Balozi Juma Mwapachu atangaza kurejea CCM...

Balozi Juma Mwapachu atangaza kurejea CCM...

Jf members wake Mara nyingi huwa hawababaishi habari zao......l
 
Wametuharibia Chadema hadi imepoteza mwelekeo.
 
Magufuli anajua anachokifanya na hana cha kupoteza kabisa hata akichukiwa, kwanza hakuwa amewekeza nguvu na rasilimali nyingi kwenye urais kwahiyo huyu jamaa hatachekea kima na hakuna wakumlaumu kuhusu mipango yao ya kugawana vyeo
 
Waswahili wanafiki sana dont dare to trust them,huwa hawana msimamo kabisa
 
Ni kweli inabidi vyama vyetu viwe na msimamo, tuwatathimini wanaohama vyama, wanakotoka na wanakoenda, watu wanaona ufahali Kuhama Chama na kupokelewa kwingine kwa mbwembwe, ifikie hatua tubadilike.
 
kwa hili la mwapachu ni full aibu. ningelikuwa mimi ndo katibu mkuu wa ccm nisingeruhusu kupokea wachumia tumbo kama hawa kamwe.....
Hii ndio wahenga waliita 'kuzeeka vibaya'! Sasa anafikiri katika umri huu arejee CCm au abaki huko alikokuwa amekwenda, kweli kuna mtu atampa hata u-DC? Hawa ndio the so called 'wasomi wa Tanzania' waliotufikisha hapa tulipo. Hahwezi kufikiri zaidi ya urefu wa pua zao!
 
Kwa masikitiko makubwa sana sana nakuhurumia mzee Mwapachu. Dah! Jamani, umeahidiwa nini weye?? Umeona nini cha kuuzidi utu wako?? Ka ingelikuwa mimi, ningekufa kijaluo na tai yangu shingoni.
Umejidhalilisha, umejivuruga, umejiua mwenyewe. Hutakaa uinuke tena kisiasa milele. Kwa heri muhishimiwa, aksante kwa kujinyonga hadharani tena ukiwa uchi. Hata wangeliniambia ningeukwaa u PM, fedheha hii haitoshi
 
Aibu ya karne,kigeugeu
Hajui kufa kishujaa huyu
Watu wanakomaa na maamuzi yao hadi mwisho
 
Lowassa aliwadanganya sana hawa jamaa zake bado Kingunge.

Mwapachu alidhani Lowassa atakuwa rais.

Teh teh teh!
 
Hizi ndimi mbili hizi hasa za watu wenye hadhi kama ya huyu mzee ni hasara kwa taifa, hatujui tunataka kitu gani kama nchi..Sababu iliyomtoa CCM ni tofauti lakini nia ni ile ile (Ubinafsi)....
 
.... "Na sasa nimeamua kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwasababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu".
 
Sasa kubwa kuliko linakuja nalo ni la fisadi Lowasa, subiri uone sasa hivi ranchi yetu Handeni iliyoporwa na fisadi Lowasa inarudishwa mikononi mwa Wananchi na hapo ndiyo mtajua kwamba Wanasiasa wa kibongo wote wezi tu!
Lowassa ni fisadi wa nini?Hebu acheni kudhalilisha watu kwa sababu ya mihemuko yenu
Ya kijinga.
 
Chadema ya mbowe ni kama demu...unamtenda baadae unarudi na hela anakusamehe,Lowasa ni kansa atabaki saana tu hadi maji yapowe kama mrema.

Hivi hauwezi kuchangia bila ya kuweka itikadi za vyama mbele?
 
.... "Na sasa nimeamua kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwasababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu".

Lipo jambo kubwa nyuma ya maneno haya...
 
Back
Top Bottom