Balozi Kilima: Asilimia 40 ya mabinti wa kazi wanaofanya kazi Oman wanatoka Kondoa

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Akizungumza katika mkutano wa Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus na Vyombo vya Habari leo tarehe 15 Novemba, 2023, kuhusu ziara za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, alizozifanya nchini Morocco na Saudi Arabia, Balozi Abdallah Abasi Kilima amesema wakati akiwa Oman katika wasichana 10 wa kitanzania wanaofanya kazi Oman, Wanne wanatokea eneo la Kondoa mkoani Dodoma.

Idadi hiyo ni sawa na asilimia 40 ambapo amesema kwa takwimu zisizo rasmi katika kila kaya yenye maisha mazuri Kondoa basi katika kaya mbili au tatu zina binti anayefanya kazi za ndani Oman

Balozi Kilima ambaye amewahi kuhudumu kama Balozi wa Tanzania huko Oman ameeleza kuwa mabinti wengi wanaofanya kazi za ndani maeneo ya Mashariki ya Kati wamewekeza kwa kiasi kikubwa nyumbani Tanzania ambapo ametoa mfano wa Kondoa kuwa kuna eneo linaitwa Muscat ambapo kuna nyumba nyingi ambazo zimejengwa na mabinti wa kazi wanaofanya kazi Mashariki ya Kati.

Ameeleza kuwa Oman kuna Watanzania 25,000 wanaofanya kazi ambapo kati ya hao 17,000-18,000 wanafanya kazi za ndani na ni asilimia 8 tu ya wanaopitia changamoto huku asilimia 92 wakifanya kazi kwa usalama na ubora. Amesisitiza kuwa wanaopitia changamoto wengi ni wale waliopitia nje ya mfumo na ndio maana Serikali ya Tanzania imesaini mikataba inayowawezesha Watanzania kufanya kazi kwa ubora na usalama.

View: https://www.youtube.com/watch?v=lSlntmRv2sA

MSIENDE KUA WATUMWA ARABUNI WADOGO ZANGU
 
Kama taifa limeona ni vizuri na bora wananchi wake wakawe watumishi wa ndani sio mbali sana tutakuwa nusu utumwa nusu huru.
 
Wanyalukolo tumejikomboa miaka 15 iliyopita mabinti wa kazi za ndani walitoka Iringa ila sasa wahehe tumejazana vyuo vikuu na vyuo vya kati.
 
Back
Top Bottom