Balozi Juma Mwapachu atangaza kurejea CCM...

Balozi Juma Mwapachu atangaza kurejea CCM...

Zipo taarifa za chini kwa chini zinazodai kuwa Balozi Juma Mwapachu ana mpango wa kurejea CCM. Mpaka sasa bado haijafahamika ni sababu zipi hasa zilizompelekea kufikia uamuzi huo.

Itakumbukwa kwamba wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana, Balozi Mwapachu alirudisha kadi za TANU na CCM na kutangaza kumuunga mkono aliyekuwa mgombea Urais wa CHADEMA, Edward Lowassa.

=======

UPDATES:

Hatimaye imekuwa kweli!

HOTUBA YA BALOZI JUMA MWAPACHU KUTANGAZA KUREJEA CCM

MIKOCHENI 16/03/2016

Ndugu zangu,

Mtakumbuka kwamba mnamo tarehe 13 Oktoba 2015, nilitangaza kuihama CCM na kurejesha kadi yangu ya uanachama kwenye ofisi ya CCM Kata ya Mikocheni. Nilitoa maelezo kwanini niliamua kujiondoa CCM (maelezo hayo pia niliyabandika katika ukurasa wangu wa facebook). Nilieleza kwamba CCM imepoteza mwelekeo kwa kuamua kumnyima haki ya kugombea mcha mungu Edward Lowassa. Nikasema Edward Lowassa ndiye chaguo la wana-CCM na ndiye chaguo la Watanzania. Nikasema nitakuwa mnafiki nikiendelea kubaki CCM huku naamini Edward Lowasa anafaa kuwa Rais kuliko John Pombe Magufuli.

Baada ya miezi miwili ya uongozi wa Magufuli nataka niseme nilikosea sana. Nililewa mahaba ya Lowassa, nililewa ahadi ya Lowassa kunipa uwaziri wa mambo ya Nje. Niliamini mafuriko ya Lowassa ambayo yakanifanya niamini kabisa anachukua nchi. Tulikubaliana na wenzangu kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa wimbi kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini baadhi wakaogopa na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo.

Leo natangaza kurudi CCM kwa sababu nimeona kazi nzuri ya Magufuli. Nimefanya kosa kubwa katika siasa ambalo nawasihi vijana kwenye siasa wasifanye. Nilihama kwa kwa sababu ya mtu (Lowassa). Nimerudi kwa sababu ya mtu (Magufuli). Nataka niwaahidi kwamba CCM ikiweka mtu hovyo baada ya Magufuli, sitahama. Usemi wa CCM kwamba Chama Kwanza, Mtu Baadaye sasa ndio nauona maana yake. Niliwalaumu CCM kwa kumuacha Lowassa lakini sikujua kwamba CCM ina uwezo wa miujiza wa kuibua jembe bora linaloitwa Magufuli.

Naomba mnisamehe kwa kulifanya jambo langu la kujitoa CCM na kurudi CCM kuwa jambo la kitaifa ukizingatia kwamba sikuwa na nafasi yoyote ya uongozi wa CCM wakati nahama na pia sijawahi kuwa hata Mjumbe wa NEC ya CCM na nilikuwa nje ya ulingo wa siasa za CCM kwa miaka 20. Niliamua kulifanya jambo kubwa ili kumsaidia Lowassa. Na sasa nimeamua kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwa sababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu.

Naomba radhi kwa familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa kuitumia kisiasa siku aliyokufa (tar 14 Octoba) na kutumia msiba wake kutoa kauli za kisiasa zidi ya chama chake alichokiunda na ambacho hadi anakufa alikuwa mwanachama.

Wananchi wote tumuombee Magufuli na tumsaidie kwani tumepata Nyerere mpya.

Mungu Ibariki Tanzania
mungu Ibariki Afrika

Balozi Juma Mwapachu
Anatafuta ukuu wa mkoa huyo. Tena nawashauri ccm muwe macho sana na watu wa aina hiyo.
 
Hata kila mtu arudi sisi tutabaki kupambana na huyu mdudu ccm
Utasubiri sanaaaaaa tu huyu mdudu haondoki itabidi WEWE ndio uwe mkimbizi.RDC,Ruanda,Malawi au Kenye wana hitaji wapiga majungu uamuzi ni wako.
Hapa ni kazi tu.
 
Hakuna kitu kibaya Mpwa kama kutojiandaa kimaisha, unategemea blaa blaa ndio uishi, ni hatari sana, kwamfano nanihii akiondolewa kwenye Uwaziri leo hii ataishije? au kwa mfano wale Wakuu wa Mikoa na Sefue pia wataishije thereafter? Labda kama walikua na plan B ambao wengi wao kwa kweli hawana. Matokeo yake ndio haya kuwa mropokaji japo kutoka moyoni mwangu kabisa nashindwa kuamini kama ni kweli hii statement ni ya kwake.......huenda pia kuna mchezo wa kutuhamisha toka kwenye ishu ya uchaguzi wa Meya Dar na House Arrest ya Maalim Seif.
Mkuu nimetoka kumwandikia msg jamaa yangu sasa hivi,nikamwambia Mwapachu karudi CCM ila hoja zake zinaonekana wazee wengi waliokuwa na vyeo serikalini huwa hawajiandai kimaisha,kazi na biashara zao wanazipeleka kwa mgongo mkubwa sana wa serikali na hivyo hawapati ugumu wa maisha,kwa hiyo hapa Mwapachu anatufundisha vijana jinsi ya kuandaa maisha ya uzeeni na kuepeka kutegemea "upendeleo" wa dola ktk kuendesha maisha yetu...ni aibu sana kwa aina ya Balozi kuonge hivi mkuu Elli
 
nani naye huyu humu, sijaona kilichomfanya aondoke na kirichomrudisha zaidi ya kisebusebu na kiroho papo
 
Duh!!

Zipo taarifa za chini kwa chini zinazodai kuwa Balozi Juma Mwapachu ana mpango wa kurejea CCM. Mpaka sasa bado haijafahamika ni sababu zipi hasa zilizompelekea kufikia uamuzi huo.

Itakumbukwa kwamba wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana, Balozi Mwapachu alirudisha kadi za TANU na CCM na kutangaza kumuunga mkono aliyekuwa mgombea Urais wa CHADEMA, Edward Lowassa.

=======

UPDATES:

Hatimaye imekuwa kweli!

HOTUBA YA BALOZI JUMA MWAPACHU KUTANGAZA KUREJEA CCM

MIKOCHENI 16/03/2016

Ndugu zangu,

Mtakumbuka kwamba mnamo tarehe 13 Oktoba 2015, nilitangaza kuihama CCM na kurejesha kadi yangu ya uanachama kwenye ofisi ya CCM Kata ya Mikocheni. Nilitoa maelezo kwanini niliamua kujiondoa CCM (maelezo hayo pia niliyabandika katika ukurasa wangu wa facebook). Nilieleza kwamba CCM imepoteza mwelekeo kwa kuamua kumnyima haki ya kugombea mcha mungu Edward Lowassa. Nikasema Edward Lowassa ndiye chaguo la wana-CCM na ndiye chaguo la Watanzania. Nikasema nitakuwa mnafiki nikiendelea kubaki CCM huku naamini Edward Lowasa anafaa kuwa Rais kuliko John Pombe Magufuli.

Baada ya miezi miwili ya uongozi wa Magufuli nataka niseme nilikosea sana. Nililewa mahaba ya Lowassa, nililewa ahadi ya Lowassa kunipa uwaziri wa mambo ya Nje. Niliamini mafuriko ya Lowassa ambayo yakanifanya niamini kabisa anachukua nchi. Tulikubaliana na wenzangu kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa wimbi kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini baadhi wakaogopa na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo.

