mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,208
- 1,109
Katika Siasa Hakuna Rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu....Lolote Lawezekana..
Zipo taarifa za chini kwa chini zinazodai kuwa Balozi Juma Mwapachu ana mpango wa kurejea CCM. Mpaka sasa bado haijafahamika ni sababu zipi hasa zilizompelekea kufikia uamuzi huo.
Itakumbukwa kwamba wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana, Balozi Mwapachu alirudisha kadi za TANU na CCM na kutangaza kumuunga mkono aliyekuwa mgombea Urais wa CHADEMA, Edward Lowassa.
=======
UPDATES:
Hatimaye imekuwa kweli. Balozi Mwapachu ametangaza rasmi kurejea CCM
MBONA HAVAI YALE MAVAZI YETU??Sitawashangaa kwa propaganda zenu hizi. kwani mlianza wakati wa kampeni kuwa LOWASA endapo akishindwa kupata uraisi atarudi CCM kwani kule CDM amefuata cheo na siyo uanachama wa CDM.
Mkapatwa na aibu kubwa sana baada ya kuona kuwa mh. Lowasa bado yupo ngangari ndani ya CDM pamoja na UKAWA bado inadunda tu.
Mlipatwa na AIBU KUBWA SANA majuzi mlipomuona Mh. Lowasa akiwa katika mkutano mkuu wa CHADEMA pale jijini MWANZA.
Mlipata aibu kubwa majuzi mliposhuhudia mama Regina Lowasa akiwa na BAWACHA pale hospitali ya Morogoro wakifanya usafi pamoja na kutoa misaada katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani.
NI AIBU YENU MILELE.
BADO MTASEMA MENGI. View attachment 330172
Sitawashangaa kwa propaganda zenu hizi. kwani mlianza wakati wa kampeni kuwa LOWASA endapo akishindwa kupata uraisi atarudi CCM kwani kule CDM amefuata cheo na siyo uanachama wa CDM.
Mkapatwa na aibu kubwa sana baada ya kuona kuwa mh. Lowasa bado yupo ngangari ndani ya CDM pamoja na UKAWA bado inadunda tu.
Mlipatwa na AIBU KUBWA SANA majuzi mlipomuona Mh. Lowasa akiwa katika mkutano mkuu wa CHADEMA pale jijini MWANZA.
Mlipata aibu kubwa majuzi mliposhuhudia mama Regina Lowasa akiwa na BAWACHA pale hospitali ya Morogoro wakifanya usafi pamoja na kutoa misaada katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani.
NI AIBU YENU MILELE.
BADO MTASEMA MENGI. View attachment 330172
Itakua aliomba mwenyewe kurudi CCM,lakini wale vijana pale Lumumba wakampa masharti magumu,mojawapo ni hili la kumchafulia jina kwa kumwandikia risala kama hii aisome au aitume mbele ya media.Tuseme hii habari ni ya kweli....
Kwani hawezi kuishi bila ya kuwa CCM?
Yaani baada ya kuondoka kwa drama vile sasa anaamua kurudi tena?
Alivokuwa anamuunga mkono lowassa na story za bruce lee hukumwona?Hana madhara huyo kwani hakuwa mwanachama wa chama chochote cha Ukawa..
Mtu mzima, tena msomi na mwandishi wa kitabu cha Uongozi/Utawala, na zaidi ya yote mwanadiplomasia, anapokosa kuwa na msimamo tunamwiitaje!? Tukisema ni kibaraka waungwana watamshangaa, na ukimwiita mnafiki marafiki zake watamwogopa kama ukoma. Sasa tumwiiteje. Nadhani inatosha kusema ni mmoja wenye akili finyu zisizoweza kufanya uchambuzi wa mambo, ambaye kama mkristo, Yesu angemwambia hajui atendalo. Hata hivyo, mimi simshangai maana hata wakati wa siasa ya Ujamaa alikuwa critic wa mfumo ule; lakini leo anamfananisha Rais JP Magufuli na Nyerere, mw,asisi na mtetezi wa mfumo huo wa Ujamaa. Linalonisikitisha ni kwamba Taifa lilipoteza raslimali zake kumsomesha mtu ambaye hakuweza kuelimika japo alipitia elimu ya juu! Chama kiwe na tahadhari naye.serikali"Aibu iliyoje!! Bado najiuliza hivi kabla ya kutoa tamko hili alipata wasaa wa kushauriana japo na familia yake? Ni fedheha kubwa Mzee kama huyu kujidhalilisha kiasi hiki"eti shughuli zake na washirika wake zisikwamishwe na serikali"
Keshapoteza hata ile heshima kidogo aliyokuwa nayo. Hata huko ugambani hawatamwamini tena.