iko nje ya inakoweza kufika dola. Yaani tawi la nje. Huo ndiyo ukweli.

Hongera zetu kwa ugeni huu. Hiki chombo kimetukuta (wengine tuko tangu 2006 na tulirithiwa kutoka BCSTIMES) na ni sala yetu kidumu kiasi kwamba tukiache kipo tutakapomaliza safari yetu.

Cha kuelewa kutokana na kutembelewa na ugeni mzito kama huu ni kwamba tunatambuliwa na kudhaminiwa kimataifa
 
No easy way to go.. But when you are determined nothing will hinder your path..
JF haikufika hapa ilipofikia kwa bahati mbaya wala kwa bahati nasibu... Imepitia njia ngumu na ya tabu nyingi bila kusahau misukosuko ya kila aina

Jr
 
Mmeanza kukaribisha mabeberu? Hawafanyi urafiki na mtu bila self motives behind their backs, be careful
 
Wenzetu wanatumia akili nyingi sana kufikisha ujumbe kwa walengwa. Huo ugeni ilikuwa ni hakikisho la Wanadplomasia kwamba Jamii Forum inafahamika kazi zake na sasa inawekewa ulinzi rasmi. Ujumbe umelengwa kwa wenye nia mbaya na Jamii Forum.. Asomae na afahamu.

Bila shaka yoyote hukumu dhidi ya kesi yao inabidi iandikwe upya..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe utakuwa ni new member , unapost vitu ambavyo watu washajadili wakachoka wakaamua kuunga juhudi
Kivipi new member Mkuu? Mimi niko na zaidi ya 11yrs hapa Ila mambo yamebadilika sana ndiyo maana sifuatilii. Wanasema if you cannot fight them, join them. Ndiyo kilichotokea. Kuna kipindi kulikuwa na malalamiko ya kuuza mechi na sijui yaliishia wapi.
 
Back
Top Bottom