Leo natangaza kurudi CCM kwa sababu nimeona kazi nzuri ya Magufuli. Nimefanya kosa kubwa katika siasa ambalo nawasihi vijana kwenye siasa wasifanye. Nilihama kwa kwa sababu ya mtu (Lowassa). Nimerudi kwa sababu ya mtu (Magufuli). Nataka niwaahidi kwamba CCM ikiweka mtu hovyo baada ya Magufuli, sitahama. Usemi wa CCM kwamba Chama Kwanza, Mtu Baadaye sasa ndio nauona maana yake. Niliwalaumu CCM kwa kumuacha Lowassa lakini sikujua kwamba CCM ina uwezo wa miujiza wa kuibua jembe bora linaloitwa Magufuli.

Naomba mnisamehe kwa kulifanya jambo langu la kujitoa CCM na kurudi CCM kuwa jambo la kitaifa ukizingatia kwamba sikuwa na nafasi yoyote ya uongozi wa CCM wakati nahama na pia sijawahi kuwa hata Mjumbe wa NEC ya CCM na nilikuwa nje ya ulingo wa siasa za CCM kwa miaka 20. Niliamua kulifanya jambo kubwa ili kumsaidia Lowassa. Na sasa nimeamua kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwa sababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu.

Naomba radhi kwa familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa kuitumia kisiasa siku aliyokufa (tar 14 Octoba) na kutumia msiba wake kutoa kauli za kisiasa zidi ya chama chake alichokiunda na ambacho hadi anakufa alikuwa mwanachama.

Wananchi wote tumuombee Magufuli na tumsaidie kwani tumepata Nyerere mpya.

Mungu Ibariki Tanzania
mungu Ibariki Afrika

Balozi Juma Mwapachu
 
Sasa ndugu yangu una quote post ndefu halafu ulicho changia eti ni kuuliza 'mwapachu ni nani'...unaweza kucomment pasipo ku quote.
unaonaje Kama ugepita kimya
 
Ku stoop so low kwa Magufuli si hoja, watu wanafanya hivyo kila siku.

The trappings of power will bend the most principled person at times.

Stooping so low so publicly in a very humiliating way is quite another matter, as if the ambassador is totally devoid of any nuance.

As they say, 'the secret is in the pudding' na huyo Mzee amekuwa very generous with the truth. get this:

"Nililewa mahaba ya Lowassa, nililewa ahadi ya Lowassa kunipa uwaziri wa mambo ya Nje. Niliamini mafuriko ya Lowassa ambayo yakanifanya niamini kabisa anachukua nchi. Tulikubaliana na wenzangu kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa wimbi kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini baadhi wakaogopa na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo".
 
"nataka niseme nilikosea sana. Nililewa mahaba ya Lowassa, nililewa ahadi ya Lowassa kunipa uwaziri wa mambo ya Nje. Niliamini mafuriko ya Lowassa ambayo yakanifanya niamini kabisa anachukua nchi. Tulikubaliana na wenzangu kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa wimbi kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini baadhi wakaogopa na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo."

Hahahahaaaaaa uwiiiii mwehu karogwa tena
 
....... nililewa ahadi ya Lowassa kunipa uwaziri wa mambo ya Nje.

.......Lakini baadhi wakaogopa na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo.

......Na sasa nimeamua kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwa sababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu.

...................................................................................
ala kumbe??

hongereni CCM mmepata mtu. atawafaa sana huyu!
Hapo kapiga pasi ndefu inayomhusi ndio atajua cha kufanya!
 
Siasa za Tanzania hatari, tulisema watu walihama CCM kwa sababu ya uchu wa madaraka watu hawakuelewa, walipokelewa na kufanywa makamanda na wao kuwa nembo ya mabadiliko badala ya wale waliyoyapigania mabadiliko kwa mda mrefu.

Sasa tusubili mzee mzima kurudi mavumbini alikotoka, maana yeye ni mavumbi.
 
As they say, 'the secret is in the pudding' na huyo Mzee amekuwa very generous with the truth. get this:

"Nililewa mahaba ya Lowassa, nililewa ahadi ya Lowassa kunipa uwaziri wa mambo ya Nje. Niliamini mafuriko ya Lowassa ambayo yakanifanya niamini kabisa anachukua nchi. Tulikubaliana na wenzangu kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa wimbi kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini baadhi wakaogopa na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo".
hata slaa alizungumza makavu kuliko hayo
 
Mtu mzima, tena msomi na mwandishi wa kitabu cha Uongozi/Utawala, na zaidi ya yote mwanadiplomasia, anapokosa kuwa na msimamo tunamwiitaje!? Tukisema ni kibaraka waungwana watamshangaa, na ukimwiita mnafiki marafiki zake watamwogopa kama ukoma. Sasa tumwiiteje. Nadhani inatosha kusema ni mmoja wenye akili finyu zisizoweza kufanya uchambuzi wa mambo, ambaye kama mkristo, Yesu angemwambia hajui atendalo. Hata hivyo, mimi simshangai maana hata wakati wa siasa ya Ujamaa alikuwa critic wa mfumo ule; lakini leo anamfananisha Rais JP Magufuli na Nyerere, mwasisi na mtetezi wa mfumo huo wa Ujamaa. Linalonisikitisha ni kwamba Taifa lilipoteza raslimali zake kumsomesha mtu ambaye hakuweza kuelimika japo alipitia elimu ya juu! Chama kiwe na tahadhari naye.
 
Mh Rais. Tunakupongeza kwa kazi nzuri unalolifanyia Taifa. Wengi wa waliokimbia ccm walikupomba kuwa wewe ni manager wala siyo leaders. Inakuwaje miezi minne tangu ushike Madaraka ndo wajidai kurudi? Kuwa makini na watu hawa. kwanini wanaorudi wameanzia Arusha na leo huu Mwapachu anasema mara biashara za wenzao zisibuguziwe kwani wameomba Radhi. Magufuri kuwa makini, kwanini waibaki hukohuko? ni vizuri pia ainisha wale wote waliokuwa against kuteuliwa kwako halafu leo bado wanashikiria vyeo ndani ya Chama na Serikali, Watu wa aina hii watakuhujumu kwa njia moja na nyingine. Ungekuwa bora kutowakaribisha kwenye vikao vyako au vyeo unavyopanga vya Kiserikala. Si watu wazuri kwa Mstakabili wa uongozi wako.
 
"Sitaki shughuli zangu na washirika wangu zikwane kwa sababu sijaiunga mkono CCM" Hii ni statement nzito sana.
Kumbe kama umemuu ga mkono Magufuli na ccm basi shughuli zako na washirika wako haziwezi kukwama. Huyu ni balozi na mtu mzima hawezi kusema hayo kwa kuropoka ni kuwa huo ndio ukweli anaoujua na kwamba kumbe Magufuli anaposema atatumbua biashara zote haramu bila kuangalia Mtu ni UONGO NA ULAGHAI hilo linawahusu tuu wale ambao hawakumuunga mkono.
Mwapachu amesaidia sana kueleweka kwa serikali iliyopo kuwa ni ya ushikaji na ushirika na sio vinginevyo.
Tunawashauri wale wote wapiga dili, magendo na biashara haramu warudi kwao ccm watuache sie tusio na ushirika bali mshikamano wa wanyonge wa nchi tuendelee kutafuta mabadiliko katika hali hihii ya kunyanyaswa na kuonewa mpaka kitakapo eleweka.
Asante Mwapachu kutufungua macho, ila umefedhehesha kizazi chako chote na utashusha mvi zako kwa fedheha kuu kaburini siku yako ikifika
 
image.jpeg
image.jpeg

Kwa hiyo kumbe Lowassa alishapanga baraza lake la mawaziri?Kwamba Waziri wa Mambo ya Nje asingekuwa mbunge wa CHADEMA bali kada wa CCM aliyehama na kubaki "bila chama".....Kwa hiyo huyu Waziri Kimvuli Msigwa asingekuwa waziri wa Mashauriano ya kigeni?Kwamba Lowassa hakuona mwenye sifa ndani ya chama alichohamia?
Kumbe Mwapachu aliondoka sbb ya cheo na anarudi sbabu "Biashara zake na washirika wake" ziende vizuri...hii nchi inaliwa sana hii,yaani mtu anatafuta nafasi ya kisiasa ili biashara zake na washirika wake ziende vizuri??Mbowe Mbowe Mbowe umesikiaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom