Ludovick Utouh: Wanawake wanaofanya kazi kwenye masoko mengi ya zamani mazingira yanayowazunguka sio rafiki

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Mkurugenzi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya WAJIBU Institute, CPA . Ludovick Utouh amesema kuwa Wanawake wanaofanya kazi soko hususani kwenye masoko ya zamani wanafanyakazi katika mazingira magumu sana.

Amesema kuwa katika utafiti wao walioufanya Mwaka juzi na mwaka jana (2022-2023) walibaini mazingira yasiyo rafiki yanayowazonguka wakina Mama wanaofanya kazi sokoni, akitolea mfano soko la Mahakama ya ndizi lililoko Mabibo, Ubungo jijini Dar es Salaam.

"Taasisi ya Wajibu kwa kushirikiana na taasisi ya Equality for Growth tulifanya utafiti kuhusu miundombinu ya masoko tuliyonayo hapa nchini, ni ukweli Serikali umejitahidi miaka 10 iliyopita kujenga masoko mapya, ambapo masoko mengi yanayojengwa sasa yanajengwa kisasa lakini masoko yetu mengi ni ya kizamani." amesema Ludovick Utouh

Ameeleza kuwa "Kuna sehemu unakuta wakina Mama wanafanya biashara mapaa hayapo, hakuna meza, ikinyesha mvua ni tope nafikiri wote ni mashahidi kama mmeshakwenda kwenye lile soko la Mahakama ya ndizi ikinyesha mvua pale ni kasheshe. Wakina Mama awa kuna wakati wanakuja na Watoto wachanaga hawana mazingira mazuri ya kukaa na Watoto wao, kwahiyo unakuta Mama hapo hapo anapofanyia biashara ana mtoto mgongoni, shughuli zote za mtoto ni hapo hapo kusema kweli inakuwa sio vyema"

Kupitia utafiti huo Mkurugenzi huyo ambaye aliwai kuwa Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amesema kwa umoja wao taasisi hizo mbili zinakusudia kutoa ushauri kwa Serikali juu kuhusu hali ilivyo na namna bora ya kuboresha masoko hayo.

"Kutokana na utafiti tulioufanya tutakaa na Serikali tuishauri namna ipi bora ya kuboresha haya masoko ya zamani'' amesema Ludovick Utouh

Hayo ameyasema Machi 22, 2023 akiwa kwenye uzinduzi wa 'zoezi la uchukuaji wa taarifa za Wanawake wafanyabiashara sokoni kupitia App' lililofanyika kwenye soko la Tabata Jijini Dar es salaam, zoezi linaloratibiwa na taasisi ya Equality for Growth (EfG).

Ambapo Mkurugenzi wa EfG, Jane Magigita amesema kuwa sokoni ni mazingira ambayo Wanawake wengi wamekuwa wakiiona wanaweza kuwekeza kwa kutokana na wengi wao kutokuwa na uwezo wa kumudu kulipia fremu kwenye maeneo mbalimbali, lakini anadai bado katika mazingira hayo wanakumbana na changamoto ambazo kuna umuhimu wa kuzitatua, ambapo ametolea mfano kuwa bado Wanawake wengi ambao ni wafanyabiashara masokoni wanawekeza pesa zoa kwenye vyanzo visivyo rasmi ambayo inawafanya washindwe kupiga hatua.

Akifafanua mfumo huo amesema "Taasisi yetu imezindua zoezi la uchukuaji wa taarifa za Wanawake wafanyabiashara sokoni kupitia App iliyotengenezwa kupitia Play store.Lengo la kuwa na jukwaa hili ni kukusanya taarifa muhimu za Wanawake wafanyabiashara sokoni Tanzania, kama mnavyofahamu shirika hili (Equality for Growth) limejikita kujenga uwezo wa sekta isiyo rasmi Tanzania hususani kwa Wanawake"amesema Mkurugenzi huyo

Akieleza juu ya muitikio wa Wanawake wafanyabiashara sokoni kuwekeza kwenye masoko ya hisa na mitaji, mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa zoezi hilo, Kaimu Afisa Mtendaji wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Mary Mniwasa amesema kiwango cha Wanawake wanaowekeza kwenye masoko ya hisa na mitaji ni wachache ukilinganisha na idadi ya Wanawake wafanyabiashara ambao wapo nchini.

"Kwenye data zetu idadi ya Wanawake ni chache ukilinganisha na Wanawake walioko nchini mwetu, na hii ni kwa vile bado Wanawake wengi awashiriki kwenye masoko ya hisa na mitaji kama wawekezaji, unakuta Wanawake wengi wanajihusisha na vikoba, ukopeshanaji, wanase upatu lakini hawakumbuki kuwekeza kwenye mifumo iliyo rasmi."amesema Kaimu Afisa Mtendaji huyoView attachment 2942548View attachment 2942549View attachment 2942550
Screenshot_20240323-140737_1.jpg


Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom